Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ok, hakuna alichofanya.
So what!
 
Ametoa ajira kwa watoto wa masikini waliouza mashamba na ng'ombe kusomesha watoto wao kwa kozi za ualimu na afya
 
Elimu bure ililetwa tokea mwaka 2015 na sio yeye ililetwa na mwendazake na ndo alisimamia hili yeye samia hajaja na sera ya elimu bure wacha kudanganya
Utake usitake Samia ndiye Rais wa JMT na Magufuli keshajifilia zake na hatorudi tena!!
 
Wakulima wamepata fursa ya kuuza mazao yao kwa bei kubwa toka 2015
 
Masikini wamejengewa vituo vya afya na madarasa pasipo kutoa mchango wa pesa hata jero
 
Sasa wewe unataka kusema huyu Ni Rais wa awamu ya tano , Hivi hata mtoto wako hapo nyumbani akikuuliza huyu Ni Rais wa awamu ya ngapi utamwambia awamu ya Tano? Akikwambia umuhesabie Marais utamwesabiaje mwanao Hadi mh mama yetu Samia Naye awe wa awamu ya Tano?

Pili huyu siyo kaimu Rais Bali Ni Rais kamili wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ndio maana aliapa kiapo walichoapa Marais wengine walio mtangulia, Hakupewa kiapo Cha ukaimu Urais na Wala hakuna kitu Cha namna hiyo katika katiba yetu, Kama unacho tuwekee hicho kifungu kinachosema huyu Ni kaimu Rais,

Mama Samia Suluhu Hassan Ni Rais kamili wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwenye mamlaka kamili ya Urais na uamiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Ni Rais kamili mwenye Amri zote na nguvu zote za Urais,
 
Amerudisha furaha na amani

Ameondoa ukabila na udini

Ameondoa uporaji kupitia TRA

Ameruhusu mazungumzo ya kulipa Kodi kidogo kidogo hata kama nadaiwa TRA 200 milioni kwa hiyo biashara zinaendelea.

Penalty za kijinga TRA zinaondolewa, unalipa Kodi ya msingi na riba tu.

Chuki za kisiasa zimepungua.
Bei ya mazao imepanda kwa sasa kilimo ni biashara yenye uelekeo
 
Kuweka kiti ndani ya kiti, hili ni jipya kama ajabu litakuwa la nane
 
Watanzania hamna shukrani.
Huyo mama wa watu kwa uwezo wake kajitahidi mno kuongoza hili taifa la watu wavivu na wanafiki.
 
Chuki hujaza ujinga
 
Miundombinu yote ni mwendazake na kikwete na sio yeye
Kama bado inajengwa unasemaje mwenda zake na kikwete!?..kikwete si rais,na magu kafa..wanajengaje miundombinu!?...Samia alisema isijengwe utasemaje!?
 
Kwamba rais akiongoza kwa miaka mitano Kisha uchaguzi inayofuata akashindwa,hiyo haihesabiki awamu kwa kuwa haijatimu miaka kumi!?...mgombea mwenza wa urais siyo mgombea!?..kwamba kipimo Cha awamu ni ilani!?..
 
Umekalisha matko yako chini unachati kwa amani, hiyo ni kazi ya Samia
 
MBOLEA YA RUZUKUUU, SOKO LA MAZAO KUFUNGUKAAA, AMANI NA UTULIVUU KUONGEZEKAA
 
Kama kweli tuthibitishe kwa 'Tume huru ya uchaguzi'.. ....!!
 
nilichokiona kutoka kwako ni chuki TU kwani watumishi sio wananchi ? kama haujui Kuna watumishi wa kipato Cha chini kabisa ndio aliowagusa kweny annual increment ya mwaka huu .
Pili Zungumzia suala la ajira Mama Katoa vibari vya ajira kada mbalimbali Tena Kwa idadi kubwa sana sasa nenda kitaa uliza wangapi wamerudi mtaan kwasabab ya kumaliza mkataba huko JKT utakimbia kaka operation kibao zimerudi kitaa coz mwamba hakutoa Ajira. Pia Kuna upepo ulipita ikaonekana hata hizi elimu zetu sio kitu tena watu Wana graduate unakuwa nao kitaa Hamna michongo lakin kwakipindi hiki dhana ishaanza kufutika watu wanachukuliwa.
kwahy kiukweli Mama anagusa maisha ya watu akiongezwa mshahara mtumishi yule Ambae si mtumishi atapata pa kupiga rungu pesa itazunguka kariakoo nyomi itaongezeka machinga Maji watauza ni hayo
 
Samia yeye anafukuzia tuzo za umoja wa maifa. Yani anaenda kinyume na magu

SSH nilikuwa na matumaini lkn sasahivi naona aibu tu kusema bora ya mwenda zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…