mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Mkuu Salary Slip, wewe ndiye uliyeongoza kwa bandiko za matukio na kuwasema watu (characteristics of small minds) na hukutaka na ulipuuza ushauri wangu kuhusu kutetea Sera zenu za "Uhuru, Haki, Maendeleo ya Watu - CHADEMA na Kazi na Bata - ACT-Wazalendo.Kutokana na laana na manung'uniko ya watu, hili Bunge litakumbwa na mikosi mpaka watajuta.
Hamkujali kauli za chuki, uchochezi na dharau za wagombea wenu dhidi ya Utawala.
Mliamini habari za mitandaoni na kuweka " video" na picha zilizochachuliwa ili kuonesha wagombea wenu walipendwa.
Hamkujua kuwa vijana waliowashabikia wagombea wenu walikuwa si wapiga kura na wengine walifanya hivyo kwa ushabiki wakitegemea kupata chochote ama kupewa na wagombea au kuwapora waliohudhuria kampeni.
Mlijua kuwa mnalishana matango pori humu JF lakini mlifunga milango yenu ya ufahamu na utambuzi.
KWA HERI UPINZANI na ASANTE KUSHIRIKI, tuonane 2025