Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22


Polimilai hazisaidii
Wazee wa ukwaju
 
Sasa kmkm na malindi ni bingwa wa bara tangu lini ndio muandishi huyo nae anajiita?
 
Pana vijana hawajui kama palikuwa na ligi ya muungano na bingwa aliliwakilisha Taifa mashindano ya kimataifa. Bahati mbaya hawajisumbui kutafuta wakiamini kila kitu kipo 'google'.
 
Mkuu, wanahesabu na ngao ya jamii.
 
Cha kuongezea, CAF wanavyosema hayo mashindano mawili yaliunganishwa, huyo mwenzetu anaangalia tu jambo moja la uwakilishi lakini anasahau pia resources ambazo zilikuwa zinatumika kwenye CAF Cup zikiwemo zawadi ambazo nazo zililetwa katika shindano jipya. Kuna mambo mengi hayazingatii.
 
Ikumbukwe kwamba kombe la klabu bingwa Afrika ilianzishwa mwaka 1965 na kombe la kwanza likitolewa na aliyekuwa rais wa kwanza wa Ghana marehemu Kwame Nkurumah na makao makuu ya Caf wakati huo yakiwa Accre, Ghana.
 
Mbona MNAUMIA SANA????maumivu makali ni sehemu ya KUJIFUNZA...SIWALAUMU
 


KWAKO MCHAMBUZI MKUBWA MWAISABULA - 1

Nianze kwa kutoa heshima kubwa kwako, @mwaisabula_mzazi mchambuzi mkubwa.

Wewe ni mtu muhimu sana kwa soka la Tanzania. Umelicheza, umelifundisha na sasa unaendeleza vijana pale Majimatitu kwa Martin Lumbanga...unastahili maua mengi sana.

Kupata nafasi ya kiufundisha klabu kubwa kama Yanga kunaonesha ni kiasi gani wewe ni mbobevu...saluti kwako mzazi!

Wewe unajua mengi sana, lakini hakuna binadamu anayejua yote. Kwenye hili suala la Ligi yetu, Mzazi nikuhakikishie, nalijua sana zaidi yako...tena mbali mno!

Nimelifanyia utafiti wa kina na wa muda mrefu...sijakurupuka!

Ungekuwa umefuatilia vizuri mfululizo wa makala zangu za awali kuhusu hili jambo, ungejua ni kiasi gani naijua hii ligi ya Tanzania.

Muda bado unao, unaweza kuzipitia, lakini anza na hizi za sasa ambazo sijui zitakuwa ngapi.

Ligi yetu ilianza mwaka 1965 na katika msimu wa kwanza vilitumika viwanja viwili; Ilala Stadium ambao sasa ni Karume, na Tanga Municipal Stadium ambao sasa ni Mkwakwani.

Mechi ya kwanza kabisa ilifanyika uwanja wa Ilala, kati ya Sigara (Tobacco) ya Dar Es Salaam dhidi ya TPC (Tanganyika Plantation Company) ya Moshi.

Ilikuwa Jumamosi ya Mei 29, na TPC ilishinda 2-1.

Kule Tanga, mechi ya kwanza ilifanyika Jumapili ya Mei 30, kati ya Coastal Union na Manchester United, zote za Tanga. Mechi hii iliisha kwa sare ya 2-2.

Ligi hii haikuwa ya Bara, bali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na iliitwa Mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Taifa.

Zilitakiwa zishiriki timu kutoka Bara na Visiwani, lakini kwa bahati mbaya timu za Visiwani, yaani Zanzibar, zilishindwa kuja.

Timu zilizoshiriki zikawa SITA tu.

TPC - Moshi
Sigara - Pwani
Yanga - Pwani
Sunderland - Pwani
Coastal Union - Tanga
Manchester United - Tanga.

NB
Wakati huo Dar Es Salaam bado haijawa mkoa. Mkoa ulikiwa Pwani na Dar Es Salaam ilikuwa makao makuu ya mkoa.

Nasisitiza. Ligi iliyoanza 1965 ilikuwa ya Muungano, siyo ya Bara.

