Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Yule dikiteta uchwara tunamfahamu anazuzuka na PhD holders usihofu CV yako itakutatulia njaa zako.
 
Si Msukuma anamfata msukuma mwenzie? kuna shida gani mwacheni akale pesa za washamba maana hakuna jipwa zaidi ya kununuana ila nawahakikishia washidi watakuwa wale waliobaki.
 
Kama hili ni kweli (tweet), maana naona shaka hata kukubali kirahisi kwamba ni kweli, basi tuna matatizo pande nyingi sana.

1. CHADEMA kuna matatizo kwa kutokuwa na chujio linaloweza kuwachuja watu kama hawa kabla ya kuwapa uongozi mkubwa.

2. CCM kuna matatizo kwa kukubali watu mamluki kama hawa na kuwafanya mbiu ya ushindi. Huyu Mashinji kimsingi akama kweli kaandika haya, kakubali umalaya wa kisiasa.

3.Tanzania tuna matatizo kwa kuweza kuwa na mtu anayekubalika kama msomi, halafu akawa na upeo mdogo hivi.
 
Kufuatia kifo cha Rais Daniel Arap Moi mwaka huu 2020 mwezi February na vipindi vya televisheni vya Kenya kuwaita wanasiasa waKenya kutoa uzoefu na mapito yao kupigania utawala wa vyama vingi Kenya nimebaini wasomi wa Tanzania ni waoga sana. Na tusitegemee kuwa na kundi kubwa la wasomi wakaoongoza mapinduzi Tanzania iweze kupata TumeHuru, Katiba Mpya na Uchaguzi Huru.

Nchini Kenya waliokuwa wanasiasa viongozi ktk mapambano ya kudai tume huru, katiba mpya na uchaguzi ni wengi mno kisasi baada ya mabadiliko wengine wakawa wabunge, majaji na magavana wakiendeleza misimamo yao uhakikisha uhuru wa mihimili ya dola.

Mtu kama Vincent Mashinji anaianika kada ya wasomi waTanzania ambao wpo katika kambi mbalimbali za siasa lakini mioyoni mwao hawaamini wanachosema. Na ndiyo maana tunaona hamahama nyingi ili kulinda matumbo yao na siyo misimamo yao.

Bora kuwa na wasomi,wanaharakati wachache wenye imani nawanachokipigania kulikokuwa na kundi kubwa lisilo na msimamo wakipewa nafasi za ulaji aukuhongwa ghafala wana ubali na kuzifukuzia matamanio ya haja za matumbo yao.


 
Ndiyo maana nimesema Mimi Zogwale kuwa sitakaa niwe wala kuwaza kuwa mwanasiasa. Nitaendelea kuitii na kujenga mkono serikali ilivyo madarakani hasa Ile ambayo maendeleo ni kipaumbele na inataenda haki kwa wananchi wake bila kujali itikadi ya vyama.

Nikiangalia clip za hao wanaohama CCM kwenda upinzani na upinzani kwenda CCM unaona ni waongo mno. Tena aibu kabisa kumeza maneno yao. Mfano Mzuri Lowasa na Sumaye. Huwa inachukua sana kudhalilika na kuhakikisha familia na wanaonihuhu. I hate kukengeuka.

Ukiwa neutral unafurahia maisha na kuunga juhudi zote positive na zile juhudi ovu unajinyamazia kimya ili siku na miaka na maisha yasonge. Usiku unalala usingizi mzito kama baby tu huna hofu.
 
..Hili jibu limepungukiwa busara.

..wao wangemshukuru Dr.Mashinji kwa mchango wake, na kumtakia safari njema ya kisiasa.

..maneno aliyoyasema Mrema hayakupaswa kusemwa na kiongozi, yalitakiwa kusemwa na wapambe na mashabiki mitaani na kwenye mitandao.
 
Huyu alibaki chadema kwa sababu ya cheo tu, katibu Mkuu ambaye angeifaa chadema Ni albanie marcus
Katibu mkuu ni mtendaji mkuu wa chama. Ni lazima awe mtu mwenye kichwa kizuri cha fikra kama ilivyokuwa Slaa na Mangula, siyo mtu wa vijembe kama Makamba au Mnyika. Angalia sasa chaguo la Mbowe! Mnyika!

Kwa ujumla Mbowe hataki Challenges akiamini kura zake anazo wakati wowote atapewa kura na wananchi na kwa uhakika zaidi, wachaga. Ruzuku itakuja na baadaye atapiga pesa.
 
By Sangu J

Leo Februari 18, 2020 tumeshuhudia uamuzi wa msomi mwingine na Kigogo ndani ya CHADEMA Dkt. Vicent Mashinji, na kuamua kuingia kwenye na Sera za Chama cha Mapinduzi.

Dkt. Mashinji ameeleza sababu mbalimbali za uamuzi wake lakini kubwa ile anayosema alitamani zaidi kuwa sehemu ya watu wanaoleta maendeleo katika nchi yake ya ahadi ya Tanzania.

Japo wanasema ni uamuzi wake kikatiba lakini mimi napenda nijadili kidogo athari zinazoweza kujitokeza kwa chama chake cha zamani hasa kuelekea kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na baada ya uchaguzi, na moja ya athari kubwa wanayoweza ipata CHADEMA kuondoka kwa Mashinji ni kukosa mvuto kwa wasomi.

Unajua kwa siasa za Tanzania Chama Tawala kwa kawaida huwa anakua na mvuto kwa kundi la wasomi kutokana na kuwa nafasi mbalimbali ambazo zinaweza kuwafaa wasomi, lakini vyama vya upinzani nchini kitu pekee kinachoweza kuwavutia wasomi ni uwepo wa wasomi wenzao ndani ya chama, ndiyo maana miaka fulani uliikuta CHADEMA iliweza kupenya mpaka Vyuo Vikuu kwa kuwa na wasomi mbalimbali kama Prof. Safari, Baregu, Kitila Mkumbo, Esther Matiko na wasomi wengine kama Slaa, Dkt. Mashinji, na kuliifanya CHADEMA kuwa kivutio kwa baadhi ya wasomi kwa sababu wenzao walikuwepo huko.

Kuondoka kwa Prof. Safari, Slaa, na Mashinji ni miongoni mwa mapigo ambayo yameikuta CHADEMA na yanaweza kuipoteza kuelekea uchaguzi wa 2020 na 2025 kwa sababu kuna baadhi ya Analysis za kisomi wanazikosa kama ilivyo kwa CCM.

Dkt. Slaa alishawahi kusema siasa ni mchezo wa hesabu za kupata watu, na mfumo bora zaidi ambao ulikuwa unatumiwa na vyama vya upinzani ni kukuza vijana kutoka Vyuoni ambao idadi kubwa huwa wanavutiwa zaidi na Prof. na Dkt.

Naiona CHADEMA itakayokuja kufanana na CUF miaka 10 baadaye kwa sababu ya kukosa wasomi, ambao chachu ya kufanya tafiti ndani ya chama.

#MaoniYangu #KijanaMzalendo
#IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh, hapa kuna kitu siyo bure...

"If you can't beat them, join them, then, fight them from within...."
 
Back
Top Bottom