Shehullohi
JF-Expert Member
- Jul 21, 2020
- 3,753
- 3,685
Akili ndg ni ngumu sana kuelewa kilichondelea hapo, Mungu saidia wewe usiwe mmoja wao. Uwe umemuelewa JPM. Ni kuulize wakina Adadi CCM safari hii ni wangapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nitampigia kura yangu Mh. Lissu usiniulize mke wangu atampigia nani maana yeye nae ni mtu mzima atachagua kiongozi anayemtaka kwa sababu sisi hatuko kama makondoo ya CCM ambayo yote yanatumia kichwa cha likondoo limoja kufikia uamuzi wa hili au lile.Yeye kama yeye kadeclear kumpigia Lissu. Anawashaurije wafuasi wake?
Membe atampigia nani? Mbona kuna kigugumizi kwenye hii issue? Chama kimeshindwa kuafikiana!?
Mmemkausha damu mzee wa watu. Inamaana yeye haaminiki?MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.
Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:
1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.
2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.
3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.
Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Natanguliza Shukran kwenu
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
Kwaheri Membe. Sasa nawe jitokeze hadharani kumuunga mkono rasmi Mheshimiwa Tundu Lissu. Hakuna mwingine zaidi ya Lissu 2020 ikulu.MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.
Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:
1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.
2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.
3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.
Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Natanguliza Shukran kwenu
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
Anaandaa Baraza la MawaziriVipi kuhusu mgombea wa chama chako Kachero Mbobezi Bernard Membe?
Mzee mambo ya Act na chadema hayakuhusu. Zungumzia ya Lumumba.Kwani wewe kinachokufanya ukatae kuwa Zitto sio msaliti ni nini? mbona hata huyo Lissu anajua na ndio maana wakamtimua chadema,Lissu mwenyewe alisema kuwa ACT si chama cha upinzani na hikjawahi kuwa chama cha upinzani hata 2015 na aliyekuwa mgombea wao Anna Mghwila walikuwa wanatumika tu serikali kuvuruga upinzani na ndio maana Anna Mghwila akaja kuzawadia cheo.
Sasa sijui wewe unakwama wapi?wewe unachokifanya ni kuunga mkono usaliti kutoka kwa msaliti aliyebobea.
Membe yuko kwenye harakati za chini kwa chini kuthibiti wezi wa TUME.Kwaheri Membe. Sasa nawe jitokeze hadharani kumuunga mkono rasmi Mheshimiwa Tundu Lissu. Hakuna mwingine zaidi ya Lissu 2020 ikulu.
Toka lini mkamwita hivyo?? Mmehamia kwa Zitto baada ya kumshindwa Mbowe.Siyo kwa 'Mnafiki / Ndumilakuwili' huyo 'aliyetukuka' kabisa.
Hehehehee mzee kachanganyikiwa......nileteeni gwajimaaa.....y
wee utakuwa polepole wewe mana ninyi ndo mlimdanganya babu wa watu kuwa chadema kimekufa kwa hiyo hakuna hata haja ya kampeni...leo hii babu kachanganyikiwa hajui aanzie wapi amalizie wap kabakia "nileteen gwa jima🔈🔈🔉🔉🔈🔈
nileteen gwa jimaaaa🔉🔉🔉🔉🔊
nileteen gwa jimaaaaaa🔉🔉🔉🔉🔉🔉🔉🔉🔊🔊📢📢
nileteeni gwa jimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊📢📢📢📢📢📢📢📣📣📣📣📣📢📢🔊🔊📢📣📣📢📢🔊📢📣📣🔊🔊📢📢📢📢📢📢📢📢📢📢📢
🤣🤣🤣🤣🤣
Mmehamia kwa Zitto tena ni i kinawauma?? Kaunga mkono chadema wewe CCM kinakuwashia nini.Unajua Katika Wapinzani Wa Tanzania Kuna haka ka kijana ka Zitto.🤣😂🤣😂 Kama huna Akili au uwe Akili ya kiBAVICHA Huwezi kukuelewa....
