Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Najaribu kuvuta picha kama Mwenyekiti angekuwa Sumaye/ Mwambe na katibu mkuu angekuwa Mashinji , dah CHADEMA ingekuwa katika hali gani sijui[emoji32]
Ila CHADEMA wana Intelijensia kali sana aisee.
 
Kwa taarifa yako, uimara na kukubalika kwa CHADEMA ilikuwa ni uwezo binafsi wa Slaa kujenga hoja. Mbowe alikuwa anatembelea nyota Slaa na ndio maana Slaa kaondoka Mbowe kaishia kuchemsha na kuomba maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu. Huyo Mashinji alikuwa takataka kama takataka nyingine.
Naunga mkono hoja yako kwa asilimia 💯
 
Wacha yajazane huko yataanza kuzodoana zodoana muda si mrefu.

Wana mapinduzi ya kweli songeni mbele.

Naona jamaa kwenye ile kesi ya viongozi wa CHADEMA yasemekana hakuwepo eneo la tukio hivyo hajumuishwi na wahalifu. Mwendesha mashitaka ameomba mahakana imwondolee mashitaka yote.
 
Yaleyale mana Lumumba yaliyosema Mashinji ni Zigo halibebeki pale CHADEMA leo eti imekuwa turufu.
 
Ukiangalia tu huo wasifu wake, inatosha kukuonyesha kwamba huyu bwana ni "opportunist."

Sasa sijui kama sifa hiyo ni nzuri au mbaya.

Kuna watu hutoa 'premium' kwa yeyote kwa kitu kinachoitwa "uaminifu."

'Opportunist' na 'uaminifu' ni vitu mbali mbali kabisa.

Bila shaka yoyote, "Jamaa" hapa kalenga kwenye 'opportunity' ya 'uwaziri' tu kwenye ngwe ifuatayo!
Naona safari yake ndefu inaelekea kutimia.
 
Hii maana yake ni moja tu kwamba CCM ni chama bora kuliko Chadema.

Kama wote hawa uvumilivu umewashinda na wamekimbilia CCM basi tatizo liliomo ndani ya Chadema ni kubwa kuliko linavyofikiriwa.

Hii siyo picha nzuri kwa wanachama waandamizi wa chama kikuu cha upinzani kukimbilia chama tawala.

Maendeleo hayana vyama!
 
Slaa alikua na nguvu Sana Chamani,lakini alivyoondoka alindoka na mke wake tu,Zito alikua Ana NGUVU Sana Chamani kwa kweli alivyoondoka alindoka na vikundi vya watu, lakini cha kushangaza CHADEMA imeendelea kuwepo,ukimya huu wa CHADEMA ni ukimwa wa kuwekewa minyororo miguuni,wakitaka kujua Kama ukimya huu ni wa kifo, wafungue hiyo minyororo.
Uoni kuondoka kwa Slaa uwawishi wa CHADEMA kupungua?
 
Je, Mashinji atahudhuria ile kesi inayomhusuu na viongozi wengine wa CHADEMA?

..kuna siku nili-post humu ndani kwamba Salum Mwalimu ahamie CCM ili yeye na wenzake wapate unafuu ktk ile kesi.

..Wema Sepetu alikwenda kifungo baada ya kuhama CHADEMA na kuachukua mawakili toka CCM.

..Natumaini itakuwa hivyo kwa Dr.Mashinji na huenda ikawasaidia na wenzake kuchomoka ktk kesi ya maandamano na kumuua Aquilina.
 
Bado ngome haijatikisika,hao walioondoka wote ni wepesi wepesi tu!
Kinachowaondoa ni uchu na tamaa ya madaraka,sasa wamehakikishiwa kuwa CCm watashindishwa hata wakishindwa!Na kwa yaliyotokea kwenye chaguzi ndogo pamoja na serikali za mitaa,wameona hawawezi kurisk kubaki upinzani!Hao ni wale wenye mioyo ya mshumaa!
CDM sio lelemama!
 
Karibu nyumbani mzalendo mashinji, chagua jimbo lolote tutakupa ugombee ubunge na wote mliobaki upinzani mkuje huku ubunge Ni Kama kumsukuma mlevi tu mnasubiri Nini? wajanja wako huku.... thanks
 
Yale ya CCM ilipokuwa tishio, waliokosa vyeo ndani yake walikimbilia Chadema na kupokewa kwa bashasha na matambo. Lakini Leo hii tumeshuhudia walio omba uongozi ndani ya Chadema na kukosa nafasi wanahamia CCM na wanapokewa kwa mbwembwe zote mbele ya kamera na waandishi wa magazeti.

Tumeona Sumaye, Mwambe na sasa Dr Mashinji wakipokewa na Polepole na nahisi bado wengi tuu walio garagazwa uchaguzi wa ndani watamiminika huko wakiimba "ndani ya Chadema hakuna demokrasia bali ipo CCM".

Hii ni dhihirisho kuwa kwa sasa Chadema ndio tishio kiasi kwamba ikitema oil chafu CCM kwake bado inafaa kuendeshea mitambo yao mikuu kuu na iliyo chakaa.

Hivi Leo hii Chadema wakiamua wamteme mtu kama Lissu na atangaze kujiunga CCM, Lumumba na Magogoni kazi zitafanyika kweli?

Au itakuwa mapumziko ya sherehe mwanzo mwisho?
 
Vyeo vya CCM vinafanana na vyeo vya Chadema?? Sidhani.
 
Hivi kwanini tuasiamue hao wanaohama vyama tukiwaona barabarani tuwazomee,tuwarushie mawe ili iwe fundisho kwa wengine, nchi haiwezi kuendelea tukiwa na viongozi wanafiki
 
Kwa ufahamu wangu ninachokiona hapa nikuwa tunapoelekea Hali ya uchumi itakuwa ngumu sana. Maana hii kuhamia CCM niwazi kuwa Wanasiasa wamepoteza Financial Security Sasa Wameamua kutafuta Political Security.

Njaa Mgunduzi Njaa haina upendeleo. Hata mtoto mchanga anayezaliwa Leo anaiju njaa. Maajabu yanaendelea.
 
Back
Top Bottom