Inavyoonekana, kati ya watu walioshadadia sana kupotea huku kwa Magufuli kwa sasa, wakiwemo Tundu Lissu, yule Chahali, na Kigogo, hawana taarifa za uhakika juu ya whereabouts za bwana mkubwa pamoja na hali yake ya kiafya.
Ndo maana unaona walianza na Nairobi, wakaenda na India, wakabadili gia angani na kuelekea Jerumani kabla ya kurudi Mzena. Kesho sijui wataenda wapi. St. Thomas hospital, labda.
Mimi binafsi sijui chochote kuhusu alipo na yu hali gani.
Popote alipo, naombea awe ni buheri wa afya tele.
Kitu ambacho nimekiona kwa wengi waliotoa maoni yao, wengi hao wanaamini kilichomsibu bwana mkubwa ni corona na si kitu au jambo jingine.
Wengi hao wanaosadiki na kubashiri kuwa ni corona, madai yao ni kwamba ama imemuua au imempelekesha sana hadi kumfanya alichungulie kaburi.
Kwa vile mimi sijui kinachomsibu, nimeziweka huru fikra zangu na nimeepuka kuhitimisha. Siwezi kuhitimisha kitu au jambo ambalo sina hakika nalo.
Yawezekana bwana mkubwa kweli alipatikana na corona. Yawezekana labda kagundulika ana saratani. Yawezekana ana matatizo mengine tu ya kiafya yasiyohusiana na corona.
Licha ya hivyo, naelewa kwa nini watu wanasadiki wanavyosadiki.
Ni kwa sababu kuna ombwe la taarifa. Ombwe hilo limetengenezwa na serikali. Hapo hakuna ubishi. Na palipo na ombwe la taarifa, watu watalijazia na walichonacho kichwani na moyoni mwao.
Hivyo basi, leo nimefikiria kitu, tuseme ubashiri wa kwamba ana corona ni wa kweli.
Vipi kama alishauriwa na madaktari aji quarantine kwa siku 14 au na zaidi kidogo?
Kwa vile yeye ni Rais, vipi kama waliona ni vyema kwa yeye kujitenga kuliko kukata mbuga na kuendelea na ratiba zake kama iliyo kawaida lakini si kwamba alikuwa mahututi kawekewa mashine ya kupumulia?
Manake si kwamba kila apatikanaye na corona anakuwa ni mgonjwa wa kulazwa kitandani.
Vipi kama hivyo ndivyo ilivyokuwa.