Zitto Kabwe: Hayati Magufuli alikuwa ananichukia

Zitto Kabwe: Hayati Magufuli alikuwa ananichukia

Wanafiki Kama Zitto Mwendazake alikuwa hawapendi.
Zitto ni mtu wa kufika Bei,ulikula vya Kikwete,kwa Jiwe ukaula wa chuya.
Nakumbuka JK wakati anamaliza alimkabidhi kwa Magu ili aendelee kula.

Kumbe falsafa za Magu hazikuwa za kuneemesha mtu mmoja mmoja.
images%20(5).jpg
 
Hiyo SGR na SG mpaka anaondoka hakuwa amefikia hata robo ya mradi mmoja tena kwa kusuasua. Mfano SGR alisema kipande cha Dar-Moro kitakamilika Nov 2019, lakini mpaka sasa bado. Na dalili ya kukwama ilikuwa dhahiri kutokana na ukosefu wa fedha kutokana na utawala wa mabavu bila mbinu sahihi.
Vipi mega projects kama SGR, JNHPP, HOSPITAL ZAHANATI na VITUO VYA AFYA, madaraja ya kisasa kama kijazi, tanzanite, busisi, wami, kule uhasibu.?
 
Hiyo SGR na SG mpaka anaondoka hakuwa amefikia hata robo ya mradi mmoja tena kwa kusuasua. Mfano SGR alisema kipande cha Dar-Moro kitakamilika Nov 2019, lakini mpaka sasa bado. Na dalili ya kukwama ilikuwa dhahiri kutokana na ukosefu wa fedha kutokana na utawala wa mabavu bila mbinu sahihi.
Hatukuona mradi wowote uliosimama from day one. Hayo unasema wewe. Kuchelewa kukamilika ni kawaida. Kibaya mradi kusimama kama ilivyosimama terminal 3 enzi za jk, Magu akaja kuifufua na kuimaliza. Ama ilivyosimama hospital ya rufaa Mara toka enzi za Nyerere Magu akaja kuifufua na kuimaliza kabisa.
 
Akina Makonda, Sabaya na kundi lake la watu wasiojulikana nao hawakuwa wafaidika binafsi?
Kama walifaidika basi walijifaidisha wenyewe. Ila sio kwa kuletewa mezani kama JK alivyotaka Magu amletee zitto mezani.
 
Wanafiki Kama Zitto Mwendazake alikuwa hawapendi.
Zitto ni mtu wa kufika Bei,ulikula vya Kikwete,kwa Jiwe ukaula wa chuya.
Je ambao hawakuwa wanafiki kama kina Lissu Mwendazake aliwapenda?

Pamoja na michezo ya kisiasa anayotumua Zitto kuendelea kuiishi siasa, bado alichosema ni kweli!

Mwendazake hakupenda kukisolewa, kushaurika, ama kutoa uwanja sawa wa wanasiasa kufanya siasa kwa usawa pasi kujali ni chama tawala au vingine. Alijiweka zaidi kama Mwenyekuti wa Chama na si Rais wa nchi kimatendo!

Tuache watu waseme wanayoyajua juu ya mwendazake maana wakati wa utawala wake HAKUTAKA KABISA watu waseme juu yake.

Kutesa kwa zamu, Leo ni zamu ya walionyimwa kusema miaka sita iliyopita sasa ni wakati wao. WAACHENI WASEME!
 
Hatukuona mradi wowote uliosimama from day one. Hayo unasema wewe. Kuchelewa kukamilika ni kawaida. Kibaya mradi kusimama kama ilivyosimama terminal 3 enzi za jk, Magu akaja kuifufua na kuimaliza. Ama ilivyosimama hospital ya rufaa Mara toka enzi za Nyerere Magu akaja kuifufua na kuimaliza kabisa.

Hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari, ndio maana alifanikiwa kukulisha data za kupika. Anasema alijenga hospitali 67 na vituo ya afya 400+, je uliwahi kuona jedwali ya hivyo vituo, tarehe ya kuanza, thamani yake na vilipo?
 
Mazuri yasemwe ila mabaya Nani atamjibia?
Matendo ya Rais sio siri. Yako katika kumbukumbu za nchi. Lazima yasomwe na kujadiliwa kwa uzuri na ubaya wake. Nyerere hadi leo anakosolewa kwa maamuzi yake ya vijiji vya ujamaa na utaifishaji wa shughuli zote kuu za uchumi. Hayuko kujibu wala majibu yake hayahitajiki.

Kama uongo ukisemwa, taasisi husika ya serikali ipo kuweka sawa ikibidi. Kama ni kutetea wapo wapambe watakotoa hoja za kutetea. In any case, Magufuli mwenyewe hakuwa mtu wa majadiliano. alikuwa akitoa amri na kukemea tu wote wasiomuunga mkono. Asingejibu kuhusu "mabaya" yake.

Tunasoma historia na kujadili matendo ya watu kama akina Christopher Columbus, Alexander the Great, Josef Stalin, Julius Nyerere, n.k. Ingekuwa lazima wawepo kujibu mabaya yao tusingewagusa na legacy zao zisingekuwepo.
 
Hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari, ndio maana alifanikiwa kukulisha data za kupika. Anasema alijenga hospitali 67 na vituo ya afya 400+, je uliwahi kuona jedwali ya hivyo vituo, tarehe ya kuanza, thamani yake na vilipo?
We kweli tindo..kwa hiyo vyombo vya habari kutokuwa huru ndio vinakuonyesha mfugale flyover, tanzanite bridge, daraja la kigongo busisi, mfugale flyover, hispital za rufaa mbeya, mtwara na mara?
 
Kwani JK alikuwa anawalisha mdomoni kwa kijiko hilo genge lake?
walifaidika basi walijifaidisha wenyewe. Ila sio kwa kuletewa mezani kama JK alivyotaka Magu amletee zitto mezani.
 
Back
Top Bottom