Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Katika pitapita zangu mitaani leo nimepita sehemu mbili za vijiwe ambazo ni garage na sokoni sitasema zllipo. Sehemu zote mbili nimekuta mabishano mazito kuhusu wapi alipo rais na hali yake ya kiafya. Mabishano yamekuwa makali kiasi cha kukaribia kushikana. Kwa bahati mbaya ubishi wenyewe una mwelekeo wa kisiasa.

Ombi langu kwa serikali yangu pendwa iliyowekwa madarakani kwa kura za wananchi ijitokeze hadharani watu wakate hii kiu waliyo nayo ya kutaka kujua alipo rais wao na hali yake. Waziri mkuu, mkuu wa mkoa Mbeya na balozi wetu Namibia wote wanejaribu kujibu maswali hayo lakini majibu yao siyo rasmi ndiyo maana vyombo vya habari hususan vya nje bado vinaendelea kuuliza.

Jibu rahisi ambalo lingezima kelele zote hizi ni kwa rais kujitokeza na angalau kuwasalimia wananchi kama tulivyozoea kumwona.
Hao wanaokamatwa kwa uzushi ni katika kujaribu kujibu haya maswali. Wanaotoa majibu mitandaoni ni rahisi kuwafutilia na labda kuwanyamazisha je hao wa mitaani na vijiweni ambao ni wengi zaidi wanafuatiliwaje na kudhibitiwaje?
 
Katika pitapita zangu mitaani leo nimepita sehemu mbili za vijiwe ambazo ni garage na sokoni sitasema zllipo. Sehemu zote mbili nimekuta mabishano mazito kuhusu wapi alipo rais na hali yake ya kiafya. Mabishano yamekuwa makali kiasi cha kukaribia kushikana. Kwa bahati mbaya ubishi wenyewe una mwelekeo wa kisiasa....
Yaani Tundu lissu, Mnyika, salum mwalim, Gwarugwa plus Faru John utegemee kupata taarifa reliable kweli du chadema majanga matupu. Hongera Halima &co kwa kujitambua, hata hivyo mmepoteza muda wenu sana huko
 
Raia wamewekwa korokoroni kwa kile kilichoitwa 'uzushi' na uzushi huu uliletwa na ukimya wa serikali.

Kwanini? Kwasababu tuliaminishwa kuwa haumwi na wengine wakaenda mbali kwa kusema 'wameongea kwenye simu' na wengine wakasema 'anatusalimia'

Hamkutoa taarifa za kuugua lakini mmetoa taarifa za msiba, hii siyo sawa.
 
Ndoto Niliyoota Leo.

Kiongozi wetu Mkuu wa Nchi alikuwa kwenye ukumbi fulani akigawa Zawadi kwa Watu mbalimbali.
Akatoa tangazo kuwa pamoja na Yeye kuwapa Hao watu Zawadi kutokana na utumishi wao, hata yeye alistahili Zawadi lakini ameamua kutupatia watanzania Wote Zawadi!

Zikaandaliwa Ngoma Kadhaa na Kisha Mkuu akachukua vijiti na kuanzia kutoa Burudani kwa kupiga Ngoma huku akicheza.

Katika kuonyesha uzoefu wa kucheza alitoa ile staili ya kuruka na kutua na makalio/matako ile anatua chini hakunyanyuka. Ndipo wakaanza kumuita lakini hakuitika, shika hapa na pale lakini hashtuki! Ikabidi wambebe kumtoa nje nadhani kumpeleka hospital. Na Nikashtuka Usingizini.

Ninakemea Roho Ya Mauti kea Viongozi wa Nchi Yetu. Na ikitokea Bwana umewaita, wajalie Kifo Chema. Ila si nipendavyo mimi bali upendavyo wewe.
Mapenzi Yako yatimizwe.

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.
Hatimaye Bwana Umemuita kwa mapenzi Yako
Jina lako lihimidiwe.
 
Yaani una maana hospitali kubwa kama KNH inakataa kupokea wagonjwa kwa sababu yupo Magufuli! Yaani huo ni uongo kupita kiasi. Mtamuombea ugonjwa mtaugua nyie, mtamuombea kifo mwishjo mtakufa nyie. Acheni uzushi na chuki!
🙄🙄🙄
 
Yaani Tundu lissu, Mnyika, salum mwalim, Gwarugwa plus Faru John utegemee kupata taarifa reliable kweli du chadema majanga matupu. Hongera Halima &co kwa kujitambua, hata hivyo mmepoteza muda wenu sana huko
🙄🙄🙄
 
Olushangiliaga, ogaluka hangi obiza okunombela nang'ho hangi ihaha?
Wapinzani wa bongo raha sana,ukiwakuta wanavyolalamika sasa mara sijui wanauliwa mara vile mara vile. Ila hao watu wenyewe sasa wanaolalamika ndio kwanza wapo busy kuzushia watu maradhi na vifo yani ndio mambo ya msingi kwao.
1
 
Inavyoonekana, kati ya watu walioshadadia sana kupotea huku kwa Magufuli kwa sasa, wakiwemo Tundu Lissu, yule Chahali, na Kigogo, hawana taarifa za uhakika juu ya whereabouts za bwana mkubwa pamoja na hali yake ya kiafya.

