Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
Kwa hiyo wabara nao wana ardhi Zanzibar?
 
Tatizo ni pale Smz wanapotoa kauli kana kwamba hilo eneo ni sehemu ya nchi yao!
Hiyo kauli haijakaa vizuri.

Hata kama kuna ukweli kwa wanayosema, kwa nini wasingewasiliana na serikali ya bara badala ya kutoa onyo kwenye vyombo vya habari?!

Kauli inaonyesha ishara ya "arrogance".
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
Kiufupi, mikataba hiyo hatuwezi kuitamgua sababu imeshakuwa superceded na mikataba mipya na halali ya kimataifa, mfano sheria za kimataifa zinataka endapo nchi zinatengenisha na maji, basi mpaka unapita katikati, labda kama wataka tuamue kwa kuoigana vita, hiyo ni sawa pia, ila sishauri, maana kwenye vita hakuna mshindi. Kuhusu Zanzibar au mtu yeyote kumiliki eneo popote nchi Tanzania hiyo ni kawaida, sioni cha ajabu Zanzibar kumiliki Ardhi Tanzania au popote pale duniani, sasa mtu kama anapesa kwanini asimiliki ardhi? Ila masharti ya hati ya umiliki yanasemaje usipoendeleza kwa muda wa miaka miwili?
 
Wazanzibar wanapaswa kuja Tanganyika Kuwekeza tu na si vinginevyo, kama ilivyo kwa Mtanganyika atakapokuwa Zanzibar ni mwekezaji na si mmiliki. Ikumbukwe ARDHI si suala la muungano.
Kumbuka mzanzibari ni mtanzania lakini sio kila mtanzania ni mzanzibari
 
Leo nimekutana na clip ya Chars Hilary akiongea akitanabaisha kuwa kuna hekta elf 6 wilayani Bagamoyo ni mali ya serikali ya Zanzibar na mtu kutoka bara haruhusiwi kufanya shughuli za aina yoyote ndani ya ardhi hiyo kwani sio mali ya serikali ya Tanzania bara.

Jambo hili limenisikitisha sana and sijajua inakuwaje wazanzibari wawe na ardhi yao Tanganyika wakati mtanganyika ukifika Zanzibar ni sawa umeenda Kenya tu.

======
Msemaji wa Serikali ya Zanzibari, Charles Hillary amesema Shamba la Zaba lililoko Makurunge wilayani Bagamoyo ni mali ya Serikali ya Zanzibar hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote eneo hilo.

Msemaji amesema Zanzibar imemiliki eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 6000 tangu mwaka 1977. Na amesema yoyete atakayeuziwa eneo katika ardhi hiyo hatalipwa fidia.

Una shangaa nini sasa wakati wana miliki kihalali
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni
Yanga na Simba 🙄
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni

inabidi uwatukane waliasisi muungano na uwahoji hasa lengo lao lilikuwa ni nini?pia uwahoji marais walioendelea kuukumbatia huo muungno walikuwa pia na agenda gani kwa tanganyika?
 
Nimeshangazwa mno kusikia kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejimegea kipande kikubwa cha ardhi nchini Tanganyika huku serikali ya Tanganyika imekaa kimya. Haiwezekani uvamizi huu ufanyike mchana kweupe kila mtu akiona. Lazima kuna jambo limejificha nyuma ya hili sakata. Inawezekana serikali ya mapinduzi ama inataka kuipindua Tanganyika au imechoshwa na muungano; sasa wanataka kuleta chokochoko ili muungano ufe wagawane mbao. Kufulilah! Lolote liwalo na liwe....kama mbwai iwe mbwai! Wasitutishe.

MAONI YANGU
Tangu zamani mimi niliwaambia kuwa huu muungano wa mchongo hauna maana yoyote hamkunisikia. Kiko wapi sasa, si mnaona wao wenyewe wameanza uchokozi? Moja ya makosa makubwa aliyofanya Nyerere ni kuinganisha Tanganyika na hawa wala urojo.

Kama Zanzibar wanaona nchi yao ni ndogo sasa wanataka kuja kupora ardhi ya Tanganyika ni bora waseme wamegewe mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kisha tuweke mipaka mipya kila nchi iendelee na mambo yake badala ya huu uhuni wanaofanya kupora ardhi ya Tanganyika kinyemela. Inauma sana.
 
Roho inaniuma ninapokutana na comment kama hizi
Niliwahi kukamatwa na polisi wa zanzibar kwa kuendesha gari bila kibali cha kuendesha gari(leseni ya tanzania bara haitambuliki ukifika kule lazima ukate permit za kuendesha gari ni kama uonavyo hapa bongo wageni wa mataifa mengine walivyo na leseni zao)
Wakati Kenya unaruhusiwa endesha
 
Back
Top Bottom