Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Najaribu kutafakari na kuunganisha dots....hivi siku za nyuma ZZK alisafiri nje ya Tz na Rais JK mara ngapi?
 
Ifweero, Ilipaswa kusomeka "Zitto ana akli kuliko viongozi wote wa CCM ukiwemo wewe Ifweero"
 
Najaribu kutafakari na kuunganisha dots....hivi siku za nyuma ZZK alisafiri nje ya Tz na Rais JK mara ngapi?

Muulize mama salma, acha umbea mtoto wa kiume fanya kazi si kubwabwaja kama vilissu
 
mwisho wa Zitto ni mbaya sana, mpaka sasa kashapoteza sifa yakiongozi, anatukana mamba wakati hata kando ya mto ajavuka!
 
Mimi Ninachojua Ni Kwamba ZZK Alikuwa Na Majukumu Mengi Sana Ya Kitaifa. Sasa Ccm Wakawa Wanampa Kazi Na Kumbana Sana Ili Asishiriki Katika Oparation Za Chama. Kwa Kuwa Ni Mtaifa Zitto Hakuwa Na Jinsi, Aliweka Uchama Kando Na Kulitumikia Taifa. Lakini Kumbe CCM Walifanya Hivi Ili Kumpunguzia Ushiriki Wake Katika Shughuli Za Chama. Mfano Wakati Kamati Kuu Ilipo Keti Zito Alitumwa Sudani, Lakini Alirudi Na Kuhudhuria Usiku Huo Huo. CCM Inawatu Wanao Fikiria Saaana. Kumkeep Bussy Zito Walitaka Wamchonganishe Na Chadema, Na Leo Hii Wamefanikiwa Chadema Hamuoni! Kwa Sasa Matarajio Ya Kushinda Uchaguzi Mkuu Hayapo Kwa Jambo Dogo Kama Hili! Tunarudishana Nyuma Kwa Kushindwa Kufikiri! Ona Wakaandaa Na Waraka, Hapo Ndo Wakawamaliza Kabisa Na Kukiri Kuwa Zitto Ni Msaliti, Mkimtoa Zitto Direction Ya Upinzani Itageuka 2015, Na Sijui Nilini Nchi Hii Itatulia Na Kuwa Na Upinzani Imara! Labda Ni Hadi Ccm Igawanyike Kama Alivyo Sema Nyerere

Hivi unadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho. ZKK ni msaliti nani atamwamini tena? Kama angekuw kiongozi mwadilifu asingesahau majukumu yake katika chama na kujikuta anakimbiza na kutekeleza sera za CCM kila anapotumwa.
 
Hatuna mwanachama anayeitwa Zitto mpaka sasa, yeye mwenyewe anafahamu alichofanya na anafahamu adhabu yake ni nini, that is over about Zitto, akafanye kazi na mahakama, hatuwezi ishi na mdudu, kawawadhalilisha sana watu wa Kigoma.
 
na huu utafutwa fasta..
leo Zitto ndiyo moderator wa Zamu..

CC: Mungi

Nadhani haya maneno yana ukweli kuwa kuna wakati zito ni moderator kwenye siasa. ni zito huyuhuyu aliongoza msafara kwenda kuzindua kampeni ya kafulila.
cc: MANI
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni kweli alienda siku ya mwisho kufunga kampeni, tena baada ya kulazimishwa kwenda, alikuwa haendi kabisa.....

Salama ya CHADEMA ni kumfukuza Zitto Kabwe

Wana JF,
Kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga Zitto hakukanyaga...Dr. Slaa kwa kumlinda akasoma ujumbe ambao Zitto alipost facebook kuomba wanaigunga wamchague Kashindye!
Which is which?
Vitu kama hivi ndivyo vinavyoishushia hadhi chadema.
 
Moderator umekuwa na tabia ya kufuta baadhi ya threads zinazohitaji majibu. Naomba uwaache wahusika watoe majibu!

Vituko vya Zitto kisiasa

Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; “Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni.”
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
“Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol. Source: Tanzania Daima
 
1: Kuhusu mke wa Emmanuel Muhimbo(Josephine musumbushi ambaye leo unaishi naye kama Mchumba wako)

2: Kuhusu kupanga nyumba ya Abla apertment pale kijito nyama huku ukilipa shilingi laki 2.5

3: Kuhusu kulazimisha chama chako kikulipe stahiki zote za mbunge kwa kujitoa kwako kugombea Ubunge na kupeperusha bendera ya urais

4. Elimu yako iliyojaa utata kutoka cheti hadi shahada ya uzamivu

5: Safari yako ya Nchi za Ulaya na mahusiano ya misaada uliyopata kuelekea uchaguzi mkuu

6: Kuhusu kadi ya CCM unayoimiliki na kuilipia mpaka sasa ilihali za wale wanaojiunga na chadema unazichoma moto. Kuna mantiki gani hapa?
 
Huyu ni SALITI maarufu sana. Alisaliti upadre, akasaliti CCM. Ni rahc kuwasaliti watanzania kama aliisaliti kazi ya Mungu.
 
kwanini mwapenda kutufuatilia sanaa....mna wagombea 40 wafuatilieni hao...tuacheni...alaah
 
1: Kuhusu mke wa Emmanuel Muhimbo(Josephine musumbushi ambaye leo unaishi naye kama Mchumba wako)

2: Kuhusu kupanga nyumba ya Abla apertment pale kijito nyama huku ukilipa shilingi laki 2.5

3: Kuhusu kulazimisha chama chako kikulipe stahiki zote za mbunge kwa kujitoa kwako kugombea Ubunge na kupeperusha bendera ya urais

4. Elimu yako iliyojaa utata kutoka cheti hadi shahada ya uzamivu

5: Safari yako ya Nchi za Ulaya na mahusiano ya misaada uliyopata kuelekea uchaguzi mkuu

6: Kuhusu kadi ya CCM unayoimiliki na kuilipia mpaka sasa ilihali za wale wanaojiunga na chadema unazichoma moto. Kuna mantiki gani hapa?

Hivi hapo ulipo mawingu yametanda nini? Inaonyesha wewe ni wale mawingu yakitanda yanawaathiri. Nauliza tu samahan kwa hlo.
 
Back
Top Bottom