Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Huyu mzee alianza kuzeeka vibaya. Hata mimi nisiyejua kwa undani mambo ya UHAINI nilijua tu kuwa mzee amefanya kosa kubwa ambalo kichaa Putin hawezi kumsamehe. Angewauliza wanajeshi wa Niger kwanini hawarudi nyuma na mapinduzi yao. Wanajua tu kuwa wakimrudisha raisi aliyepinduliwa madarakani basi wao watakufa kama senene. Yeye alishindwa kuyajua haya? Putin ameamua kumwondoa kabisa na baadae kidogo na Putin naye atakufa.
Eti putin naye atakufa hujitambui.
 
Angeenda ingemweletea shida SA hata kuwekewa vikwazo, ilikuwa mtego lkn hakuna wa kumkata hakiwa SA
Wanawaza karibu sana hao wanaosema Putin angekamatwa akiwa SA, kitendo cha kumkamata Putin ndani ya nchi yoyote ni kumtangaza vita na Moscow na Urusi itamtoa kafara Putin lakini hiyo nchi itajiandaa kuua mamilioni kama sio mabilioni ya watu
 
Anazidi kujiletea matatizo tu
Isome kwanza historia ya Urusi ndio ukomenti, yaani kabisa Urusi ipate matatizo Kwa sababu ya huyo mkuu wa Wagner? Kama ni kuwaza, jaribu kuwazua Zaidi.

Hapo Russia imepeleka ujumbe Kwa wote wanaofikiri Moscow ni pepesi kiasi hicho na hapo katika lugha ya picha wanasema kuwa ukicheza na Moscow umecheza na moto.

Kifupi nimefurahi sana, Kila siku yanatolewa maonyo na Urusi juu ya wanaotaka kujaribu kufanya jaribio lolote ndani ya Urusi lakini hawaeleweki, naamini Kuna siku dunia itaandika historia ya kilio kikubwa sana.

Endeleeni kufurahia tu, oooh! Superpower wa mchongo anapigwa na Ukraine ,mara oooh! Drone za Ukraine zimepiga ndani ya Urusi, mara oooh! Kuna siku hiyo oooh! Itasikika uwiiiiii

Kila siku sisi tuliojalowa jicho la hekima tunaona Ukraine anajiingiza kwenye hatari tena kubwa sana na ningepata nafasi Leo ya kumshauri Zelensky Rais wa Ukraine ningemwambia hivi ACHA KUCHEZA NA MOSCOW NA HIZO DRONES ZAKO KUNA SIKU UTALIA KILIO KIKAVU.
 
Unao uhuru wa kuandika yaliyotokea ukiwa kwenye tukio
Nimesoma majibu yako na mifano uliyoitoa sikumbuki kuwafahamu so siwezi sema chochote.

ila tukiielewa historia ya Russia, ndio utaelewa kwanini iko hivi ilivyo leo.

Russia kwa muda mrefu Imekuwa ni military state, Kwa sababu ya utawala wa kifalme na Mavamizi/matishio ya kutokea nje-napoleon, hitler, NATO. So taifa la dizaini hiyo, unaweza elewa mtazamo wa watawala dhidi ya wapinzani. Hatari ya historia ya mavamizi, huzaa ufisadi na ubwenye. At least baada ya Putin kuingia for 20 yrs amedhibiti power struggle iliyokuwepo kwa miaka mingi. Kwa ufupi Russia bado ni taifa linalojitafuta kuelekea kuwa taifa la 'kisasa' zaidi.

Comperatively, Marekani ina bahati kubwa ya kijiografia. BAHARI. Kuzungukwa na bahari, imeifanya kuwa na jeshi imara la majini, hivyo kuwa ngumu kuvamiwa na rahisi kujilinda.
 
Acha naye huyo, Kuna mwenzake alianzisha Uzi eti " Kuangalia taarifa ya habar ni kutafuta umbea".
kuna mmoja nimemkemea vikali hivi punde baada ya kunitaka nibadilishe chaneli akinishangaa kwa nini natazama taarifa ya habari huku akiniuliza inasaidia nini hiyo taarifa ya habari?
 
Nashangaa watu wanaomsifia Putin ni mwamba kumbe jamaa muoga sana anashinda ndani tu.angeenda south Africa
Kiongozi mwenye busara anatakiwa kuongoza kwa kutumia busara na akili na sio nguvu na Moja ya busara kubwa ni kuacha hata kama una uwezo wa kufanya na kunyamaza hata kama una uwezo wa kuongea.

Jaribu kufikiri Zaidi ya hapo unapofikiri ili uione busara ya Putin:

Kama angeamua kwenda na lingefanyika jaribio la kutaka kumkamata ndani ya SA, unadhani Russia ingekaa tu na kutulia kisa SA ni mshirika mwenzake? Jibu, ni hapana angetumia nguvu na hata angeweza kuipiga vibaya SA lakini Kwa kutokwenda kwake SA imepona. Hiyo ni busara kubwa mno

Fikiria Zaidi, kama Kila nchi inaogopa kuingia kwenye mgogoro na Russia ambao utapelekea kuwa vita ,kama angeenda na kukamatwa SA maana asingepelekwa nchi nyingine na SA ingeachwa kama Chambo, kitendo ambacho ni hatari Kwa usalama wa SA.

Nakuhakikishia jambo Moja ,sio Kwa sababu nina uhakika nalo ila Kwa sababu naamini Russia atalifanya, siku Putin akipewa mualiko kwenda Uingereza, Ujerumani au Ufaransa ataenda vizuri na watampatia ulinzi wa kutosha Kwa sababu wanajua kitakachofuata.
 
Unao uhuru wa kuandika yaliyotokea ukiwa kwenye tukio
Pia umezungumzia kuhusu Urusi kushindwa na Finland, chechen na Georgia. Sijui wewe vita huitazama vipi, but kwangu mimi vita ni matokeo ya nani anapata nini baada ya vita kutokana na malengo. Mfano, lengo la US ilikuwa ni kuilinda dola dhidi ya tishio la Gadafi, so licha ya kumuua gadafi, ameiangamiza kabisa libya kiuchumi-haitokuja tena kuwa tishio kwake. So, amefanikiwa.

Finland alisurrender mara zote mbili na kukubali kuachia ardhi yake kwa Soviet, achilia mbali maamuzi ya fedheha ya kukubali kuwashitaki na kuwafunga wanajeshi wake wenyewe waliopigana dhidi ya uvamizi wa soviet. Sawa na leo ukraine iwashitaki majenerali wake eti kwa kosa la kuzuia uvamizi wa Urusi.

Georgia kusini hadi leo iko chini ya Urusi.
 
Hivi hii outsource sio tu kifuniko cha kuificha urusi na uingizaji wa jeshi nchi za wengine.TUNADANGANYWA SANA ILA MI NAONA NI KITENGO KAMILI CHA JESHI LA URUSI.ni mawazo yangu lakini.
Uko sahihi, ila kiutawala inakuwa imejipunguzia majukumu, na hayo majukumu kuhamishiwa kwa kampuni binafsi (wabobezi wa vita) ambao wanalipwa na utawala.

Kwa namna nyingine, utawala wao unakuwa umewapa maazimio hicho kikundi, nini wanataka yawe matokeo.

Ni sawa na wewe uingie mkataba na hicho kikundi, ukitaka kikalinde labda Niger; kwa hiyo wewe majukumu yako yatategemea na maazimio ya mkataba, je ni kuwapa silaa na fedha, usafiri, chakula n.k

Tunahitimisha; kwa sababu wameajiriwa na Urusi kwenye hayo mapigano na wanalinda maslai ya Urusi, kwa hiyo anayepigana pale ni mrusi.
 
Back
Top Bottom