Zanzibar 2020 Zanzibar: Mgombea Urais wa Tanzania, Tundu Lissu (CHADEMA), afanya Mkutano Uwanja wa Kibandamaiti

Zanzibar 2020 Zanzibar: Mgombea Urais wa Tanzania, Tundu Lissu (CHADEMA), afanya Mkutano Uwanja wa Kibandamaiti

Act tuliaambiwa bara waungane na Chadema ili wagawane wabunge wakang'ang'ania mgombea wa kuazima toka ccm hao awauziki tangu lowsa alipotutenda,
Kwa bara wangeungana tu, ila kwa Zanzibar sina uhakika kama Chadema wamesimamisha mgombea, maana hata mkutano wa Lissu jana ametambua kuwa hata waliokwenda kwenye mkutano wake ni wafuasi wa Maalim Seif tu.
 
Lisu na kubenea ni marafiki wakubwa Lisu Ndie alimpa ushauri wa kisheria kubenea jinsi ya kumwekea pingamizi mgombea ubunge wa Chadema ubungo Boniphace Jacob
Punguani weee Kubenea alikuwa Jimbo la Kino...mijitu ya Chato bana
 
Akiongea kwa sauti kali ya kimamlaka, Ndugu Tundu Lissu amewataka Wazanzibar kuuchukulia serious uchaguzi wa mwaka huu na kwamba wasikubali hata kidogo kudhulumiwa ushindi.

Ndugu Lissu amewaasa wazanzibar kuwa, wasiwape nchi watu wanaopandikizwa na Bara (Tanganyika) na kuwatawala bila ridhaa yao.

Lissu amesema, sababu kubwa ambayo huwa inawafanya Wazanzibari waporwe maamuzi yao kwenye sanduku la kura huwa ni kwa sababu upande wa bara huwa ni dhaifu kwa hiyo wazanzibar huletewa majeshi kuwathibiti ndani ya nchi yao, akasema safari hii haitokuwa hivyo kwa sababu hata bara safari hii hawatokubali kuibiwa kura!. Lissu akasema wakijaribu kuchezea maamuzi ya wananchi huku bara Watasongesha watu Barabarani kukataa uporaji huo.

Lissu amewataka Wazanzibar wasikubali kuporwa ushindi na akawashauri kuwa iwapo wataporwa ushindi basi nao Waingie Barabarani kwa makumi elfu

Huku wakimshangilia kwa kutaja jina lake la "Lissu, Lissu, Lissu", Wazanzibar wameipokea hotuba hiyo ya kihistoria ya Lissu kwa hamasa kubwa na kwa ari kubwa kabisa

Pia Lissu amezungumzia kuhusu Masheikh, waislamu waliowekwa ndani na serikali ya Chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila ushahidi wa kosa wala hukumu, amesema kwenye mikutano mingi kuwa Chadema ikiingia madarakani itawawaweka huru masheikh hao.

Pia amezungumzia kuhusu Muungano, Lissu amesema iwapo Chadema itaingia madarakani wao watarudi kwenye katiba ya Warioba

Sehemu ya hotuba hii, hii hapa chini:

 
Back
Top Bottom