Ndo maana unaona walianza na Nairobi, wakaenda na India, wakabadili gia angani na kuelekea Jerumani kabla ya kurudi Mzena. Kesho sijui wataenda wapi. St. Thomas hospital, labda.

Mimi binafsi sijui chochote kuhusu alipo na yu hali gani.

Popote alipo, naombea awe ni buheri wa afya tele.

Kitu ambacho nimekiona kwa wengi waliotoa maoni yao, wengi hao wanaamini kilichomsibu bwana mkubwa ni corona na si kitu au jambo jingine.

Wengi hao wanaosadiki na kubashiri kuwa ni corona, madai yao ni kwamba ama imemuua au imempelekesha sana hadi kumfanya alichungulie kaburi.

Kwa vile mimi sijui kinachomsibu, nimeziweka huru fikra zangu na nimeepuka kuhitimisha. Siwezi kuhitimisha kitu au jambo ambalo sina hakika nalo.

Yawezekana bwana mkubwa kweli alipatikana na corona. Yawezekana labda kagundulika ana saratani. Yawezekana ana matatizo mengine tu ya kiafya yasiyohusiana na corona.

Licha ya hivyo, naelewa kwa nini watu wanasadiki wanavyosadiki.

Ni kwa sababu kuna ombwe la taarifa. Ombwe hilo limetengenezwa na serikali. Hapo hakuna ubishi. Na palipo na ombwe la taarifa, watu watalijazia na walichonacho kichwani na moyoni mwao.

Hivyo basi, leo nimefikiria kitu, tuseme ubashiri wa kwamba ana corona ni wa kweli.

Vipi kama alishauriwa na madaktari aji quarantine kwa siku 14 au na zaidi kidogo?

Kwa vile yeye ni Rais, vipi kama waliona ni vyema kwa yeye kujitenga kuliko kukata mbuga na kuendelea na ratiba zake kama iliyo kawaida lakini si kwamba alikuwa mahututi kawekewa mashine ya kupumulia?

Manake si kwamba kila apatikanaye na corona anakuwa ni mgonjwa wa kulazwa kitandani.

Vipi kama hivyo ndivyo ilivyokuwa.
😆😆😆
 
Wapinzani wa bongo raha sana,ukiwakuta wanavyolalamika sasa mara sijui wanauliwa mara vile mara vile. Ila hao watu wenyewe sasa wanaolalamika ndio kwanza wapo busy kuzushia watu maradhi na vifo yani ndio mambo ya msingi kwao.
Wapinzani raha, wanazusha eeh, wanasingizia eeh, haya MATAGA
 
Wapinzani raha, wanazusha eeh, wanasingizia eeh, haya MATAGA
Ndio mkuu wapinzani wako busy na kuzushia watu maradhi na vifo, wangapi wamezushiwa vifo ila bado tunawaona hai? wangapi wamezushiwa maradhi ila tunawaona wazima?

Huyo Magufuli alizushiwa kachanjwa chanjo ya corona ila alipofariki wao wao tena wanazusha kafa kwa corona. Tuna wapinzani wa hovyo wasio na msaada wowote kwenye taifa ni wapenda umbeya wa kisiasa tu.
 
Ndio mkuu wapinzani wako busy na kuzushia watu maradhi na vifo, wangapi wamezushiwa vifo ila bado tunawaona hai? wangapi wamezushiwa vifo ila tunawaona wazima?

Huyo Magufuli alizushiwa kachanjwa chanjo ya corona ila alipofariki wao wao tena wanazusha kafa kwa corona. Tuna wapinzani wa hovyo wasio na msaada wowote kwenye taifa ni wapenda umbeya wa kisiasa tu.

ukiwa mfuasi wa upinzani bongo inabidi uwe na tundu kichwan na uwe tayar kubadilika mda wowote, yaaani mabosi wanaweza kuamka wakasema lowasa sio fisadi tena na wale praise team wakaendeleza ngoma
 
Ndio mkuu wapinzani wako busy na kuzushia watu maradhi na vifo, wangapi wamezushiwa vifo ila bado tunawaona hai? wangapi wamezushiwa maradhi ila tunawaona wazima?

Huyo Magufuli alizushiwa kachanjwa chanjo ya corona ila alipofariki wao wao tena wanazusha kafa kwa corona. Tuna wapinzani wa hovyo wasio na msaada wowote kwenye taifa ni wapenda umbeya wa kisiasa tu.
sasa walimzushia MBOWE nao ni CUF?
 
Yaani inaudhi tumepitia huku kila baada ya miezi kadhaa sijui wapi wanaombea au kumngojea Rais aumwe? Ili kiwe nini?

Kama anaumwa vya kutisha mnasema, kama ni uzushi mnasema na hata kumwonyesha kama alivyofanyiwa Dr. Mpango.

Nililisema hili hata wakati wa zile tetesi nyingine wakati ule. Rais ni Mwanadamu, hata kama wakati mwingine anazungumza kama mwenye ufunguo wa mbinguni. Mwisho mtasababisha taharuki isiyo ya lazima na kufanya watu wamposti Mama Samia tena.

Kama anahitaji kuinuliwa katika maombi huu ndio wakati. Kama hakuna jambo serious mnasema hivyo nakerekaga kweli.

===

UPDATE 12.03.2021:

Waziri Mkuu atoa kauli: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni?
Mzee habari yako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom