Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Haongelei kiuchumi wala miundombinu ya vitu bali haki ya raia kujiamlia mambo yao kama tulivyozoezwa kusema "Kila mtu ana haki ya kwenda atakako kusema atakacho na kukutana na watu mradi havunji sheria". Hizo nchi hazina hilo inabidi kila nyendo za kila raia ziratibiwe kisiri siri.

MAENDELEO YA NCHI SI VITU BALI NI WATU WENYEWE. Fafanua.
1. Nani alikuambia raia wa south Korea hawana Uhuru ?

2. Nani alikuambia raia wa Russia hawana Uhuru ?

3. Nani alikuambia raia wa China hawana Uhuru ?
 
Kuifananisha nchi inayo nuka umasikini[ Tanzania ] na mataifa Kama China, Russia, South Korea unaya vunjia sana heshima hayo mataifa.
South Korea nimeiandika kimakosa. Ni North Korea ...... hizo nchi zimezidi sana katika ukandamizaji wa haki za raia wake ..... same as Tanzania.
 
Wamesema kukashifu siyo kukosoa
Kukosoa si kosa,kosa ni kukashifu.
Vyote ni sawa vinatofautiana kidogo tu.
Ukimkosoa wa chini yako au wa juu yako mwenye hekima unaonekana genius na mwenye busara umetambua makosa yaliyopo, Ila ukimkosoa mpumbavu ata utumie njia ya kistaarabu utaonekana unamkashifu kwa kuanikani ulemavu wake wa kufanya maamuzi (wewe una uwezo mkubwa wa kufikri kumzidi) na hii ndio viongozi wengi wanayo wanajihisi wao Wana akili sana kuwashinda waongozwa
 
1. Nani alikuambia raia wa south Korea hawana Uhuru ?

2. Nani alikuambia raia wa Russia hawana Uhuru ?

3. Nani alikuambia raia wa China hawana Uhuru ?
Wana controlled fredom. Naongelea NK maana nimefanya kazi kule chini ya mwavuli wa kimataifa, tunaambiwa usiongelee siasa, uhuru wa watu bali fanya kazi yako kama ni kuhusu wanawake na watoto basi. Je unapokuta mama amenyang'anywa ardhi yake aliyopewa kulima anapewa mtu mkubwa, huna uwezo wa kumwambi shtaki sababu mahakama ni za wananchi ambazo zipo controlled. Hata china yule dada aliyesema alidhalilishwa na top official wa Tennis aliishia wapi?
 
South Korea nimeiandika kimakosa. Ni North Korea ...... hizo nchi zimezidi sana katika ukandamizaji wa haki za raia wake ..... same as Tanzania.
Huo ukandamizaji wa haki za binadamu kwa mujibu wako [ MTANZANIA ] au kwa mujibu wa raia wa hizo nchi ?
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura😬

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
Hawezi kushinda kwenye tume ya utumishi wa umma kwa kuwa kule wamejaa makada.. Pia kuna kuibeba Serikali..
Labda baada ya kutoka huko aende Mahakamani.....anaweza kushinda huko...
 
Machawa yanatafuta vyeo kwa kufukuza wenzao,kwani yeye ni nani mpaka asikosolewe?
 
Wana controlled fredom. Naongelea NK maana nimefanya kazi kule chini ya mwavuli wa kimataifa, tunaambiwa usiongelee siasa, uhuru wa watu bali fanya kazi yako kama ni kuhusu wanawake na watoto basi. Je unapokuta mama amenyang'anywa ardhi yake aliyopewa kulima anapewa mtu mkubwa, huna uwezo wa kumwambi shtaki sababu mahakama ni za wananchi ambazo zipo controlled. Hata china yule dada aliyesema alidhalilishwa na top official wa Tennis aliishia wapi?
Yule mwanatenesi wa kimataifa wa kichina yupo na alitoka hadharani kupinga hayo mashataka unayoyazungumzia wewe na wale wote wa magharibi waliozungumza hizo habari.
 
Back
Top Bottom