Itaendelea
 


KWAKO MCHAMBUZI MKUBWA MWAISABULA - 2

Mzazi @mwaisabula_mzazi, tofauti kati ya Ligi ya Bara na Ligi ya Muungano naijua vizuri sana.

Nadhani wasiojia ndiyo wanaohesabu mataji waliyonayo sasa.

Narudia, Ligi iliyoanza 1965 ilikuwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, japo miaka ya mwanzoni timu za Zanzibar zilishindwa kushiriki.

Kutoshiriki kwao hakukuondoa uhalali wa ligi kuwa ya kitaifa kwa sababu milango ilikuwa wazi na hawakuja kutokana na sababu zao, kubwa zikiwa ni za kiuchumi.

Mwaka 1972 timu za Zanzibar ndiyo zikaaza kushiriki.

Hicho kipicha ni cha andiko la mwaka 1973 likizungumzia ligi ya mwaka huo.

Unaiona hapo Ujamaa ya Zanzibar, hii ina maana kwamba ile ligi haikuwa ya Bara pekee.

Na nikuongezee kitu. Nadhani unaikumbuka Nyamagana Thriller, ile mechi ya Yanga na Simba iliyofanyika Agosti 10, 1974 kwenye uwanja wa Nyamagana Mwanza.

Mechi ile ilikuwa fainali ya Klabu Bingwa ya Taifa, na ndiyo mechi ya kwanza rasmi kuzikutanisha Yanga na Simba nje ya Dar Es Salaam.

Sasa mwaka ule, mechi ya ufunguzi iliyofanyika Julai 18, ilizikutanisha timu za Magunia kutoka Moshi dhidi ya Jeshi Zanzibar.

Mechi hii iliyoisha kwa ushindi wa 5-4 kwa Magunia, ilikuwa na msisimko mkubwa kutokana na funga nifukufunge yake.

Yanga walitinga fainali baada ya kuitoa Miembeni ya Zanzibar kwa ushindi wa 2-1.

Ligi hii iliyoitwa mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Taifa, ilianza 1965 hadi 1981.

Mabingwa

Yanga (7 - 1)
Simba - (8)
Cosmopolitan (1)
Mseto (1)

Hawa ndiyo mabingwa wa Klabu Bingwa ya Taifa, mashindano yaliyokuwa na sura ya Muungano.

Sasa baada ya hapa, yaani kuanzia 1982, ndiyo mfumo mpya wa mashindano ukaja.

Huo mfumo mpya ndiyo uliokuia kuleta ligi ya bara, ligi ya Zanzibar na ligi ya Muungano.

Soma sehemu inayofuata...
 
Katika hili Yanga na Simba waliungana kutupiga kamba, TFF waje waweke hesabu sawa
 
Katika hili Yanga na Simba waliungana kutupiga kamba, TFF waje waweke hesabu sawa
Hata kama ni makubaliano ila Yanga walikuwa vinara walijimegea keki kubwa kuliko mwenzake
 
Ok tufanye assumption kuwa mwaka 1965 ligi ilikuwa ya muungano ila timu za Zanzibar zilishindwa kuja.
Swali je baada ya mwaka 1965 ni mwaka upi timu za Zanzibar ziliamua kuja?
Ligi ya muungano halafu timu zishindwe kuja, hapo inaama ligi ya muungano ilikuwa haina umuhimu ni kama bonanza?
 
Soma post 273
 
1972 team za Zenji zilishiriki ligi ya Muungano
 
Chemsha majani mabichi ya mwarobaini halafu uyaache yapoe; baada hapo chuja maji uyanywe. Matatizo yako yote yatakwisha.
 
Chemsha majani mabichi ya mwarobaini halafu uyaache yapoe; baada hapo chuja maji uyanywe. Matatizo yako yote yatakwisha.
Majibu ya maswali yenu mliyokuwa mnaiza karibia yote yamejibiwa.

Mna lipi la kusema kuuonesha Umma kurwa nyie ni mabingwa mara 29?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…