Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Huu uzi ni kama ule wa anaefahamu jpm anatupeleka wapi ambao uliwekwaga sticker note.

Nadhan watu wanataka tu umaarufu, mtu hana hata siku 100 ofisini,mbongo kashakuja huku kuanzisha uzi eti hajui Rais anatupeleka wapi.

Determinant factor yako ni ipi...huoni ni mapema sana kuanzisha uzi judgemental kama huu.
 
Samia yuko very real, je ni mara ngapi alitaka kujiuzulu?
.usichokijua sio kwamba watu Walimpenda JPM ,bali wengi tuipigia kura ccm kwa ili tumiliki ndege,umeme ,barabara,maendele ya vitu. Tulikataa Tundulisa kwa sera ya maendeleo ya watu.
 
Sio kweli amejifunua bayana kwamba hakukubaliana na nmna alivyokuwa anawaongoza ila haijulikani ni kwanini hakujiuzulu kujenga heshima iliyo bora kuliko kumsema vibaya marehemu ambaye kwa sasa hana kauli ya kujitetea kutokana na kile anachokiagiza sasa hivi kufanyika. Amesikika akisema ataunda tume kufanya utafiti kama wakubali au kukataa kupokea chanjo ya UVIKO wakati akijua kabisa hayati alishaunda tume hiyo tayari kufanya utafiti huo na majibu wayawakilishe kwenye mamlaka husika kwa hatua kama sio kudhoofisha urithi (undermining legacy) huo ni nini ambao na yeye alikuwa sehemu yake?

Je, walikuwa na uadui baridi wakiviziana kwa muda mrefu ili tujue na yeye ashauri kuwa makini na washauri wa karibu ndio humpoteza kiongozi?
man umepotosha mbaya. kwanza kwenye kauli zake bi mkubwa. hakuna mahali kasema eti ataunda team ya kukubali au kukataa chanjo.

alichosisitiza ni kuwa tanzania si kisiwa, tuna intergration na mataifa yenye covid.
tume itakayoundwa ni ya kufanya tafiti na kutoa ushauri nn kifanyike ili kupambana na madhara ya covid.

pili hakuna mahali mama kamsema marehemu vibaya. sijasikia kwenye kauli yake akisema hakukubaliana na uongozi wa JPM. Hakuna

muache kumlisha rais maneno yenu.
 
Bora Hata magu tulikua tunamjua ni mtambo na hajifichi wala nini , sasa huyu Mama anajifanya anatupooza kinafiki wakat Moyo wake anaujua wenyewe ulivyo
 
She is not our president , we never elected her, hatumtaki, huyu Mama sio mtu mzuri , my instincts are seldom wrong
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Mnapenda kuambiwa wanyonge na wazalendo 'Things will change for the better, though not overnight we have to be patient '
 
Ni kazi kubwa! Wafanyakazi wanataka ongezeko la mishahara, wafanyabiashara wanataka mishahara ipungue (maana yake kodi ipunguzwe), kazi kwake SASHA.
Kodi ilishapunguzwa kwenye ngazi ya chini tu; ngazi ya kati na juu ni kidogo sana. Mshahara ndio unatakiwa kuongezwa maana mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2015 kinyume na sheria za kazi. Vyama vya wafanyakazi na chama cha waajiri KIMYA. Ukiwauliza je, kiongozi anaweza kumudu maisha kwa malipo ya shilingi 80,000/= hadi 150,000/= kwa mwezi kwenye miji yenye kiwango cha hali ya maisha kuwa juu kama Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma nk
1. Makato NSSF-8,000-15,000
2. Gharama chakula mlo mmoja shilingi 2,000 mara tatu mara watu wanne tegemezi inaleta jumla shilingi 24,000/= kwa siku mara mwezi mzima jumla kuu shilingi shilingi 720,000
3. Usafiri kwa siku shilingi 3,000 mara mwezi mzima angalau siku 26 au 28 jumla shilingi 84,000
4. Gharama za kumwezesha mtoto kuhudhuria shule ijapokuwa ada inalipwa na serikali kwa kiwango cha chini ni shilingi 300,000 kwa mwezi
5. Gharama za matibabu ni kubwa sana (angalau matumizi ni 150,000) kwa mwezi

Gharama kwa mwezi shilingi 1,269,000/=

Kipato kati ya shilingi 80,000/= hadi 150,000/= je atamudu vipi maisha kama sio kuwafundinsha kufanya WIZI kwa gharama ya hatari kwake binafsi na mwajiri wake?
* Minimum salary must be pegged at least at TZS 400,000/= and price of the consumable goods controlled to the maximum to avoid inflating the value for personal gain.
 
man umepotosha mbaya. kwanza kwenye kauli zake bi mkubwa. hakuna mahali kasema eti ataunda team ya kukubali au kukataa chanjo.

alichosisitiza ni kuwa tanzania si kisiwa, tuna intergration na mataifa yenye covid.
tume itakayoundwa ni ya kufanya tafiti na kutoa ushauri nn kifanyike ili kupambana na madhara ya covid.

pili hakuna mahali mama kamsema marehemu vibaya. sijasikia kwenye kauli yake akisema hakukubaliana na uongozi wa JPM. Hakuna

muache kumlisha rais maneno yenu.
Karejee vizuri kusikiliza jkwa kutumia 'contents interpretation analysis' halafu rejea hapa. Kasema ataunda timu. Ndio hakuna sehemu aliyotamka JPM kwani mamlaka kabla yake alikuwa nani anapohoji anataka kujiridhisha wakati alikuwepo wakati hayati akisema kitu hicho hicho? Usiegemee upande wowote kutoa maoni, weka rula unyooshe ulichokielewa sio kupinga tu.
 
Mataga posho ilipanda kutoka buku saba hadi 50k.... sasa mtakula kwa jasho
 
Kati ya mazuri mengi ya SSH, ni amejua kuwakera! You are in for long 4 Years, kuleenyai! Mtakunywa maji na karai miaka hii!
 
Mtasema mengi sana,
Dira na mipango yote ya maendeleo huwa anayo Rais kama mali yake?
Mbona uzi huu dhahir una hasad, ni wa kishetani sana.
Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya JMT,mleta uzi ulitakaje ?
Una roho mbaya sana, unahitaji toba.
Una chuki binafsi, hufai kabisa.

Nyinyi ndio wavunja nchi, mescenaries,mna tabia za kimalaya malaya, mnahongwa.
 
Tukisema huyu Mama hajielewi wala haelewi hii nchi inataka nini kwa sasa,kuna watu wanakuja na hadithi za Sukuma Gang Mara MATAGA!!
Mwacheni Madam afanye Kazi. Pole yenu mliozibiwa mianya ya Kujimwambafai. Watu tuko happy tunamuelewa. Amelaaniwa amtegemeaye Mwanadamu kuwa Kinga Yake Kwa Sababu Mwanadamu hadumu Duniani.
 
Msiwe wanafiki nyie kwa mnavyo muona huyo mungu mtu wenu alikuwa anashaurikaa?na hii ni kazi ya lile kundi tunalo ambiwa limepewa kazi maalumu kuhakikisha kila jambo la mama wanaliponda ili tu kufanya aonekane hafai.

Maana mmekazana kumlaumu mama mnasahau hata yeye magufuli kabla ya kuwa rais alikuwa waziri ndan ya serikali ya kikwete lakini alipo pata madaraka akajifanya yeye ndiye rais bora kuliko marais wote na aliwananga sana wenzie tena kwa maneno ya kejeli bora hata mama ana staha ya maneno na mlikuwa mkimshangilia sana wakati yeye katoka huko huko tena miaka mingi tu akiwa waziri.

JPM alinadi ilani tofauti na ya watangulizi wake. Ilani ya Samia ni ipi?
 
Back
Top Bottom