Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Thread closed
 
Kilimo cha mdomo rahis kweli sio cha shambani. Ukodishe shamba kama huna, utafute vibarua, ununue mbegu, mbolea hii inayopanda kila siku, madawa, sumu za wadudu, booster. Hapo bado hujaibiwa
Ndio maana vijana wamekimbilia kwenye umachinga watu waliopata vimafanikio kidogo huwaona wanao hustle kuwa hawana akili hivi
 
Tukubaliane kazi za kufanya zipo kibao kweli ila je uwiano wa faculty zibazosomewa ni afifu na kuna shortage kubwa ya wataalamu, sayansi imekimbiwa kabisa, Tunataka madaktari bingwa, tunataka tunataka watu wa I.T, tunataka ma engineers lakini cha ajabu wengi wanakimbilia kusomea procurement, business administration, human resource lakini tunakosa watalaam kwenye maeneo mengine.. Hapa tuitake serikali waangalie hili motisha ziwepo kwa wanaosoma sayansi pia malipo yao yavutie, ili tutengeneze ajira kwa wingi kama taifa
 
Waziri wa biashara nchi hii huwa Hana kazi yoyote. Hakuna kabisa zaidi ya kupiga picha na kurekwbisha tai shingoni.
Ajabu sana kabisa. Inakuwaje mtu unakuwa na post kubwa kama Waziri unashindwa kufanya any remarkable reforms katika sekta yako.

Kuna radical changes zinahitajika kama tunataka kuendelea kweli. Mfumo wa kiutawala Tanzania ni mizuri sana ila mfumo wa uongozi ni mbovu. Mfumo wa kiutawala unamfikia kila mtu lakini aina ya viongozi wanaohusika kwenye mfumo huo ni shida. Huwezi kuweka diwani darasa la saba akasimamie mkurugenzi wa Halmashauri mwenye PhD/Masters. Mbunge darasa la saba au darasa la 12 la kufeli katika Zama hizi??

Hatuwezi kuendelea na mfumo wa darasa la saba enzi hizi ni kujidanganya wenyewe. Dunia imebadilika sana. Watu wanadhani innovation ni katika mambo makubwa tu kumbe hata mambo madogo. Yaani leo Waziri au Karibu Mkuu au Whoever at higher position, anachukuliwa pesa ya dalali ya mwezi mzima wa kodi ya nyumba anayolipa huku akijua hiyo pesa haina legitimacy yoyote. Na yeye anaona huo mfumo sawa tu,siku zinaenda. So bad.
 
Dar ndiyo soko lilipo maana serikali imeshindwa kufungua milango ku export nje so tunategemea kila kitu kipelekwe dar kiuzwe ni shida sana ndiyo maana dar ina yield pato kubwa kwenye pato la taifa
 
Siwanangi, nawaamsha wasikae sebuleni kwa dada zao miaka 3 ama zaidi wakisubiria ajira ambazo hazipo na hazitakuwepo.

Wajiajiri kwenye kilimo.
Kwa taarifa yako watu wengi wamejiajiri na hawakai tu bure so acha kunanga watu tembea huko vijijini ujionee na sio kuandika nadharia ka umebarikiwa mshukuru Mungu usione wengine wajinga
 
Kwa taarifa yako watu wengi wamejiajiri na hawakai tu bure so acha kunanga watu tembea huko vijijini ujionee na sio kuandika nadharia ka umebarikiwa mshukuru Mungu usione wengine wajinga
Mchukulie tu kama msukuma bila kujisifia moyo wake hautulii
 
Ungesema hivi, vijana wajiajiri kwa kufanya vitu wanavyovipenda hapo ndipo watafanya kwa moyo na maendeleo yatakuja sasa nchi nzima vijana wote wakiwa machinga, wakulima na bodaboda huo si unakuwa ni ujinga sasa.

Kwahiyo watu wakifanya vitu wanavyovipenda na wasomi wakawezeshwa kufanya vitu wanavyovipenda au kazi zinazoendana na fani zao ikiwa wanazipenda, uchumu wa nchi utapaa kwa kasi ambayo haijawahi kuonekana tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
 
Msomi mwenye digrii anapaswa kutumia kiasi kikubwa cha mbolea ili kuongeza tija ktk kilimo.
Jiweke kwenye miguu ya kijana asiye na ajira mtaji wake ni elimu huo uwekezaji kulima kibiashara anapataje, Ukizingatia umesema bado yuko anafua chupi za shemeji na hata Kama ardhi ni bure
 
hiyo ajira hakuna sasa na miaka yanazidi kwenda mko tayari kueendelea hivyohivyo na mishen town au nafuu tu mkamalizie maisha kwenye kilimo huenda mkatokelezea huko
 
Kuna watu wako kwa shemeji zao mwaka wa 4 huu wanasubiri ajira. Wanakula nn muda wote huu? Inashindikana vipi kula wanachokula wanapokuwa mashambani?
Mkuu unaongea vitu practically havipo,kula mashambani as if unapanda leo na vitu vinaota kesho!
 
hao ma I.T na engineers labda kama wewe unawahitaji ila serikali haiwahitaji wamejaa sana mtaani na serikali haiwapi ajira kama ulivyodai wanahitajika
 
Acha kupotosha watu. Mimi mikoa unayosema nimeishi mfano katavi kukodi shamba ekari Moja kwa ajiri ya kilimo cha mpunga inarange 150K Hadi 250K na kilimo cha mahindi,maharage,pamba na ufuta ekari Moja kukodi ni 50K . Mashamba ya Bure hupati in short Hakuna shamba la Bure.
 
Mkuu huna baya, umeconclude vizuri sana. nakazia AJIRA TUNAZIDAI!!!!
 
I agree kuna fursa kwenye kilimo, kina potential sababu kuna ardhi kubwa nzuri tu, ila wasomi wajengewe msingi itakayo watayarisha both mind and body kukabiliana na kilimo, tatizo sio upatikanaji wa ardhi peke yake, Utampa graduate wa engineering piece of land afanyie nini? Kuna kujua wapi ni pa nini,nitapigana vipi na madalali wa mazao etc hapo unaona umuhimu wa kuwa na basic knowledge ya kilimo, mzigo wote unarudi kwa serikali. Serikali inapoteza rasilimali watu kwa kutotomia fani za watu vyema. Engineering hakupaswa kwenda kilimo,na kama ulikua unataka akimaliza Huyu engineering graduate afanye kilimo basi ungemuandaa kwa ku incorporate agriculture kwenye syllabus aliyokua anasomea. Kumsomesha mtu miaka 3 halafu usimpe ajira ni wastage of resources! Things can be improved ila ni jukumu la serikali kujenga good infrastructure
 
hao ma I.T na engineers labda kama wewe unawahitaji ila serikali haiwahitaji wamejaa sana mtaani na serikali haiwapi ajira kama ulivyodai wanahitajika
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Eti labda wewe unawahitaji we mshikaji wewe , mimi naongelea serekali hazitoi motisha ni pamoja na kutota ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…