Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Eeenh Heee!

Atakuwa ni kiongozi wa ajabu sana. Hata Kim atakuwa hamfikii kwa staili ya namna hiyo!
Sijui hasa atakuwa anafaidika vipi na aina hiyo ya kuongoza nchi.
Unaacha watu wajiachie na kutoa sumu zao wanazobeba, na wewe hata hazikustui chochote!
Usishangae ndugu yangu...ushamba na ulimbukeni ndio desturi zake.
 
..kama bwana mkubwa ni mgonjwa, na hawezi kutimiza majukumu yake, they have to tell the nation.

..tena Ikulu wakiwa wametangulia kutoa taarifa kunakuwa hakuna uwezekano wa watakaofuata kuzusha uongo...
Katika mambo aliyofanikiwa ni kuua taasisi au kuzigeuza 'ndondocha'
Ameondoa uwezo wa watu kufikiri bila kujali viwango vyao vya elimu, ufahamu au weledi

Rais ni mtumishi wa taasisi ya Urais ambayo ni kamili. Katika mazingira kama ya leo, taasisi ilipaswa kujitokeza na kueleza nini kinachotokea ima kukanusha kwa ushahidi au kukubali na kueleza hali inakabiliwaje

Kuna nafasi za utumishi zinazohitaji busara na weledi, katika mazingira ya vyeo kwa kujipendekeza aina hiyo ya watu imetoweka. Kinachoendelea sasa ni mkanganyiko tu kwa jambo ililowazi, kanusha au thibitisha.

Sidhani kama ni suala la Gerson peke yake, hili ni kutokana na kufeli kwa taasisi nzima ya mawasiliano Ikulu, Ofisi ya Rais ,Msemaji mkuu wa serikali n.k. Ni kufeli kwa 'think tank' ambayo ingeweza kuziba ombwe la kufeli kwa taasisi.

Hatuna formal think tank, lakini wazee wazoefu na wastaafu wangalikuwa msaada katika hali iliyopo.
Nao pia kama taasisi wamefeli hawawezi kusimama kwa masilahi ya Taifa, wanaogopa yao.
 
Katika mambo aliyofanikiwa ni kuua taasisi au kuzigeuza 'ndondocha'
Ameondoa uwezo wa watu kufikiri bila kujali viwango vyao vya elimu, ufahamu au weledi..
Hii ndio maana halisi ya One Man Show. Maana yake taasisi hazifanyi kazi wote wanasubiri maelekezo ya mtu mmoja.

Hata kwenye hili ni hivyo hivyo,hawana cha kufanya mpaka wapate go ahead. Kwenye hili wamepigwa ganzi, kutetea wanashindwa kusema ukweli wanashindwa. Wakitetea wanahisi kuna matukio yatawaumbua
 
..kama bwana mkubwa ni mgonjwa, na hawezi kutimiza majukumu yake, they have to tell the nation.

..tena Ikulu wakiwa wametangulia kutoa taarifa kunakuwa hakuna uwezekano wa watakaofuata kuzusha uongo...
Mkuu, "situation is tight" lakini kitaja eleweka weekend.

Ila huwezi kuwalaumu Msigwa wala Mwigulu.

Kama wakumbuka uzuri ile ya mwaka jana kule home town ndio ilikuwa ni "shielding place".

Ila kila kitu kipo chini ya mikono salama.

Tuvute subira.
 
1615514995386.png
 
Hehehehehe moto unawaka huku jamani,, msema kweli ni mpenzi wa Mungu,Msemaji wa sirikali waambie ukweli taifa lako, ndugu zako_____kinachoendelea maana mnatuweka kwenye koma!!!
 
Aliyepaswa kwanza kunyamaza Ni nani. Mleta fununu bila picha au anayetuhumiwa bila kujua. Unapokuwa huna akili Basi ukimya ndo kinga. Je unatafuta katiba Ili kiongozi akisingiziwa na muhuni fulani Basi ajibu. Tuambie ibara ya ngapi tuiweke.
Naona uvivu hata kukuelewesha.
Nitapoteza muda.
Haya mambo ni magumu kwako MATAGA
 
Kwani kasema kafa?

Kasema anaumwa na ameanza kutibiwa Nairobi - Kenya na sasa yuko India..

Akipona na kurudi, haitafuta ukweli kuwa aliugua; akapelekwa Kenya na kisha India...

Kama siyo, kanusheni. Kimya maana yake manakubaliana na ukweli huu...!!

Hatuna sababu ya kukanusha chochote maana hamjathibitisha kitu hapo; mmezusha tuu kama kawaida ya mizuka yenu ya njaa --- weka muziki, acha maneno, sawa!???
 
Hii ndio maana halisi ya One Man Show. Maana yake taasisi hazifanyi kazi wote wanasubiri maelekezo ya mtu mmoja.

Hata kwenye hili ni hivyo hivyo,hawana cha kufanya mpaka wapate go ahead. Kwenye hili wamepigwa ganzi, kutetea wanashindwa kusema ukweli wanashindwa. Wakitetea wanahisi kuna matukio yatawaumbua

Hii ndiyo tunataka sasa; hatutaki nchi kila mtu anajiropokea tuuu. Who are you!???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom