Zitto ni mwanasiasa na ni public figure, kila alipo , anachofanya na kusema kinaangaliwa kwa mtazamo mpana na wa kina zaidi, ndivyo ilivyo! kwa maneno mengine 'Fame' inakuja na responsibilities na moja ya hilo ni kauli
Zitto alipaswa kujiridhisha neno analotumia, kwanza, anajua maana yake! na pili , anajua wapi pa kulitumia na kwa wakati gani. Amefeli katika hili.
Jiulize kama Chiba 'lingekuwa neno la mama'' hivi leo dunia ingemuelewaje.
Ni kwa bahati tu Chiba pengine halijulikani sana lakini uzito wake kwa kuangalia maumbile ya mwanadamu na mateso aliyopitia TL, ni tusi kubwa sana
Kumuona TL anatembea ni zawadi kubwa sana kwa mola! huyu mtu amepitia mazito yaisyosemekana.
Zitto where's your moral compass bro.
Ameomba msamaha, mjadala uishie hapa! kadri unavyozidi unaumiza watu wengi sana kuliko tusi lenyewe. Tufunge mjadala !