Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Inasemekana Prigozhin alikuwa agombee urais dhidi ya Putin.Putin ni muuaji kabisa.Hivi wanashindwa vipi yeye kumuua ?
Prigozhin sio presidential material kabisa na hakuwa tishio kisiasa za demokrasia. Yule ni criminal ana kesi zake nyingi na hana CV ya kumsimamisha juu ya serikali. Urusi ni nchi ngumu sana kuongoza sio kama Marekani mtu anatembea kwa tabu na anakuwa Rais
 
Nimeeleza taratibu za kawaida ambazo hufanywa na nchi hizi ziloendelea.

Lakini imethibitishwa rasmi kwamba Prigozhin ni miongoni mwa walokufa.

Wagner wenyewe wamethibitisha kupitia Telegram.
Na vingine wanavyovisema huwa unawaamini au Unaamini hili tu?
Wanataka uamini amekufa ulitaka wareport aje?
 
Na vingine wanavyovisema huwa unawaamini au Unaamini hili tu?
Wanataka uamini amekufa ulitaka wareport aje?
Nikiwa ni mmoja wa watu tunofuatilia kwa makini, binafsi nilikwishamwona Prigozhin kama "deadman Walking", hivyo si jambo la kustua sana kwa wanofahamu.
 
Kwa ufupi:
1. Admiral Nikolai Kuznetsov aliyeipigania nchi kwenye vita ya pili ya dunia akiongoza jeshi la majini baada ya vita alifukuzwa kazi mara mbili jeshini, kushushwa vyeo na kufukuzwa tena kazi na kuwekwa marufuku kujihusisha na jeshi la maji mpaka anakufa. Miaka kama 10 baadaye veterans na baada ya viongozi waliomfanyia vile kubwa wamekufa na wamestaafu ndio wakashinikiza serikali irudishe heshima yake akiwa marehemu.

2. Stalin aliua majenerali wengi jeshini kwenye Great Purge akihofia wenye uzoefu, uwezo na ushawishi watampindua. Aliua majenerali, wanasiasa, wahadhiri na kila sekta muhimu watu zaidi ya laki saba mpaka operation inaisha kama 1936 hivi. Ukitaka kujua madhara yake, vita na Finland walifanya vibaya sana sababu majenerali waliuwawa na wamefungwa wamebaki ndio mzee na wasio na uzoefu. WW2 inaanza Stalin akalazimika amtoe Konstantin Rokossovsky jela maana vilaza hawawezi ongoza jeshi na huyo jamaa akawa kati ya watatu muhimu kwenye jeshi vita ile.

3. Marshal Zhukov alifutwa vyeo baada ya kuwa maarufu vita ya pili ya dunia, akapelekwa uko mbali na akaja kurudishiwa vyeo baada ya Stalin kufariki.

4. Baada ya Stalin kufariki, mkuu wake wa usalama alihukumiwa kuuwawa wakiwa kwenye kikao cha kwanza cha kutafuta mrithi. Hapohapo kasomewa mashtaka na mtu asiye jaji, hakutakiwa kujitetea na akauwawa. Lavrentiy Beria alikuwa na roho mbaya sana yule, na aliuwa wengi yeye mwenyewe.

5. Putin alivyokuwa Rais alimuua mpinzani wake na aliyekuwa mwanasiasa makini zaidi ambaye alitakiwa ndio arithi badala ya Putin ila alikuwa mkali na amenyooka. Aliuwawa mtaani mjini Moscow mchana kweupe. Assume Lowassa alikuwa the best kuliko Magufuli, Magu achaguliwe na mafisadi, baadae aue upinzani na Lowassa apinge hiyo hatua, Magu amuue Lowassa.

6. Yuri Gagarin yule binadamu wa kwanza kwenda space alikufa kwa ajari ya ndege. That time astronomer ndio mtu wa maana sana nchi ile na anayeonekana ana akili sana. Yuri Gagarin akawa maarufu kuliko wanasiasa, wakamuua.