Dogo Anajua kabisa Tundu Hawezi Kushinda Ila, ila Tundu anaushawishi kiasi Fulani kwenye Siasa za Kibongo ila Ushawishi usiomshinda Magufuli.
Sasa Dogo keshaona Kabisa CHADEMA inakwenda kufa kifo cha mende na Mwisho wake Ni Baada ya Uchaguzi so what next.....
Wapo watakaoenda CCM ila sio Lissu wapo watakwenda ACT. But kwa ushawishi alionao lisu sio Wa kuhamia chama lazima ashawishiwe kwa nafasi na ahadi nono. So Leo Lissu anamuunga mkono Lissu akijua hatashinda ila Atakuwa Wa msaada kwenye Malengo yake ya KIKIUWA CHADEMA COMPLETELY.... Tukumbuke Kabisa haiwezekani Zitto kuipenda CHADEMA kuliko ACT.... Sasa CHADEMA INAKWENDA KUFA NA HAITAKUWA CHAMA KIKU CHA UPINZANI NI ACT NDIO INAKWENDA KUSHIKA HATAMU .....RUZUKU ....HAYA HUKO NDIO PESA YA UPINZANI INAKWENDA KUWA NONO UNAFIKILI TUNDU LISSU MPENDA HELA ATABAKI CHADEMA INAYOKWENDA KUWA NCCR ILIYOCHANGAMKA🤣😂🤣😜 LISSU ATAHAMA CHADEMA KWENDA KWENYE NEEMA NA HAPA NDIPO UPINZANI WA UKWELI TANZANIA UNAKWENDA ZALIWA, UPINZANI UTAWEZA ITINGISHA CCM.
WAFUASI WA MAALIM SIEF NA WA TUNDU LISSU
NA MIMI NINACHOKIANGALIA NI HIKI CHA 2025 KUWA UCHAGUZI MGUMU KWA CCM SIO HUU WA 2020 MAGU ANASHINDA MAPEEEEEMA ......NA YEYE NDIO AKAEUWA TENA ACT KWA MAMBO ATAYOFANYA IN 2020-2025🤣😂🤣😂🤣 ACT ITAFURUKUTA ILA HAITASHINDA 2025 MAANA HAWATAKUWA NA SERA PINGAMIZI ZA KUIANGUSHA CCM
HAPA NDIO MTAMKUBALI MAKONDA KWAMBA RAIS WA KUINAGUSHA CCM YUPO WAPI
..Msando amechemka.*ANAANDIKA ALBERT MSANDO KUHUSU UNAFIKI NA USALITI WA ZITTO*
Ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto,
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo,
Bangwe, Kigoma Mjini.
Kwanza, nichukue nafasi hii kukupa pole kwa ajali na kumshukuru Mungu kwa kukuponya na ajali hiyo.
Pili, nimeona kwa haraka kabisa nibebe jukumu la kukujibu wewe binafsi kuhusu Tamko lako lenye kichwa cha habari, “Nitampigia Kura Tundu Lissu ili awe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.
Nilitegemea sana kwamba baada ya kufungwa kengele ya unafiki na usaliti na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo miaka yote ile leo ungesimama na kuwaeleza ukweli watanzania badala ya hiki ulichokifanya.
Mimi nilikuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kwamba wewe ni mnafiki na msaliti. Tulisimama wote muda wote ulipopewa jina baya ili ufe kisiasa (“wazungu wanasema “give a dog a bad name and hang it”).
Ila leo umethibitisha yaliyosemwa na hao ulioamua kushikana nao mikono. Hii yote ni kwa sababu tu ya uchu wa madaraka na imani kwamba kuna uwezekano wa kupata nafasi endapo TL atashinda. Umediriki KUTAMKA hadharani UONGO na UPOTOSHAJI ili kukidhi matamanio ya nafsi yako.
Umesaliti na kutupa chini ya basi misimamo yako binafsi na ya wale ambao wameendelea kukuamini hata baada ya sisi wengine kukaa pembeni na kukuacha ili ujenge Chama chako. Najua hawatakwambia ila mioyoni mwao watakuwa wanaumia sana na sasa wameelewa wewe ni mtu wa aina gani. Ila ndio basi tena!
