Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Ifike mahali wakizusha ikabainika sio kweli wakione cha mtema kuni

Walimzushia Sabaya, kaonekana mzima hana hata dalili na bila aibu wapo tu wanadunda
Ndio maana SABAYA alionekana pale msibani akilia sana, NADHANI kwa hofu.
Lakini baada ya ka-mwezi kupita akaanza kutamba hadharani.
 
Yaani inaudhi tumepitia huku kila baada ya miezi kadhaa sijui wapi wanaombea au kumngojea Rais aumwe? Ili kiwe nini?

Kama anaumwa vya kutisha mnasema, kama ni uzushi mnasema na hata kumwonyesha kama alivyofanyiwa Dr. Mpango.

Nililisema hili hata wakati wa zile tetesi nyingine wakati ule. Rais ni Mwanadamu, hata kama wakati mwingine anazungumza kama mwenye ufunguo wa mbinguni. Mwisho mtasababisha taharuki isiyo ya lazima na kufanya watu wamposti Mama Samia tena.

Kama anahitaji kuinuliwa katika maombi huu ndio wakati. Kama hakuna jambo serious mnasema hivyo nakerekaga kweli.

===

UPDATE 12.03.2021:

Waziri Mkuu atoa kauli: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni?
Tulinyimwa wasaa wa kumuombea Lissu , tukanyimwa kumuombea JIWE maana hatukuambiwa alipo, tena wakubwa wakatwambia yupo mapumzikoni, mara yupo salama, mara ametoa fedha za maendeleo.

Kuvaa Flana ya "Pray for Lissu" ilikuwa ni jinai na watu waliwekwa ndani, yani hii nchi inahitaji malaika ashuke na moto, kuna watu wana roho mbaya kuliko shetani , alafu wanajigamba kutembea na VX.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom