View attachment 1722460
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amemjibu Mwanasheria mkuu wa CHADEMA ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mh. Tundu Lissu na kumuonya vikali kwa kitendo cha kuulizia alipo Rais Magufuli na kama yupo salama kupitia mitandao ya kijamii. Dkt. Mwigulu amenukuu vifungu vya sheria vilivyovunjwa na Mh. Tundu Lissu na kusisitiza kuwa sheria inapovunjwa hakuna mipaka wala muda kupita. Aidha Dkt. Mwigulu amewaonya waropokaji wote kuzingatia sheria na kwamba serikali ipo kazini.
Dkt. Mwigulu alisema hayo kupitia mtandao wa instagram ambapo ameandika "Kiongozi wa Nchi sio Parishworker Kanisani wala sio Mzee wa Kanisa kwamba alipangiwa zamu na hakuonekana!, Kiongozi wa Nchi Sio Mtangazaji wa TV kwamba alikuwa na kipindi Ila hakuonekana! Kiongozi wa Nchi sio kiongozi wa jogging clubs kwamba anatakiwa kuwa tu mtaani kila siku na kurusha selfie. TUACHE UPUUZI UPUUZI HATA KAMA HATUNA JAMBO LA KUFANYA.
Umeichafua sana nchi umeshindwa, mmetamani tukwame mmeshindwa,Sasa mnaombea mabaya nchi yetu na Kiongozi wa Nchi yetu. SHERIA YEYOTE INAPOVUNJWA, HAKUNA CHA MIPAKA, WALA HAKUNA CHA MUDA KUPITA. KWA WANAOROPOKA ZINGATIENI KIFUNGU CHA 89 cha Penal code na 16 cha Cyber Crime, SERIKALI IPO KAZINI"
Hata hivyo Mh. Tundu Lissu ameonekana kukaidi onyo hilo na kuendelea kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika kupitia mtandao wa Twitter.