Yesu akirudi leo atasali wapi? Kwa Wayahudi, RC /Wasabato au Kwa Walokole? Au Mashahidi wa Yehova? Naomba majibu

Yesu hata zamani alikuwa anasali ila alikuwa hafuati sheria za Kiyahudi, bali alifuata maelekezo ya aliye mtuma. So yy sio mtu wa kufungamana na Imani,bali Mungu aliye mtuma.
 
Atakuja tena jwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu. Nao ufalme wake hautakuwa na mwisho.


Yesu Kristo atarudi kama alivyosema na akirudi hasali. Atafanya hayo niliyoeleza hapo juu.
 
Sasa mnamwita Mu gu halafu unauliza atasali wapi sasa asali ili iweje wakati mnaamini ni Mungu.
Yani wewe ujiombe mwenyewe
 
1 Wakorintho 12:3,12-13
[3]
Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
[12]
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.
[13]
Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
 
Sasa mnamwita Mu gu halafu unauliza atasali wapi sasa asali ili iweje wakati mnaamini ni Mungu.
Yani wewe ujiombe mwenyewe
Aliwahi kujumuika na wayahudi kwenye Sinagogi, akija atafikia wapi?
 
Unamaanisha dini zote ni viungo kwenye mwili wa Kristo?
 
Atakuja tena jwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu. Nao ufalme wake hautakuwa na mwisho.


Yesu Kristo atarudi kama alivyosema na akirudi hasali. Atafanya hayo niliyoeleza hapo juu.
Atahukumu akiwa wapi?Vatican au Israel?
 
Yaani hizi hadithi kuna watu wanazielezea wakiwa serious hadi wanasahau kama walikaririshwa nao wanawaambukiza wengine ukaririsho
 
Yaani hizi hadithi kuna watu wanazielezea wakiwa serious hadi wanasahau kama walikaririshwa nao wanawaambukiza wengine ukaririsho
Sorry bro Mimi sijidai kuwa mwema sana ila Nina uzoefu na amani ya Mungu. Sipo Kwa Yesu kwa sababu Kuna mtu aliniambia. Nilikutana nae mwenyewe, pia nikitenda dhambi utukufu wake ukiondoka nausikia kabisa. Na pia ukirudi nausikia. Sio habari za kusimuliwa wala ni habari za kweli. Fanya majaribio mwenyewe usidanganywe danganywe tu.
 
Kwanini, umekuwepo msisitizo wa dini yaani ukiwaambia watu namwamini Mungu watakuuliza unasali dini ipi? Ukiwaambia Mkristo watakuuliza dhehebu!!
Madhehebu ndio kitu ambacho sitaki hata kukisikia,unakuta watu Dini moja lakini wanabaguana sababu ya Madhehebu na kufuata mafundisho ya Madhehebu badala ya Dini. Leo unakuta kijana ni Moravian anataka kuoa binti wa Pentekoste,yaanza majungu utaoaje mtu ambaye sio Dhehebu letu,halafu haohao ndio wanakazia kuwa Dini imeagiza tupendane. Walioanzisha Madhehebu hawastahili msamaha kabisa
 
Kabisa inaonekana huu sio mpango wa Mungu, ni mpango wa kutugawa
 
Unasali wapi mkuu?
 
Yaani hizi hadithi kuna watu wanazielezea wakiwa serious hadi wanasahau kama walikaririshwa nao wanawaambukiza wengine ukaririsho
Mkuu wewe huamini uwepo wa Mungu?
 
Dini ni culture, alisali kwa wayahudi sababu alizaliwa kwenye culture ya kiyahudi.

Hivyo hata akija leo atasali popote pale ila mafundisho yake yatabeba kweli na sio culture ya dini, kama alivyofanya kwa wayahudi wakamsurubisha.

Hayo ni mawazo yangu na sio facts.
 
Kama dini ni tamaduni za mahali husika je, ni sahihi Sisi kufuata tamaduni za ulaya magharibi na Asia?
 
Mpaka sasa hivi Sina kanisa la kwenda. Niliondoka katoliki. Nipo namuuliza Mungu wapi nitalishwa.
Ukiondoka katoliki utagundua kila sehemu Kama inapwaya hivi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…