Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Kwa hali ya umbea ilivyo sasa, hali ya ubashiri, na pengine hata uzushi, wanaomtaka Rais Magufuli ajitokeze au sijui aonyeshwe [as if yeye ni li sanamu au mdoli]hata akijitokeza au kuonyeshwa, watu hao sitoshangaa endapo watahamisha magoli...
A Real Talk in Town....!!!!

Solution ya ku-fix hii speculation ambayo wewe unaita stupidity ni kwa Serikali.

kujitokeza na kuuleza umma wa Watz wapi alipo Rais.....!!!

Upuuzi wa matamko ya..." oh Rais ni mzima wa afya anaendelea kuchapa kazi ndo juhudi za kujaribu kutaka ku-fix stupidly of the system....!!!
 
Nadhani idara ya mawasiliano ikulu ina wajibu wa kutoa taarifa iliyo sahihi au kukanusha panapotokea uvumi wa namna yoyote ile unaogusa taasisi ya Urais, kumbua Afya ya rais,and his whereabout ni jambo la kitaifa na waliomweka kwenye hiyo mamlaka wanahaki ya kujua kiongozi mkuu wa nchi yupo wapi, kumbuka wakati Mzee mkapa anaumwa taarifa zilitolewa, JK vilevile, na hata wanapofanya ziara pia taarifa hutolewa...
Who are you!? Si mlisemaga rais wenu ni Mr Mzungu, mmemkana tena jamani!?
 
Nadhani idara ya mawasiliano ikulu ina wajibu wa kutoa taarifa iliyo sahihi au kukanusha panapotokea uvumi wa namna yoyote ile unaogusa taasisi ya Urais, kumbua Afya ya rais,and his whereabout ni jambo la kitaifa na waliomweka kwenye hiyo mamlaka wanahaki ya kujua kiongozi mkuu wa nchi yupo wapi, kumbuka wakati Mzee mkapa anaumwa taarifa zilitolewa, JK vilevile, na hata wanapofanya ziara pia taarifa hutolewa...
On the one hand, naiona hoja yako. On the other, hii si mara ya kwanza watu kudai Magu ni mgonjwa taabani mpaka kakimbizwa nje ya nchi.

Unakumbuka ule uvumi/ uzushi wa Mwakahesya juzi kuwa kakimbizwa Ujerumani? Watu waliweka hadi picha za chumba alicholazwa!!

Kumbe ulikuwa ni uzushi tu.

Hiyo kurugenzi ya mawasiliano iwe inajibu mambo kama hayo?

I’m conflicted...
 
Rais wetu Magufuli amejipambanua kuwa anaipenda sana nchi yake na watu wake. Hata kusema hakuna lockdown Tanzania ni muendelezo wa moyo na nia yake safi kwa taifa na watanzania, kwenye hilo hana maslahi binafsi zaidi ya kuyaangalia maisha ya wananchi na uchumi wao kama utawaambia wasitoke nje kwa mwaka mzima sasa tangu corona iwe janga la dunia.

Mimi binafsi sioni ajabu, ubaya wa dhambi kama Rais pia kama binadamu ataugua corona kama walivyougua hata marais wengine wa nchi kubwa kama Marekani na Uingereza.

Watanzania wanamfahamu vema Rais wao anapenda kuzungumza mwenyewe na wananchi wake popote alipo nchini. Anapenda kuonekana hadharani akitatua kero za wananchi na kukagua utendaji wa serikali yake kutima ahadi za chama kwa wananchi.

Kinachowaogopesha wanananchi ni kuona hawamuoni wala kumsikia kiaongozi wao, pia kuona watu wakimsemea Rais kwamba yupo, ana afya nzuri, anachapa kazi, nk. Hiyo sio desturi ya Rais wao, labda kama ndio ameianza hivi karibuni.

Watupe taarifa juu ya kiongozi wetu ili tufurahi nae au tuhuzunike nae na ikiwezekana tuombe pamoja kama ana shida inayomkabili, maana yeye ni mtu anaeyaamini maombi badala ya kila mtu kuhisi kivyake.

Kwa Mwenyezi Mungu hakuna dogo wala kubwa wala jipya lizilowezekana.
 
Raisi wangu mpendwa Magufuli ako na nia ya dhati. Toka moyoni. Msimamo wake na imani yake ndio imekuwa chanzo cha visa.

Ila ukichunguza kwa makini yuko sahihi. Wengine wanatafuta kukubalika waonekana kama wanawaonea huruma wananchi. Kumbe no. (OPPOSITION)
 
Wahusika hawataki muwaulize kuhusu alipo Rais wao, wakiamini kuwa tunamchuria.

