Huo ni ukweli ulio bayana.
Ukiangalia na kusikia ya hapa na pale ndani ya muda ambao Rais Samia amechukua madaraka hakika magomvi,dharau na kutuhumiana waziwazi kwenye kada mbalimbali kumetamalaki.
Mfano ni katika Idara mbalimbali za Serikali Viongozi wengi kwa muda mfupi baada ya kifo cha Magufuli waziwazi ama wanatishana kuuana kwa sababu ya maslahi ama wanadharauliana na kuchongeana ili tu mmoja wao aonekane bora dhidi ya mwingine.
Kinachosikitisha hayupo yeyote anayewakemea ama kuwaadhibu.Mamlaka za wagomvi wale zipo kimya jambo ambalo katika Utawala uliopita kamwe wajinga wale wasingevumiliwa.
Kwa muktadha huo naliona mapema sana anguko la Samia.