Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na ukapiga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!
Thread closed
 
Kilimo cha mdomo rahis kweli sio cha shambani. Ukodishe shamba kama huna, utafute vibarua, ununue mbegu, mbolea hii inayopanda kila siku, madawa, sumu za wadudu, booster. Hapo bado hujaibiwa
Ndio maana vijana wamekimbilia kwenye umachinga watu waliopata vimafanikio kidogo huwaona wanao hustle kuwa hawana akili hivi
 
Tukubaliane kazi za kufanya zipo kibao kweli ila je uwiano wa faculty zibazosomewa ni afifu na kuna shortage kubwa ya wataalamu, sayansi imekimbiwa kabisa, Tunataka madaktari bingwa, tunataka tunataka watu wa I.T, tunataka ma engineers lakini cha ajabu wengi wanakimbilia kusomea procurement, business administration, human resource lakini tunakosa watalaam kwenye maeneo mengine.. Hapa tuitake serikali waangalie hili motisha ziwepo kwa wanaosoma sayansi pia malipo yao yavutie, ili tutengeneze ajira kwa wingi kama taifa
 
Waziri wa biashara nchi hii huwa Hana kazi yoyote. Hakuna kabisa zaidi ya kupiga picha na kurekwbisha tai shingoni.
Ajabu sana kabisa. Inakuwaje mtu unakuwa na post kubwa kama Waziri unashindwa kufanya any remarkable reforms katika sekta yako.

Kuna radical changes zinahitajika kama tunataka kuendelea kweli. Mfumo wa kiutawala Tanzania ni mizuri sana ila mfumo wa uongozi ni mbovu. Mfumo wa kiutawala unamfikia kila mtu lakini aina ya viongozi wanaohusika kwenye mfumo huo ni shida. Huwezi kuweka diwani darasa la saba akasimamie mkurugenzi wa Halmashauri mwenye PhD/Masters. Mbunge darasa la saba au darasa la 12 la kufeli katika Zama hizi??

Hatuwezi kuendelea na mfumo wa darasa la saba enzi hizi ni kujidanganya wenyewe. Dunia imebadilika sana. Watu wanadhani innovation ni katika mambo makubwa tu kumbe hata mambo madogo. Yaani leo Waziri au Karibu Mkuu au Whoever at higher position, anachukuliwa pesa ya dalali ya mwezi mzima wa kodi ya nyumba anayolipa huku akijua hiyo pesa haina legitimacy yoyote. Na yeye anaona huo mfumo sawa tu,siku zinaenda. So bad.
 
Kama kilimo kingekuwa kinalipa,basi mikoa ya Kanda ya ziwa,nyanda za juu kusini ingeongoza kwa kipato kimkoa na mchango kwenye pato la Taifa,lakini unajua mkoa unaoongoza?ni Dar es salaam,mkoa ambao hauna shughuri kubwa za kilimo lakini unachangia asilimia 80 ya pato la Taifa!!
Kwa kila shilingi 100 inayoingizwa kwenye mfuko wa Taifa,asilimia 80 inatoka Dar!!hiyo mikoa inayolima ipo wapi??
Hoja zako kwamba vijana wakiomaliza vyuo waende mikoani,wakamate ardhi(ambayo ipo bwelele)walime,zimekaa kinadhalia tu na ni story za kwenye makaratasi hazina uhusiano na Hari halisi iliyopo kwenye mazingira yao.
Huwezi kutoka hapa ukaenda Katavi,ukachukua ardhi,ukaanza kulima mahindi,ukavuna!na ukapiga pesa ndeefu!?
Mfuko wa mbolea unauzwa 100000Tsh,gunia la mahindi linauzwa 20000Tsh!
Dar ndiyo soko lilipo maana serikali imeshindwa kufungua milango ku export nje so tunategemea kila kitu kipelekwe dar kiuzwe ni shida sana ndiyo maana dar ina yield pato kubwa kwenye pato la taifa
 
Siwanangi, nawaamsha wasikae sebuleni kwa dada zao miaka 3 ama zaidi wakisubiria ajira ambazo hazipo na hazitakuwepo.

Wajiajiri kwenye kilimo.
Kwa taarifa yako watu wengi wamejiajiri na hawakai tu bure so acha kunanga watu tembea huko vijijini ujionee na sio kuandika nadharia ka umebarikiwa mshukuru Mungu usione wengine wajinga
 
Kwa taarifa yako watu wengi wamejiajiri na hawakai tu bure so acha kunanga watu tembea huko vijijini ujionee na sio kuandika nadharia ka umebarikiwa mshukuru Mungu usione wengine wajinga
Mchukulie tu kama msukuma bila kujisifia moyo wake hautulii
 
Screenshot_20211014-175548_1.jpg
 
Kwani umachinga na bodaboda vinahitaji ujinga mkuu? Kazi ya elimu ni kupambana na changamoto za mazingira yako.

Nchi zetu za Afrika hazina mazingira yanayomfanya msomi aishi mtaani kwa elimu yake. Watu hawasomi vitabu, watu hawahitaji msaada wa kisheria, hawahitaji ushauri wa kisaikolojia, hawahitaji ushauri wa kuanzisha na kuendeleza biashara, hawahitaji ramani kujenga nyumba, hawahitaji ushauri wa kiafya na kitabibu. Haya yangefanyika wasomi wangekuwa lulu.
Ungesema hivi, vijana wajiajiri kwa kufanya vitu wanavyovipenda hapo ndipo watafanya kwa moyo na maendeleo yatakuja sasa nchi nzima vijana wote wakiwa machinga, wakulima na bodaboda huo si unakuwa ni ujinga sasa.

Kwahiyo watu wakifanya vitu wanavyovipenda na wasomi wakawezeshwa kufanya vitu wanavyovipenda au kazi zinazoendana na fani zao ikiwa wanazipenda, uchumu wa nchi utapaa kwa kasi ambayo haijawahi kuonekana tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
 
Msomi mwenye digrii anapaswa kutumia kiasi kikubwa cha mbolea ili kuongeza tija ktk kilimo.
Jiweke kwenye miguu ya kijana asiye na ajira mtaji wake ni elimu huo uwekezaji kulima kibiashara anapataje, Ukizingatia umesema bado yuko anafua chupi za shemeji na hata Kama ardhi ni bure
 
7 years (Primary)+4 years (O level)+2 years (A level)+4 years (Bachelor)=17years (Assuming hujafanya masters and PhD), nimepoteza miaka 17 shuleni, nikiamini kwamba hiyo miaka na jasho langu nililoliweka kwenye hiyo miaka ndiyo uwe mtaji wangu kupitia ajira rasmi, then uniambie futa hiyo miaka 17, ukaanze upya kwa kilimo!! Kuwa serious!! Je hiyo miaka 17 ningefocus kwenye kilimo bila kushurutishwa na serikali na wazazi kwenda shuleni unadhani ningemsumbua mtu kutaka ajira zenu? Ajira tunazidai sababu tumetumia jasho letu kwa miaka 17 ili kuipata hiyo ajira, ambayo since day 1 tunaingia shule tuliulizwa unataka kuwa nani, na tukajichagulia tu like Banker, Engineer, Rubani n.k.., then namaliza unaniambia nikalime?
hiyo ajira hakuna sasa na miaka yanazidi kwenda mko tayari kueendelea hivyohivyo na mishen town au nafuu tu mkamalizie maisha kwenye kilimo huenda mkatokelezea huko
 
Kuna watu wako kwa shemeji zao mwaka wa 4 huu wanasubiri ajira. Wanakula nn muda wote huu? Inashindikana vipi kula wanachokula wanapokuwa mashambani?
Mkuu unaongea vitu practically havipo,kula mashambani as if unapanda leo na vitu vinaota kesho!
 