7. Kabla ya Sergei Shoigu kuwa waziri wa ulinzi, kuna Anatoly Serdyukov alikuwa waziri. Aliwekwa hapo baada ya Russia kufanya vibaya vita ya Georgia kanchi kadogo sana Kusini pale, na wakati huo jeshi lilitoka kufanya vibaya kwenye vita za Chechens ikaonekana hata kama inatakiwa ndiyo mzee, jeshi limeoza. Serdyukov alifanya makubwa sana ndani ya muda mfupi, huyo alichukiwa na wala rushwa wote na alikuwa very competent akaondolewa. Mageuzi aliyoianzisha yamelisaidia sana jeshi.

Hawa wapinzani wengine na waandishi wa habari wanaopewa Novichok na Polonium tuachane nao, nazungumzia mtu aliyeteuliwa na serikali akafanya kazi yake kwa ufasaha na aka-outnishe wakubwa. Usidhani IT specialists, developers, tech gurus, lecturers na wanasayansi wakubwa wanaokimbia Urusi ni wajinga. Nchi haina meritocracy kabisa ile.
Asante kwa maelezo haya
Vipi kuhusu huyu mwamba nae naona watamla kichwa nae Gen Surovikin huyu nae vipi
Unaujua ushawishi wa South Africa ndani ya AU? Unaujua ushawishi wa South
ICC hawakumuadhibu wakati huo Al Bashir alipokuja SA hilo.ndio nimeuliza mkuu kulingana na hoja yako
 

Attachments

  • Screenshot_20230823_214737_Chrome~2.png
    Screenshot_20230823_214737_Chrome~2.png
    198.9 KB · Views: 2
Wafuasi wake wanasema kauliwa na kombora la warusi.
Prigozhin maadui wake wakubwa walikuwa ni jeshi la Russia na wizara ya Ulinzi ya Russia.

Baada ya lile jaribio la uasi hawa walikuwa wakilalamika sana kwa Putin kwamba kwanini jamaa aachwe awe atembea tu akiwa huru.

Hivyo huenda pia Putin hausiki na hili lakini ni system ya ujasusi ndio itakuwa mtuhumiwa namba moja.

Haiwezekani taarifa ya abiria wa ile ndege iwe ipo available mara tu baada ya ajali.
 
Huyu mzee alianza kuzeeka vibaya. Hata mimi nisiyejua kwa undani mambo ya UHAINI nilijua tu kuwa mzee amefanya kosa kubwa ambalo kichaa Putin hawezi kumsamehe. Angewauliza wanajeshi wa Niger kwanini hawarudi nyuma na mapinduzi yao. Wanajua tu kuwa wakimrudisha raisi aliyepinduliwa madarakani basi wao watakufa kama senene. Yeye alishindwa kuyajua haya? Putin ameamua kumwondoa kabisa na baadae kidogo na Putin naye atakufa.
 
Kawaida mbona baadhi ya vifo vichache vya wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine havitajwi kuepuka kulipa fidia nyingi. Wakiona hoehae wanatupa uko hujulikani ulienda wapi. Mtoto wa maskini umetoka Tula vijijini uko mpakani familia yako itaandamana saa ngapi.

Ila private jet ni ya Prigozhin ingawa hakuna confirmation kutoka serikalini kwamba alikuwemo, kilichotajwa ni kwamba kwenye passengers list yupo. Labda kuna muujiza alisitisha safari kabla dakika za mwisho.
Magulyati
 
Hakufanya kosa usimlaumu. Mambo mwishoni hapo yalikuwa ni ya kulazimisha kila option ni ngumu.

1. Kundi lake linateketea kwa uzembe wa wakuu wa wizara ya ulinzi, asipolitetea litamuua lenyewe.

2. Katetea kundi lake wakuu wake wakaona wakimpa kila anachotaka atafanya vizuri na credit apate kisha atishie maslahi yao, wakambania.

3. Akafokea wakubwa zake na kuwaita wasaliti na wazembe, wakamchukia zaidi. Makamanda wa jeshi ndani humo wengi tu wanamkubali.

4. Mwezi June pale Shoigu akafanya mpango wa kumuua Prigozhin ukafeli, akaona hana cha kupoteza wacha ajaribu maana vyovyote vile ashakuwa wa kufa.

