Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe avamiwa kwenye Uchaguzi mdogo Muhambwe

Sasa ndio naiamini ile kauli aliyosema Mama Samia kwamba "Mimi na hayati Magufuli ni kitu kimoja"
 
Mmh! Kama ni hizi Nissan Patrol zenye "model" ya zamani, nyingi zikiwa na rangi nyeupe basi utambue ya kwamba watu kutoka katika kitengo kile nyeti wameshirikishwa pia katika ufedhuli huo.

 
Huyu ni snitch tu Sasa unataka watz tukusaidie kwa lipi wakati wewe mwenyew ni msanii tu, wenzio wamegoma kushirik ww ukaamua kusalit wenzio, ifike mahal bora CCM waendelee tu kutawala maana mna tamaa sana, badala ya kulilia katiba yenye kubalance mambo nyie bado mmeziba masikio pamba mkihofia matumbo yenu.
 
Tatizo la zitto ni Kama kirusi hivi, Yan haelewekieleweki hivi, anajua sababu za wenzie kutoshiriki chaguzi hzo, anajua vzr suala la tume kuwa haiko huru, vilevile anajua kuwa katiba Bado inafavour upande mmoja Lakini Hana msimamo wa kutetea haki ya chama chake na Vyama vingine vya upinzani!

Kama ni kweli. Basi ndugu Zitto ujifunze kutokana na makosa, ila kwa Sasa pambana na hali yako!
 
Poleni sana ACT Wazalendo lakini mnastahili kuvamiwa, CHADEMA walisema haya mambo hayajaisha nyie mkapeleka mgombea haya sasa ndio mavuno.

Muwe mnasikiliza Wenzenu, CCM ni genge kubwa likiongozwa na state apparatus. Eti kaenda kuripoti Polis

 
Shetani hana rafiki , huyu tulishamuonya mapema sana lakini akapuuza , atavuna alichopanda
 
CCM hawaamini ushindi wa sanduku la kura Tena [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Uroda walioupata kipindi Cha mwendazake hawataki uishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…