Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Huyu mama ataongoza kama kiongozi wa kawaida.....
sidhani kama ana vision....
ie anataka kutupeleka wapi katika levo za kiuchumi...

Uchumi gan,kwan hapa tulipo tumeachiwa uchumi gan na huyo Hayati mwendazake..??

Ni kama nyerere alivyoiacha nchi KWA mwinyi tuh,mama ana kaz kubwa ya kufufua uchumi kwanza na iman ya uwekezaji KWA Taifa hili,

Mbona mnaongea kama mmelewa hivi,anasema alikuwa anapambana na ufisadi na rushwa,mbona ameondoka na madudu yako vile vile Tena ni MAKUBWA zaid
 
Enzi za utwana zilikuwa enzi za jiwe alipokuwa amefikia hata hatua ya kuweza kuamua kutupangia muda wa kulala na kuamka bila sisi kuweza kufurukuta
Ukweli wa Mambo hatuna kiongozi ni matatizo matupu tutajuta ,sababu tunarudishwa enzi za ubwana na utwana .mama upeo wake ni mdogo sana na ujasiri Hana hata kidogo.
 
Inapendeza sana kuona wanafiki wanaumbuana ...!

CCM mlipora kura za kwenye box mkajipa ushindi wa mezani mkiuita wa kishindo...

Mkadai wapinzani wanawachelewesha mkataka Jiwe atawale hadi atakapochoka....

Leo mnashikana mashati na Mama aliyesema hata wasiposhinda wataunda serikali...
 
Mleta mada unajifanya humfahamu jiwe wewe ??? Nani mwenye ujasiri wa kumpinga Hadharani ndani ya Serikali kama akina Lema walipojaribu kusema ukweli walijikuta wako Jela?

Acheni roho mbaya mpeni Mama Muda atafanya Mambo makuu. Nyota Njema huonekana asubuhi.
 
Sijui kwa nini mzee yule alisema tutamkumbuka!!! Hizi speech future yetu sijui

Tunaamini ni mtu mzuri lakini pia washauri wake wajitaidi kumsa
 
Aliyepita alikuwa hashauriki wala haambiliki.
VP alibaki hapo akisubiria fursa kama hii ijitokeze aonyeshe uwezo wa kuongoza bila kuteka wala kutesa.
Ukosoaji unaofanya mleta mada ingekuwa wakati wa mwendazake ungeenda pimwa mkojo.
 
Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!
[/QUOTE]
nakuunga mkono hata kama alimchukia sana mwenda zake apime kaurizake yake maana bado kuna watu wengi bado wanaona mwendazake alikuwa sahihi kwenye baadhi ya mambo, matendo yawe mengi kuliko maneno asionyeshe yeye ndo mdomo wa kikwete ni mapema sana kwa wao kutangaza ushindi.Kama alivyokuwa mnafiki kwaJPM watakuwa wanafiki kwake nawachumia tumbo walisha msoma sasa ni mwendo wa kukashifu utawala uliopita ambao kwa hakika NI huu huu wake na aliyeondoka ni , sioni tofauti maana hata yeye anatumia vitisho kwa sauti Nyororo mimi nbado nampamuda maana madaraka siku za mwanzo ni sawa na new money mpaka uzoee (New Money Spends by Trends, Old Money Spends by Tradition)
 
Nahisi kama mleta mada ana multiple ids maana si kwa majibu hayo

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Kuna kundi kutoka SUKUMA & CO .LTD na wamepewa kazi maalum ya kupinga na kukosoa kila hatua ya Rais mama samia kwa sababu tu mipango yao ime kwama baada ya waliye mtarajia awe mpendwa wao wa kudumu kutwaliwa na ndio hao mnao ona wana haha huku mitandaoni kutukana na kukejeli kila hatua ya Mh. Samia suluhu na kinara wao mpanga mikakati anafuatiliwa bila yeye kujijua.
 
Back
Top Bottom