Tukubaliane kazi za kufanya zipo kibao kweli ila je uwiano wa faculty zibazosomewa ni afifu na kuna shortage kubwa ya wataalamu, sayansi imekimbiwa kabisa, Tunataka madaktari bingwa, tunataka tunataka watu wa I.T, tunataka ma engineers lakini cha ajabu wengi wanakimbilia kusomea procurement, business administration, human resource lakini tunakosa watalaam kwenye maeneo mengine.. Hapa tuitake serikali waangalie hili motisha ziwepo kwa wanaosoma sayansi pia malipo yao yavutie, ili tutengeneze ajira kwa wingi kama taifa
hao ma I.T na engineers labda kama wewe unawahitaji ila serikali haiwahitaji wamejaa sana mtaani na serikali haiwapi ajira kama ulivyodai wanahitajika
 
Nimesema kwenye uzi wangu kwamba mashamba yanapatikana hiyo mikoa 5 bure kwa maana ya bila gharama. Unajitambulisha kwa mwenyekiti unakatiwa eneo linakuwa lako. Ama Kuna watu Wana maeneo makubwa wanatafuta mtu awe analima ili kupunguza msitu. Jamani ingieni kwenye kilimo.
Acha kupotosha watu. Mimi mikoa unayosema nimeishi mfano katavi kukodi shamba ekari Moja kwa ajiri ya kilimo cha mpunga inarange 150K Hadi 250K na kilimo cha mahindi,maharage,pamba na ufuta ekari Moja kukodi ni 50K . Mashamba ya Bure hupati in short Hakuna shamba la Bure.
 
7 years (Primary)+4 years (O level)+2 years (A level)+4 years (Bachelor)=17years (Assuming hujafanya masters and PhD), nimepoteza miaka 17 shuleni, nikiamini kwamba hiyo miaka na jasho langu nililoliweka kwenye hiyo miaka ndiyo uwe mtaji wangu kupitia ajira rasmi, then uniambie futa hiyo miaka 17, ukaanze upya kwa kilimo!! Kuwa serious!! Je hiyo miaka 17 ningefocus kwenye kilimo bila kushurutishwa na serikali na wazazi kwenda shuleni unadhani ningemsumbua mtu kutaka ajira zenu? Ajira tunazidai sababu tumetumia jasho letu kwa miaka 17 ili kuipata hiyo ajira, ambayo since day 1 tunaingia shule tuliulizwa unataka kuwa nani, na tukajichagulia tu like Banker, Engineer, Rubani n.k.., then namaliza unaniambia nikalime?
Mkuu huna baya, umeconclude vizuri sana. nakazia AJIRA TUNAZIDAI!!!!
 
I agree kuna fursa kwenye kilimo, kina potential sababu kuna ardhi kubwa nzuri tu, ila wasomi wajengewe msingi itakayo watayarisha both mind and body kukabiliana na kilimo, tatizo sio upatikanaji wa ardhi peke yake, Utampa graduate wa engineering piece of land afanyie nini? Kuna kujua wapi ni pa nini,nitapigana vipi na madalali wa mazao etc hapo unaona umuhimu wa kuwa na basic knowledge ya kilimo, mzigo wote unarudi kwa serikali. Serikali inapoteza rasilimali watu kwa kutotomia fani za watu vyema. Engineering hakupaswa kwenda kilimo,na kama ulikua unataka akimaliza Huyu engineering graduate afanye kilimo basi ungemuandaa kwa ku incorporate agriculture kwenye syllabus aliyokua anasomea. Kumsomesha mtu miaka 3 halafu usimpe ajira ni wastage of resources! Things can be improved ila ni jukumu la serikali kujenga good infrastructure
 
hao ma I.T na engineers labda kama wewe unawahitaji ila serikali haiwahitaji wamejaa sana mtaani na serikali haiwapi ajira kama ulivyodai wanahitajika
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Eti labda wewe unawahitaji we mshikaji wewe , mimi naongelea serekali hazitoi motisha ni pamoja na kutota ajira
 
Back
Top Bottom