Samahani mkuu...mie sio mbishani ila nimetaka tu kuweka vitu sawa na wala sina muda wa kutupiana maneno ya hovyo na mwingine.
Huyu mama samia anajikanyaga kwa kuwa...Mara baada ya kupitishwa kuwa rais wa TZ baada ya mzee.magu kufariki ilitakiwa yeye awe raisi wa 6 awamu ya tano...Simply:-
Kwanza, Kwa kuwa hawamu hiyo haikumalizwa na ili ikamilike ni kipindi cha miaka.10.
Pili, Yeye ni member wa chama sawa ha alichotoka hayati yaani CCM.
Tatu, Hakuna Awamu za kuteuliwa au kukaimu katika kitiba ya nchi yetu...bali awamu huja baada ya chaguzi(kupigiwa kura) kufanyika na mgombea husika kupatikana, kuthibitishwa na kuapishwa.
Nne, Na ikumbukwe kila awamu(kipindi cha miaka.10)...inakuja na Ilani/Malengo yake ya utekelezaji.
Turudi kwenye mada....
Hivyo kwa kuzingatia ivyo hapo juu...YAANI MAGU HAKUMALIZA AWAMU YA 5(MIAKA.10), YEYE RAIS.SAMIA HAKUCHAGULIWA KWA CHAGUZI NA PIA BADO ANATEKELEZA ILANI YA AWAMU YA 5 YA MAGU, Hakustaili kuitwa rais wa awamu ya 6...kwa kuwa hadi ivi sasa hakuna ilani ya awamu yake bali bado ni ya magu.
Na kama wewe utaibuka kusema hii ilani iliyopo ni ya awamu ya.6 EBU TUKUMBUSHE YEYE ANAYEJIITA RAIS WA AWAMU YA.6 ALIINADI WAPI ILANI YA AWAMU YA 6?(maana ilani kabla ya kutekelezwa ni lazima inadiwe na ilani hunadiwa kipindi cha chaguzi kwa mujibu wa katiba yetu ya 1977)
Hivyo basi, alistaili kuwa raisi wa 6 katika awamu ya tano(yaani anamalizia utekelezaji wa ilani ya magu/Ya CCM 2015-2025), then kwa mujibu wa katiba kwa kuwa alikaimu muda uliosalia kwa kipindi kilichozidi miaka.3( yaani miaka.4 iliyobakia)...katiba itamruhusu kugombea miaka.5 tu inayofuata akitaka kuendelea na sio zaidi.
Lakini kama angekaimu miaka mitatu au pungufu ya hapo...katiba ingemruhusu kugombea kwa kipindi cha miaka kumi kama akitaka kugombea, yaani hiyo mitatu, miwili au mmoja isingehesabika iliyosalia kwa huyu aliyefariki isingehesabika.
Hivyo, Ata mambo mengi MNAYOSEMA AMEYAFANYA NI UONGO KWA KUWA...MASUALA HAYO YALIKUWEPO KWENYE ILANI YA CCM MWAKA.2015-2025(Awamu ya tano[miaka.10])...hivyo kwa sababu yeye ni awamu ya 6...Fanya utuletee apa ilani ya awamu ya 6 unayoijua wewe na vipaumbele vyake wote tuvichambue apa jukwaani na useme aliinadi wapi?