Katika pitapita zangu mitaani leo nimepita sehemu mbili za vijiwe ambazo ni garage na sokoni sitasema zllipo. Sehemu zote mbili nimekuta mabishano mazito kuhusu wapi alipo rais na hali yake ya kiafya. Mabishano yamekuwa makali kiasi cha kukaribia kushikana. Kwa bahati mbaya ubishi wenyewe una mwelekeo wa kisiasa.
Ombi langu kwa serikali yangu pendwa iliyowekwa madarakani kwa kura za wananchi ijitokeze hadharani watu wakate hii kiu waliyo nayo ya kutaka kujua alipo rais wao na hali yake. Waziri mkuu, mkuu wa mkoa Mbeya na balozi wetu Namibia wote wanejaribu kujibu maswali hayo lakini majibu yao siyo rasmi ndiyo maana vyombo vya habari hususan vya nje bado vinaendelea kuuliza.
Jibu rahisi ambalo lingezima kelele zote hizi ni kwa rais kujitokeza na angalau kuwasalimia wananchi kama tulivyozoea kumwona.
Hao wanaokamatwa kwa uzushi ni katika kujaribu kujibu haya maswali. Wanaotoa majibu mitandaoni ni rahisi kuwafutilia na labda kuwanyamazisha je hao wa mitaani na vijiweni ambao ni wengi zaidi wanafuatiliwaje na kudhibitiwaje?