Ally Dangote auawa jijini Arusha
Thubutuu!

Mbona wakati akiwa hai mlikuwa mnajificha uvunguni kama vitoto vya kuku!

Mwamba akisugua jambia lake kwenye jiwe wote mnatimka nduki mnaenda kujibanza kwenye sketi za dada zenu! Chezea Ali Dangote wewe!

Amekufa ndio unajifanya kubweka kama MANUNU! THUBUTU YAKO!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mmoja kati ya walinzi wa Polisi Jamii ambaye alishiriki kwenye msako wa kumtafuta Ali Dangote, kijana mhalifu anayetajwa kuwaua takribani watu wanne, amesema kijana huyo alianza kufanya mauaji, siku ya Mechi ya Simba na Yanga (Novemba 5, 2023).

Amesema alianza mauaji hayo baada ya kuachiwa kutoka jela ambapo juhudi za kumsaka zilikuwa zikigonga mwamba mpaka alipopatikana jana, Novemba 20 na kuuawa.

Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwa kutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni

Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi, majira ya Leo mchana wananchi wenye hasira kali wamemtia nguvuni na kumpokonya uhai.
---
Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wamejitokeza kushuhudia mwili wa kijana anayetambuliwa kwa jina la Ally Dangote (19) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, akidaiwa kutoroka baada ya kukamatwa.

Dangote kabla ya kutajwa kuhusika na matukio ya mauaji alikuwa rumande Magereza kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji na hatimaye mwaka huu aliachiwa huru na Mahakama kutokana na kukosekana ushahidi lakini alikamatwa tena baada ya tuhuma za uhalifu mwingine.

Akizungumzia kifo hicho leo Jumatatu Novemba 20, 2023 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salvas Makweli amesema Dangote ameuawa baada ya kupata jeraha la risasi wakati akiwatoroka polisi.

"Ni kweli huyu mtuhumiwa alikuwa anasakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi na mauaji na leo baada ya kuwekewa mitego tulimkamata na wakati anakwenda kuwaonesha wenzake aliruka kwenye gari na ndipo alipigwa risasi na kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki akiwa hospitali," amesema.

(Imeandikwa na Mussa Juma)

Pia soma > Kibaka maarufu, Ally Dangote atiwa mbaroni Arusha

View attachment 2820024
Ally Dangote(Kulia)​
OLEWAKE ARUDI TENA.....
 
YAANI KAKIJANA KA MIAKA 19 KANATETEMESHA JIJI ZIMA LA UTALII KWA SILAHA YA KISU TUU, BASI KANGEJIITA HATA KOMANDO KIPENSI KULIKO KUCHAFUA JINA KUBWA HIVYO LA DANGOTE.
ILA JAMII INAJUAGA KABISA VIJANA WAHALIFU WA MTAA NDIO SABABU WAKIWACHOKA WANATOA HUKUMU ZAO ZA MTAANI.
 
Jamii hisiyotaka kuwajibika kwa matendo yake yenyewe huzalisha akina Ally Dangote wengi tu.

Jamii inayoshindwa kumdhibiti kijana wa kiume wa umri wa miaka 19 tu ni jamii iliyoshindwa kwa maana katika uso wa ulimwengu huyo bado ni mtoto.

Mtoto alieua watu 9 na mara zote akafanikiwa huku akijeruhi wengine.

Mtoto mmoja alieishinda jamii ya maelfu ya watu wazima wa kila kariba mpaka jeshi la polisi.

.

Wameshamshughulikia. Walimpa nafasi hakuitumia.
 
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwa kutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni

Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi, majira ya Leo mchana wananchi wenye hasira kali wamemtia nguvuni na kumpokonya uhai.
---
Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wamejitokeza kushuhudia mwili wa kijana anayetambuliwa kwa jina la Ally Dangote (19) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, akidaiwa kutoroka baada ya kukamatwa.

Dangote kabla ya kutajwa kuhusika na matukio ya mauaji alikuwa rumande Magereza kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji na hatimaye mwaka huu aliachiwa huru na Mahakama kutokana na kukosekana ushahidi lakini alikamatwa tena baada ya tuhuma za uhalifu mwingine.

Akizungumzia kifo hicho leo Jumatatu Novemba 20, 2023 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salvas Makweli amesema Dangote ameuawa baada ya kupata jeraha la risasi wakati akiwatoroka polisi.

"Ni kweli huyu mtuhumiwa alikuwa anasakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi na mauaji na leo baada ya kuwekewa mitego tulimkamata na wakati anakwenda kuwaonesha wenzake aliruka kwenye gari na ndipo alipigwa risasi na kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki akiwa hospitali," amesema.

(Imeandikwa na Mussa Juma)

Pia soma > Kibaka maarufu, Ally Dangote atiwa mbaroni Arusha

View attachment 2820024
Ally Dangote(Kulia)​
Rest in Hell kwake kijana wa hvyo huyo,

Sent from my TECNO WX3LTE using JamiiForums mobile app
 
Tuangalie case ya huyu Allay Dangote.

Angalia size yake na size ya hao Askari aliojaribu kuwatoroka.

Tuangalie kwa u ndani hayo mazingira na namna ya ukamataji unaoshindwa kumdhibiti mtoto wa miaka 19 akiwa chini ya ulinzi mpaka apate mwanya wa kutoroka.

Na mwisho tuangalie kwanini watuhumiwa wote wanaojaribu kutoroka ni lazima wauawe kabisa badala ya kuvunjwa miguu (kwa risasi) ili kumaliza hizo mbio?

Tukubali tu ni jamii tuliyoshindwa. Mitaa inawatengeneza kina Ally Dangote then mamlaka zinazopaswa kudeal nao kwa kufuata utaratibu tuliojiwekea sisi wenyewe, zinafanya maamuzi ya kutumia njia ya mkato kumaliza tatizo jambo ambalo badala litoe matokeo chanya linaleta matokeo tofauti na hatimaye a circle of misery is created.

Kuna watu lazima wawe eliminated ili Dunia iwe salama
 
Nani angeenda kutoa ushahidi kuithibitishia mahakama kuwa aliua? Mahakama haiwezi kupata ushahidi wa uhalifu, jamii inayomzunguka ndiyo inayomjua. Hayajawahi kukukuta ndiyo maana unasema R.I.P kwa muuwaji aliyeuawa. Wakati mwingine tukubali tu kuna wahalifu tunaishi nao kwenye jamii zetu inatakiwa wasiishi wanasumbua kuanzia wazazi wao. Jamii za zamani wazazi walikuwa wana declare kwamba huyu katushinda wazee wanamaliza wenyewe. Huwezi kuishi mtaani mnashindwa hata kutuma mtoto dukani kwa sababu ya pimbi mmoja ambaye mnamjua
Vema.
 
Back
Top Bottom