Ni sawa kama kuna mkataba na mzanzibar anahaki zote kumiliki ardhi Zanzibar,ila kama Mtanganyika nayeye anahaki ya Utanzania kwanini yeye haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar wakati sisi wote status yetu wote ni Watanzania?
 
Tunaweza kunyang'anywa hata bahari yote!
Nimejikuta napatwa na hasira kwa jambo ambalo halinigusi mimi wala maslai yangu
Nchi hii yenye majeshi yote
Nchi hii yenye DEEP STATE
Kuna watu nanajiona wao ndio watanganyika halisi yaani wazalendo kweli kweli
Uswenge kama huu unatendeka wao ni kusifu ma kuabudu chama tawala na sasa wanajitengenezea ukuta imara yaani "untouchable" yaani chochote akifanya kiwe kizuri or kibaya hakuna wa kuuliza kisheria ama kimatendo...[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Ahsante P umetusaidia sana
1. Umekwepa kusema kuwa Ngosha wewe huwezi miliki hata nusu heka pale zanzibar.
2. Ati ilikuwa mali ya sultani wajerumani walitusaidia huyo sayid aliibeba kutoka maskat au?
3. Hongera zako P na Januari najua mpo kujipongeza kwa bajeti ya kishindo. Mitungi 100 mmegawana kimya kimya... nchi hii inawachawi wengi sana Mungu kawaumbua mama salma katopoka
 
Na sisi Bara tuna eneo ekari 500 Chanjamjawiri na 500 nyingine Donge.
Kwa ukubwa wa zanzibar
Hawawezi kubali heka 1000 zote ziwe mali za tanganyika zaidi ni yellow propaganda!
Kwa sheria zao tu mzanzibar ambaye sio mzawa kuna haki ananyimwa(fuatilia hii program za bima ya afya kwa wazanzibar)
Sembuse aridhi!!?
 
Kaka yangu mayala, hivi eneo la JMT ni tanganyika tu ama ni tanganyika na zanzibari. Kama ni hizi nchi zote 2 mbona inapotajwa umiliki wa aridh yaan wazanzibari wanahesabika sawa na watanganyika ila watanganyika kwenda znz ni big ni. Yaan znz ni kama mwanamke na mumewe wote wana mishahara ila mke mshahara wa kwake na mume mshahara wa familia nzima akiwemo na mke wake ndo huu muungano ulivyo
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni
Kwakweli hii kitu inaboa kweli. Yani siku hizi ulipita mitaani watu ni habari za yanga na simba 24/7/365. Hakuna kitu kingine cha maendeleo watu wanachojadili. Huko kwenye magroup ya whatsapp ndio usiseme. Redioni nako, ni habari za mpira tuuuu. Hivi ntakula huo mpira. Inaudhi sana
 
"Mali ya Sultani wa Zanzibar".
Sultan hakuwahi kuikabidhi Zanzibar wala mali zake nyingine kwa wazanzibar.

Zanzibar wenyewe walimkimbiza Sultan wao na kumnyang'anya mali zake. Katika kumnyang'anya huko, haimaanishi kila alichokua nacho Sultan kitakua ni mali ya Zanzibar, la hasha. Sultani alikua na mali nyingine huko kwao Oman, Je hizo mazo Wazanzibar wana haki nazo?

Kwa namna yoyote ile, chochote kile alicho kimiliki Sultan upande wa huku , maadam Zanzibar waliamua kufanya mapinduzi na kumfukuza na kumpokonya, basi cha upande wa huku hakiwahusu, kinabaki kuwa chini ya watu wa huku, wakati Zanzibar wao wakibaki na mapinduzi yao.
 
Ni kwann Tanganyika ilikufa alafu Zanzibar ikabaki kama si muungano wa kiin macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…