5. Akafanya mutiny akiamini ataungwa mkono na majenerali wa Urusi ambao hawautaki uongozi wao mbovu wa kijeshi maana unafelisha vita na kuifanya iwe ndefu sababu uko incompetent. Wagner ikafanya safari kutoka mpakani siku nzima hakuna kikosi kimejitokeza kuizuia (kulikuwa na kamgomo baridi jeshini). Wakajitokeza jeshi la anga wachache na helicopters zao na relay aircraft zikadunguliwa.

6. Serikali ikawa kama haiamini ikalipua vituo vya mafuta njiani na kuchimba mahandaki barabara ya kuingia Moscow upande walipokuwa Wagner na kikosi maalum kikakaa kuwasubiri. Jioni ile mazungumzo yanaendelea baina ya Prigozhin na serikali, yakashindikana sababu Putin hakutaka kumuondoa Shoigu kama Prigozhin alivyotaka.

7. Jioni ile baada ya kuona hakuna uungwaji mkono na majenerali wengine wa jeshi (hawa kina Surovikin na wengine ambao walikuwa wanasoma upepo, na watauwawa wengine hii pigia mstari kabisa) ndipo Prigozhin akaona hawezi fika Moscow. Akakubali ofa ya kwenda Belarus ila akaweka sharti la kufutiwa mashtaka hivyo asingeweza shtakiwa.

Prigozhin alifanya uasi kwa kulazimishwa, ile attempt ya kumuua mapema ingefanikiwa asingefika kote uko. Na alijua hana uwezo wa kupindua nchi, ila kushawishi majenerali wengine ndio wafanye mapinduzi. Na wanaomlaumu kwanini alikuwa uraiani, sasa Belarus na Moscow tofauti yake nini yani unaikimbia serikali ya Marekani unaenda kuomba hifadhi Uingereza? Si ni sawa na kukimbia kwa baba kwenda kwa babu, baba akikutaka si anakufata na kukuchukua.
Black Sniper soma hapa kuhusu Surovikin. Inavyosemekana Surovikin alijua taarifa za uasi wa Prigozhin akakaa kimya hakutoa ripoti. Baadae kinafiki alipokwishafanya assesment na kuhisi mpango utafeli ndipo akatuma video mtandao live ya kumuomba Prigozhin asitishe uasi. Wale ni marafiki na inajulikana hivyo, ila hii move inaonekana kama alikuwa anaandaa mazingira ya baadae either kujikataa au kuunga mkono. Nadhani kati ya watu Prigozhin alitarajia wamuunge mkono wa kwanza ni yeye sababu pale juu jeshini wapo Waziri Shoigu na Chief of General Staff, General Gerasimov ambao wawili hawa ni watiifu kwa Putin ila wanalaumiwa kuwa wabovu kiuongozi.
Vyeo vya deputy ministers of defence vipo kama saba hivi ila havina ngumu kimakusudi. Mwenye sifa na anayependwa jeshini ni General Surovikin. Kashaondolewa nafasi yake na hajulikani alipo.
Bado General Sergey Surovikin wa Aerospace Forces ambaye ameondolewa cheo baada ya kufichwa tangu sekeseke la Wagner.
Taratibu za vifo vya vigogo wa Urusi huwa ni zilezile, sumu kwenye chai, kudondoka kutoka ghorofani, ajali hasa za magari, kujiua kwa aina mbalimbali.

Tiyari General Gennady Zhidko aliyeongoza operation nzima mwanzoni akaja kuondolewa kwa performance mbovu amefariki wiki iliyopita kwa "ugonjwa wa muda mrefu"View attachment 2726575
Huyu ndiye aliyeondolewa kuongoza majeshi ya Urusi nchini Ukraine na akaletwa Surovikin, na Surovikin akaondolewa vilevile.
Wiki hiyohiyo ya jana General Gennady Lopyrev alifia jela alikokuwa amefungwa kwa miaka kadhaa kwa kesi gani sijui. Huyo alikuwa kikosi cha kumlinda Putin.

Majenerali wa Ukraine hawa hapa kina Budanov hawaumwi hata mafua na kichapo wanaendelezaView attachment 2726580
 
Back
Top Bottom