Moderator umekuwa na tabia ya kufuta baadhi ya threads zinazohitaji majibu. Naomba uwaache wahusika watoe majibu!
Vituko vya Zitto kisiasa
Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni.
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia, alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol. Source: Tanzania Daima