Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Baadhi ya watanzania wanakuwa wapole kupitiliza pale Kenya inapokuwa inalaumiwa. Je kuna wanaonufaika na Kenya kibinasfi au kitaasisi? Au ndio ni ule msema wa "Adui wa adui yako ni rafiki yako"
 
Barua gani tena?

Hakuna barua iliyotumwa Tanzania.

Labda useme hiyo ya malori yanayorundikana hapo Namanga, kama ndiyo unayaita barua.

Huu ni uhuni wa kipekee wanaofanya Kenya, na niuchokozi wa maksudi kabisa.
Mkuu heshima kwako,
Katazo hilo la Kenya limetolewa na wizara ya kilimo Kenya, na wameonesha kweli kwamba mahindi yetu yana sumu kuvu, Zitto anazunguka anakiri ni kweli mahindi ya Dodoma na Manyara yana sumu Kuvu, ila anasema diplomasia itumike..
Naamini Tanzania tuna wizara ya kilimo iliyojaa tafiti za kutosha kuhusu mahindi yetu mara mia ya wakenya, kwanini wao wasijibu kuliko kuacha upotoshaji ukiendelea, tena na wakenya..

Wakenya hawajaanza kula mahindi ya Tanzania leo wala jana.. ni tangu kitambo kirefu sana.. swali tujiulize kwanini sasa, na tutumie wataalam kuliko watu wa maneno matupu
 
Nakubali ukweli ni kwamba hii ni dili ya watu ndani ya Kenya. Yaani wanamahindi kibao kwenye magodauni tena ya Tanzania waliyo nunua huko nyuma halafu wanasubiri bei ipande wauze. Ni rushwa maana shirika la chakula Duniani mpaka sasa lina nunua mahindi ya Tanzania!
 
Kiongozi wa Chama ndugu Zitto ameitaka Serikali kulinda soko hili kwa wivu mkubwa na amekemea tabia ya viongozi wa Serikali kuchukua maamuzi dhidi ya Kenya ambayo madhara yake ndio haya tunayoona sasa. Kenya na Tanzania ni ndugu na wanachama wa EAC hivyo mgogoro wowote utatuliwe kwa kutumia Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC, alisisitiza.
Unalinda "soko mhimu" huku mwenye soko akikutia vidole?

Alichokosa kutaja Zitto ni kwa nini hawaisukumi serikali itafute soko pana, badala ya kutegemea soko hilo hilo la kipuuzi.

Hakupendekeza pia kufanywa juhudi za kusindika haya mahindi ya ziada, kama kutengeneza ethanol, vyakula vya kuku, nguruwe, ng'ombe, samaki, n.k.

Anachojua yeye ni hilo hilo soko muhimu la Kenya; soko lisilo la kutegemewa hata kidogo.
 
Kwani dipromasia ni kuwa unyanyaswe kila mara kisha ujibebeshe kwa udhaifu ndio dipromasia?
Kila upande unatakiwa kutumia hiyo dipromasia,
Kama wakenya ni bingwa wa dipromasia wasingezuia mahindi kihuni bali wangewasiliana na viongozi wenzao wa nchi yatokayo hayo mazao.
Mbona nyie mlikuwa wa kwanza kuchoma vifaranga vya wakenya kwamba wao hawaoni hasara isipokuwa nyie tu?
 
Kuna uwezekano mkubwa sana, kwamba tatizo sio mahindi yana sumu, bali kukawepo sababu ya kutoa hicho kama kisingizio.

Kwani utaratibu unajulikana vizuri katika mambo ya biashara kama hizi ndani ya ushirikiano wetu.

Kama Kenya wamepima wakakuta kuna sumu zaidi ya kiwango kinachokubalika, hatua inayofuata ni kutoa taarifa kwa Tanzania juu ya vipimo hivyo na mzigo hasa unaohusika. Taratibu zinaeleweka vizuri kabisa. Sio kuandika barua na kupiga marufuku hata bila ya kuwapa taarifa wenye mzigo wao.

Kwa hiyo, Kenya kwa sababu zao wenyewe, wameona kutuweka vidole machoni, bila kujali maumivu tutakayoyapata.

Mshirika katika mambo ya biashara anapokufanyizia hivi, huyu si mshirika bali anakuchokoza. Kama huna ubavu wa kujibu mapigo ataendelea kukutia vidole hata sehemu ambazo hukutegemea angefika.

Kenya ni wachokozi. Dawa ya mchokozi ni kumlipa kwa uchokozi wake ili akili umuingie kichwani.

Hiyo diplomasia anayozungumzia Zitto ni baada ya kumpa fundisho mchokozi.
 
Back
Top Bottom