Tukiulizia ama kutaka taarifa za uwepo na hali ya nchi kuhusu UVIKO tunapewa takwimu za malaria, pumu, magonjwaya moyo nk, ni kama vile kuugua UVIKO ni uhalifu.
 
Kiukweli hapa Ni kumuona tu popote ALIPO ILI kulimaliza hili. Ni haki yetu Kimsingi. Sasa tunafanya siasa ndefu!
 
Raisi wangu mpendwa Magufuli ako na nia ya dhati. Toka moyoni. Msimamo wake na imani yake ndio imekuwa chanzo cha visa.

Ila ukichunguza kwa makini yuko sahihi. Wengine wanatafuta kukubalika waonekana kama wanawaonea huruma wananchi. Kumbe no. (OPPOSITION)
Una akili kisoda.
 
Kiukweli hapa Ni kumuona tu popote ALIPO ILI kulimaliza hili. Ni haki yetu Kimsingi. Sasa tunafanya siasa ndefu!
Kwani chaajabu ni nini kwenye hili. Tunakuwa kama watu tusiokiwa na matumaini. Rais wetu ni mcha mungu na anafahamu kuwa hata yeye ni binadamu sawa na wengine, ndiyo maana haachi kumtanguliza Mungu kwenye kila jambo. Kwanini watu wanakuwa na hofu nae?
 
Inavyoonekana, kati ya watu walioshadadia sana kupotea huku kwa Magufuli kwa sasa, wakiwemo Tundu Lissu, yule Chahali, na Kigogo, hawana taarifa za uhakika juu ya whereabouts za bwana mkubwa pamoja na hali yake ya kiafya.

Ndo maana unaona walianza na Nairobi, wakaenda na India, wakabadili gia angani na kuelekea Jerumani kabla ya kurudi Mzena. Kesho sijui wataenda wapi. St. Thomas hospital, labda.

Mimi binafsi sijui chochote kuhusu alipo na yu hali gani.

Popote alipo, naombea awe ni buheri wa afya tele.

Kitu ambacho nimekiona kwa wengi waliotoa maoni yao, wengi hao wanaamini kilichomsibu bwana mkubwa ni corona na si kitu au jambo jingine.

Wengi hao wanaosadiki na kubashiri kuwa ni corona, madai yao ni kwamba ama imemuua au imempelekesha sana hadi kumfanya alichungulie kaburi.

Kwa vile mimi sijui kinachomsibu, nimeziweka huru fikra zangu na nimeepuka kuhitimisha. Siwezi kuhitimisha kitu au jambo ambalo sina hakika nalo.

Yawezekana bwana mkubwa kweli alipatikana na corona. Yawezekana labda kagundulika ana saratani. Yawezekana ana matatizo mengine tu ya kiafya yasiyohusiana na corona.

Licha ya hivyo, naelewa kwa nini watu wanasadiki wanavyosadiki.

Ni kwa sababu kuna ombwe la taarifa. Ombwe hilo limetengenezwa na serikali. Hapo hakuna ubishi. Na palipo na ombwe la taarifa, watu watalijazia na walichonacho kichwani na moyoni mwao.

Hivyo basi, leo nimefikiria kitu, tuseme ubashiri wa kwamba ana corona ni wa kweli.

Vipi kama alishauriwa na madaktari aji quarantine kwa siku 14 au na zaidi kidogo?

Kwa vile yeye ni Rais, vipi kama waliona ni vyema kwa yeye kujitenga kuliko kukata mbuga na kuendelea na ratiba zake kama iliyo kawaida lakini si kwamba alikuwa mahututi kawekewa mashine ya kupumulia?

Manake si kwamba kila apatikanaye na corona anakuwa ni mgonjwa wa kulazwa kitandani.

Vipi kama hivyo ndivyo ilivyokuwa.
 
Chahali anadanganya watu aliwahi kuwa mwajiriwa TISS. Hili jambo limeondoa sifa kidogo iliyobaki ya Tundu Lissu....Kigogo hii ni mara ya pili, amepoteza credibility
Inavyoonekana, kati ya watu walioshadadia sana kupotea huku kwa Magufuli kwa sasa, wakiwemo Tundu Lissu, yule Chahali, na Kigogo, hawana taarifa za uhakika juu ya whereabouts za bwana mkubwa pamoja na hali yake ya kiafya....
 
Mimi naamini hata wangetoa taarifa mapema kabisa kwamba anaumwa bado hao wahuni wangesema kafa!

Imagine watu wanasema yuko Nairobi, India, China Mzena hospital na Ujeruman na watu wanaamini!

Yani ni umsukule wa aina gani huu!?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom