Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Hili ni funzo, nakumbuka kuna mtu aliwahi nichomea nikiwa std 4 kwa ishu ambayo ilikuwa very personal. Siku hio nilipewa adhabu nikawa nimepiga goti nje.Ndo kawaida haswa wale chawa kupenda sifa. Ndo maana izo group za kazini hata kama ya ishu zenu binafsi kama magroup ya vitengo, labda mnacheza vikoba, magroup ya harusi ukijifanya umeshare mambo kama hayo Kuna wambea unachomwa kweupe kwa boss.
Out of the blue kuna classmate alifungua bag yangu kimya kimya kulikuwa kuna daftari moja la rough, nilikuwa mchoraji mahiri sana nikiwa yanki sasa akawa anatafuta daftari nalochoreaga. Ndani kulikuwa na picha za magari na watu, katuni akawa anaangalia ila kuna page moja ilikuwa ina conversation ya ajabu. Hio siku nilihisi ganzi, maana sikuelewa kisa kilianziaje mpaka kesi ikafikia nahitwa kwa head master.
Kuna siku moja home niko na bro yangu mmoja alikuwa ananifundishaga hesabu. Siku sina mood tukaingia kwenye matani tukaanza kujibizana kwa kuandika. Utani utani ukaenda kwenye matusi kibao.Ile kurasa ikawemo kwenye hilo daftari na ndio kitu kiliniletea hio kesi.
Kwa mara ya kwanza naambiwa peleka mzazi shuleni.