Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Sasa kwani ku save unatakiwa u save ngapi?Mzeebaba una save laki na 30 tu kwa mwezi π³π³
Apo umeishatowa na yale makato ya nssf?
750k ni takehome baada ya makato yote.Sasa kwani ku save unatakiwa u save ngapi?
Kasema 750 so assumption yangu ni hela anayochukua kutumia baada ya makato
Mzee baba umetisha.Umeeleweka sanaMshahara ni budget...ukipokea 750k kwa mwezi matumizi yako hayatakiwi yapindukie 15000 kwa siku. Utafanyaje ili ukutoshe? Hakikisha kwanza unaweka shehena ya nafaka ndani, nunua unga kg 10, mchele kg 10 ,ngano kg 10, sukari kg 5, maharage kg 7-10 na mafuta ya kupikia atleast 5litre na gesi inategemea na ujazo ila ule mtungi wa elfu 55-60 unakutosha kumaliza mwezi-miezi miwili.
Mbogamboga jitahidi uwe unapitia sokoni kununua maana kuna unafuu kiasi, ukipata sado zako mbili za viazi, Dagaa kg 2-3, vitunguu kg 2-3, viazi vitamu au ndizi mbichi. Hapa bajeti ya kula mwezi mzima humalizi laki na 20 ikiwa una familia ya mke na watoto 2-3.
Jitahidi kukaa maeneo ambayo ni karibu na kazi! Sio unafanya kazi posta halafu unaishi mpiji magoe ndani ndani huko...nauli tu kwa siku unamaliza zaidi ya 6,000. Ishi sehemu ambayo utatumia gharama ndogo ya sh 500 kwenda na 500 kurudi. Epukana na kupenda sana kutumia bodaboda kwani zinacost. Usiishi maisha ya kujinyima sana kwa wiki jitahidi ule hats nyama mara 2. Epukana na anasa za ulevi wa pombe,kamari na wanawake. Hapo utaona jinsi utakavyosave zaidi ya 300k kila mwezi.
Kama ni bachela jitahidi sana uwe na life skills kama kujua kupika, kuosha vyombo,kufua nguo zako n.k utasave pesa nyingi sana unazoenda kuzipotezea migahawani.
Kama umepanga chumba kimoja basi jitahidi kodi isizidi 50k kama ni vyumba viwili isipindukie 100k kwa mwezi
Duh basi life ni tough sanaSasa kwani ku save unatakiwa u save ngapi?
Kasema 750 so assumption yangu ni hela anayochukua kutumia baada ya makato
Zamani nilipooa nikimfundisha mke wangu jinsi ya kubudget pesa! Huwezi kuamini hii 5000 watu wanayoidharau unaweza ukaipangilia na ikatosha kwa siku nzima. Majirani walikuwa wakija walituona ni matajiri kwa jinsi tulivyokuwa tunakula vizuri kumbe budget kwa siku haizidi hata hiyo 5k.Mzee baba umetisha.Umeeleweka sana
Wewe una save sh ngapi kwa mwezi?Duh basi life ni tough sana
Mimi ni mjasiriamali ivyo kila siku nasave siyo chini ya 40k piga hesabu apoWewe una save sh ngapi kwa mwezi?
Kachape kazi...wengine humu wanakuvunja moyo tu....mi nakumbuka Nimeanza kazi 2009 mshahara 322,000/= , take home 258,000/= .hilo ndio daraja Leo wanaanzia 940,000/=. Kikubwa mipango yako tu. Humu Kila mtu tajiri.Pamoja.
Ngoja nikapige kazi
Vijana sikilizeni and take it from me, unapoanza maisha hata ukiwa na familia ya watoto watatu, elfu tatu inatosha sana kwa siku.Zamani nilipooa nikimfundisha mke wangu jinsi ya kubudget pesa! Huwezi kuamini hii 5000 watu wanayoidharau unaweza ukaipangilia na ikatosha kwa siku nzima. Majirani walikuwa wakija walituona ni matajiri kwa jinsi tulivyokuwa tunakula vizuri kumbe budget kwa siku haizidi hata hiyo 5k.
Kikubwa uombe Mungu usipate mke waruwaru! Omba upate mke msikivu ambaye utamuelekeza jambo atakusikiliza,kukushauri na kukutii! Mtafika mbali sana kwenye maisha sio hawa chupi dera kila siku ana michango ya sherehe,vigoma,mabeseni,birthday n.k atakupasua kichwa na utaona kuwa pesa hazikutoshi.
Kwanza ana nidhamu achaaa...haha kashifa ana nyuzi za ujinga MMU [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]yaani namheshimu yule bro acha kabisaa sijawahi ona Hata kama kashawahi jikweza ktk nyuzi zakeHalafu unakuta hana makeke hawezi kusimanga ambao hawana magari.
Ila ngoja ukutane na hawa wanaomiliki alteza sijui subaru used tena za bongo mamaeeee kipindi cha mvua wanaturushia maji watembea kwa miguu.
Hii imekaa poa Sana.Huo mshahara unaweza kutosha kama unaweza kutenga Bajeti ya matumizi yako kwa kufanya walau hivi;-
Hela ya Kula 10,000@siku 30 =300,000/-
Akiba = 138,000/-
Kodi ya nyumba/mwezi 70,000/-
Nauli 3,000/siku 24 = 72,000/-
Vocha/bundle /mwezi =15,000/-
Bill Umeme/Maji = 25,000/-
Mavazi = 50,000/-
Sadaka siku za Ibada 10,000@ wiki 4=40,000/- (Nimefanya reference ya ibadani kwetu tuna Sadaka zaidi ya 3 kwa siku).
Michango/Harusi/Misiba/Kusaidia Ndugu =20,000/- (Tunaishi kwenye Jamii muhimu ku socialize)
Outing kwaajili ya ku relax na kusocialize na watu na kumwagilia Moyo =20,000/-
NB; Unaweza kufanya maboresho kadri unavyoona inafaa.