Nikukumbushe mambo mawili tu ambayo umeyasemea UONGO na kujivika joho na UNAFIKI kwenye tamko lako.
1. Umetamka kwamba kutokana na uwepo wa sheria kandamizi ya Vyama vya Siasa, ushirikiano wa kisheria tumeona hauna maana kwetu kama Chama kwani Msajili wa Vyama hawezi kuidhinisha jambo linalokwenda kuiondoa CCM madarakani. Zitto, wewe ni muongo sana. Sana. Kifungu cha 11A cha Sheria ya Vyama vya Siasa inaruhusu USHIRIKIANO wa vyama vya siasa MIEZI MITATU kabla ya uchaguzi. Mikutano Mikuu ya Vyama husika lazima vipitishe maamuzi ya ushirikiano huo (coalition). Nikuulize, mngekaa lini? Miezi mitatu mazungumzo yenu na CHADEMA kuhusu ushirikiano yalikwamishwa na nini? Na nani? PIA Msajili wa Vyama hana mamlaka wala hapaswi KUIDHINISHA AU KURIDHIA ushirikiano wa vyama. Mkishasaini na kukabidhi BASI. Hata hili umeamua kuongopa.
2. Umetamka, “zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu”. Umesahau nani alikuwa kinara wa sisi kufukuzwa CHADEMA kwa aibu? Umesahau? Ni nani alikunyima HAKI ya kusikilizwa? Ni nani alisema Kamati Kuu isikusikilize wewe ni msaliti? Nani alisema hupaswi kuaminiwa kwa chochote? Unaongopa. Unakana hata kile nafsi yako inachokijua na ilichopitia kwa uchungu mkubwa. Umemsahau Tundu Lissu tuliekimbizana nae Mahakamani kusimamia haki zako za kutaka uenyekiti, kusikilizwa na heshima kwa jamii?
Nimalizie kwa kukukumbusha, umeshindwa kutamka nani achaguliwe kwenye Kata na Majimbo. Sio kwa bahati mbaya. Nafsi yako imekusuta. Umesema wapigiwe wagombea wenye ushawishi. Mbona mliweka wagombea ambao hawana ushawishi? Hutaki umma ujue kwamba Chadema walikugomea kukuachia baadhi ya majimbo na kata? Na sababu ni ile ile kwamba hawakuamini? Na sehemu ambazo hamjaweka wagombea ni kutokana na ukosefu wa fedha? Si ukiri tu?
Bernard Membe. Umemuacha kwenye mataa. Huyu wala simuhurumii. Alitaka mwenyewe. Angetumia akili kidogo tu angejua kona ambayo ungemuachia. Tatizo lake (na lako) ni uongo. Alikudanganya ana FEDHA nyingi za uchaguzi kumbe hata hela ya fomu ilikuwa ni mtihani kuitoa. Madeni aliyokuachia yatalipika kwa kudra za Mwenyezi Mungu. ILA hujataka hata kumzungumzia kwenye tamko lako. Wala hatma yake hujagusia. Kichaka kwamba WEWE BINAFSI utampigia kura Tundu Lissu ni cha kitoto sana. Wenye akili wataelewa. Imefika mwisho.
#JPMMitanoTena #CCM
Albert Gasper Msando,
MwanaCCM, Ndugu yako.
16/10/2020.
Yeye kama yeye kadeclear kumpigia Lissu. Anawashaurije wafuasi wake?
Membe atampigia nani? Mbona kuna kigugumizi kwenye hii issue? Chama kimeshindwa kuafikiana!?
Unamjuwa Zitto au unamsikia tu? Kwa taarifa yako tu ata Magufuri agombee ubunge Kigoma mjini hawezi kamwe kumshinda Zitto.Mmechemka vibaya,wewe mwenyewe huna uhakika kama wananchi watakurudisha bungeni safari hii. Msaliti kamuunga mkono kibaraka. Hongereni
Vipi kuhusu mgombea wa chama chako Kachero Mbobezi Bernard Membe?
Weweje, umepona pia? Maana nilikuona sehemu ukichukua dawa kwenye kituo cha wagonjwa wa akili...