Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Ndo kawaida haswa wale chawa kupenda sifa. Ndo maana izo group za kazini hata kama ya ishu zenu binafsi kama magroup ya vitengo, labda mnacheza vikoba, magroup ya harusi ukijifanya umeshare mambo kama hayo Kuna wambea unachomwa kweupe kwa boss.
Hili ni funzo, nakumbuka kuna mtu aliwahi nichomea nikiwa std 4 kwa ishu ambayo ilikuwa very personal. Siku hio nilipewa adhabu nikawa nimepiga goti nje.

Out of the blue kuna classmate alifungua bag yangu kimya kimya kulikuwa kuna daftari moja la rough, nilikuwa mchoraji mahiri sana nikiwa yanki sasa akawa anatafuta daftari nalochoreaga. Ndani kulikuwa na picha za magari na watu, katuni akawa anaangalia ila kuna page moja ilikuwa ina conversation ya ajabu. Hio siku nilihisi ganzi, maana sikuelewa kisa kilianziaje mpaka kesi ikafikia nahitwa kwa head master.

Kuna siku moja home niko na bro yangu mmoja alikuwa ananifundishaga hesabu. Siku sina mood tukaingia kwenye matani tukaanza kujibizana kwa kuandika. Utani utani ukaenda kwenye matusi kibao.Ile kurasa ikawemo kwenye hilo daftari na ndio kitu kiliniletea hio kesi.

Kwa mara ya kwanza naambiwa peleka mzazi shuleni.
 
Hawezi kushinda kwenye tume ya utumishi wa umma kwa kuwa kule wamejaa makada.. Pia kuna kuibeba Serikali..
Labda baada ya kutoka huko aende Mahakamani.....anaweza kushinda huko...
Mahakamani nako labda apate Wakili msomi(Kibatala au arudi Tundu Lissu) lakini kinyume na hapo asijisumbue, atapoteza hata kile kidogo alichokuwa amechuma.
 
Hili ni tatizo la kiutamaduni ni big problem. utamaduni wetu ni wa kijinga katika suala ukosoaji tuko ziro eti mkubwa hakosei na hakosolewi, ni upumbavu tu. Ili nchi isonge mbele watoto wafundishwe kuwa kukosoa wakubwa ni sahihi na wakubwa kuomba msamaha wadogo wanapowakosea ndio modern civilization!

Jamaa kaonewa ana haki ya kukata rufaa maana kuna haki za binadamu "freedom of speech" zifuatwe tumesaini wenyewe UN!
Hii kitu imeanza ngazi ya familia. Ndio maana kuisha itakuwa ngumu. Until kije kizazi kingine
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

View attachment 2331170
View attachment 2331171
View attachment 2331172
Upo serikalini Tena kwenye nafasi ya uteuzi,unapopinga Yale yanayosimamiwa kupitia sera na miongozo ya serikali,huo ni utovu wa nidhamu,kama hukubaliani nao,Kaa kimya,toa maoni jinsi ya kuboresha lakini sio kukosoa kwa kuonyesha jinsi viongozi wako wa juu wanavyokosea,uwezi kumkosoa boss wako harafu akuache tu,hii ni logic simple kabisa.

Viongozi wa kisiasa wanapo amua mwelekeo wa jambo fulani kupitia sera,sheria miongozo au maagizo,mtumishi wa umma ni kutekeleza tu,huwezi kutumia nafasi hiyo kupinga,na kuleta upinzani,hii sio Sawa,lazima utekeleze Yale wakubwa wa kisiasa wanataka serikali ifanye kwa niaba ya wananchi,sio jukumu lako kusema hiki hakifai!wewe hujachaguliwa na wananchi,waliochaguliwa ndio Wana haki na uwezo wa kutenda kwa niaba ya wananchi.

Sasa fikiria Dakitari wa hospitari ya umma,wakati waziri na nchi wanahamasisha chanjo ya COVID,yeye apite kimya kimya chini chini anawashawishi watu wasipime kwa vile ina madhara!!sasa serikali haiwezi kufanya kazi na mtu asiyekwenda na miongozo inayoitoa,lazima upigwe chini.
 
Watumishi wa Umma wengine ni kichefu chefu sana, unakuta mtu yuko ofisini kazi kukaa mitandao ya jamii kutwa hafanyi kazi, na huko mitandoni kutukana na kukashifu serikali ya CCM kwa kila namna, Mtumishi wa hivyo ni hasara sana kwani productivity ni zero, in a week unakuta kafanya kazi say 10% tu, kazi mitandao tu, acha ajifunze hana adabu kama Manara.

Ila wakikaa huko ofisini na kuisifia Serikali ni sawa hata kama hawafanyi kazi wanazopaswa?
 
Ndio inakuwa hivyo. Kuna wale chawa max pro. Wanasogeza file tu mahali tayari.
Hizi ofisi za umma uchawi mwingi. Bora mie kampani yangu jf tu. Group itakuwa ndio lililomponza. Watu wanaponda serikali kumbe kuna wapashkuna nao wao kazi yao kupeleka ukuda tu
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura😬

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
kumfukuza kazi ndio suluhisho?

Mama angefungua kesi sheria ifate mkondo wake

kumfukuza kazi ni one sided decision which ni kumuonea

Ingeenda mahakamani kesi izungumzwe ionekane kweli alitukana kwa proof....sio hizi maneno za one side na kwa vile ana madaraka basi

Nonsense
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

Nampata huyu jmaaa sna Ni jirani yangu Ni meneja wa itc wa trc hili swla ameniambi kitambo San japo tuhuma za Kwanza alizo kuwa anatuhumiwa nazo Ni kumtukana ndugai kumuita kilaza ktk group la wastup dhid ya lile sakata la kina mdee na wezake 19
Ni rasm sas jamaa Yuko mtaani rasmi kupambana na maish nnje ya trc

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ni kosa kisheria kwa mtumushi wa umma kukosoa. KUSHAURI SI SAWA NA KUKOSOA.
 
Nampata huyu jmaaa sna Ni jirani yangu Ni meneja wa itc wa trc hili swla ameniambi kitambo San japo tuhuma za Kwanza alizo kuwa anatuhumiwa nazo Ni kumtukana ndugai kumuita kilaza ktk group la wastup dhid ya lile sakata la kina mdee na wezake 19
Ni rasm sas jamaa Yuko mtaani rasmi kupambana na maish nnje ya trc

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
nchi ngumu sana hii eti mtu hutakiwi kuongea mawazo yako ni kupokea maelekezo tu! unachotakiwa ni kusifia vilaza tu kina Nduguyao na kusambaza ujumbe "anaupiga mwingi" hata kama huoni "huo mwingi"
 
Utakuta kuna mtu ali screenshot alichoandika akatuma management.
Nakufahamu hili sakata sna kwani naishi na huyu jmaa jirani sna. Na Ni rfk angu ishu ni kwamba aliandiak kwenye group la a level nadhani ndio alikuwa anamkashfu ndugai na mam kumbe ktk like group Kuna mashushu ndio wakampelekea kadogosa na kasogosa akamsimamisha kazi yule jamaa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom