Akiongea kwa sauti kali ya kimamlaka, Ndugu Tundu Lissu amewataka Wazanzibar kuuchukulia serious uchaguzi wa mwaka huu na kwamba wasikubali hata kidogo kudhulumiwa ushindi.
Ndugu Lissu amewaasa wazanzibar kuwa, wasiwape nchi watu wanaopandikizwa na Bara (Tanganyika) na kuwatawala bila ridhaa yao.
Lissu amesema, sababu kubwa ambayo huwa inawafanya Wazanzibari waporwe maamuzi yao kwenye sanduku la kura huwa ni kwa sababu upande wa bara huwa ni dhaifu kwa hiyo wazanzibar huletewa majeshi kuwathibiti ndani ya nchi yao, akasema safari hii haitokuwa hivyo kwa sababu hata bara safari hii hawatokubali kuibiwa kura!. Lissu akasema wakijaribu kuchezea maamuzi ya wananchi huku bara Watasongesha watu Barabarani kukataa uporaji huo.
Lissu amewataka Wazanzibar wasikubali kuporwa ushindi na akawashauri kuwa iwapo wataporwa ushindi basi nao Waingie Barabarani kwa makumi elfu
Huku wakimshangilia kwa kutaja jina lake la "Lissu, Lissu, Lissu", Wazanzibar wameipokea hotuba hiyo ya kihistoria ya Lissu kwa hamasa kubwa na kwa ari kubwa kabisa
Pia Lissu amezungumzia kuhusu Masheikh, waislamu waliowekwa ndani na serikali ya Chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila ushahidi wa kosa wala hukumu, amesema kwenye mikutano mingi kuwa Chadema ikiingia madarakani itawawaweka huru masheikh hao.
Pia amezungumzia kuhusu Muungano, Lissu amesema iwapo Chadema itaingia madarakani wao watarudi kwenye katiba ya Warioba
Sehemu ya hotuba hii, hii hapa chini: