Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Walivyokuwa wakipokelewa Chato mlikuwa kimyaa
Hizo za chato hazikua ziara rasmi nchini ila za kikazi. Ukisikia rais anafanya ziara nchi fulani..hizo ndio tunata wapokelewe dodoma sio dar au makunduchi.
 
Hii ni kwa mujibu wa wewe.

Rais Mama Samia yupo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Nyinyi mnajifanya wajuaji sana.

Eti Mama hajafanya chochote. Crap!
 
Ule mji mkuu ki uhalisia ka mzigo!! Kila kiongozi sasa anakuwa na makazi mawili na ofisi mbili ambapo ni gharama mno ku-host ofisi mbili za kiongozi mkubwa.
 
Hayo mawe mazito kama Katiba Mpya hatagusa, atapapasa kwenye kumalizia SGR, na Stiglers, aendelee kutuzubaisha na teua tengua zake, safari za hapa na pale, then iwe end of her story.
 
Hii ni kwa mujibu wa wewe.

Rais Mama Samia yupo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Nyinyi mnajifanya wajuaji sana.

Eti Mama hajafanya chochote. Crap!
Kuna watu ili Rais aonekane kafanya lolote ni Lazima Ang'atuke awaachie wao madaraka'

Ndio maana unaona stori kama hizi👇

1- Kuleta katiba mpya yenye matakwa ya wananchi.
2- Kuwepo tume huru ya kusimamia chaguzi zote za mwakwa 2024 na 2025 na mbele.
👆👆

Sasa sisi wananchi wa kawaida tunachotaka ni Ajira, Usalama, Masoko ya mazao, huduma za afya, barabara, maji na haki.

Na mpaka sasa matumaini bado yapo tunayaona.

Yakipotea tutasema.
 
Hizo za chato hazikua ziara rasmi nchini ila za kikazi. Ukisikia rais anafanya ziara nchi fulani..hizo ndio tunata wapokelewe dodoma sio dar au makunduchi.
Kwa hiyo kule chato walikuwa wanaenda kutalii au
 
Anatembelea nyota ya jpm mpaka sasa.ukweli ofisi aliyopewa uwezo wa kui manage una walakini.inshort uwezo Hana.
 
Tuendelee kumkumbusha Rais wetu mpendwa mpaka sasahivi ajafanya chochote chenye multiple effect kwa watanzania.

Tuendelee kumkumbusha ajenda kuu za nchi hii ni

Kutengeneza mifumo imara ya kiutawala
Kuleta katiba mpya yenye matakwa ya wananchi.
Kuwepo tume huru ya kusimamia chaguzi zote za mwakwa 2024 na 2025 na mbele.

Kutengenisha siasa na biashara yaani sector binafsi iwe na nguvu sio kuwa na wafanyabiashara wanasiasa hawa hawatalipa kodi.

Kuwa na elimu maalifa (ujuzi) ( tetchnical education) sio elimu vyeti na kuzalisha watu wasio ajirika hapa tutaondoa tatizo la ajira.

Sera za kibenk kwa vijana ili mabenk yaweze kuwakopesha vijana pesa na watu wafanye biashara sio kukopa mpaka uwe na nyumba au shamba kama ilivyo sasa.

Mawazo ya biashara yapewe mikopo na ziwepo bima za mikopo hiyo.

Mifumo bora ya watanzania masikini kujengewa nyumba na NHC na wao kuzinunua kwa bei ndogo na malipo yawe kidogokidogo.

Sio zijengwe tena zinunuliwe na hao hao wajenzi hapana utengenezwe utaratibu wa kutambua wanaonunua ni masikini au ni matajiri?

Mama Fanya mambo ambayo yanaweza kuleta multiple effect kwa wananchi wote sio siasa za majukwaani au mambo ya kimbizana na wakina Sabaya na wengine.

Ni ushauri wangu tu safari bado ndefu na muda ni mchache tengeneza mifumo wa kisheria kikatiba hata aje mwehu kiasi gani atapita mle mle ndani ya katiba.
Kazi ipo, kuongoza hii nchi Ni Tabu, yaani mtu ana siku 90 tu unataka amalize yote??? Budget vipi umeipitia mkuu, una maoni gani juu ya budget ya mwaka 21/22
 
Acha majungu fake.Mama kwa muda mfupi ameleta:
1.kuunganishiwa umeme 27,000.
2.Sasa wananchi tuko huru na tunapumua.
3.Bia bei atashuka
4.Boda faini 10,000
5.Amewaondoa viongozi wahahalifu akgna Sabaya,Chalamila.
6.Ameshusha PAYE
7.AMEWARUHUSU WATUMISHIKWENDA NJE YA NCHI.
Hongera sana mama yetu
 
Pole kwa BAN Mkuu..
Ana laana za kaka yake Magufuli kwa hiyo hawezi kufanikiwa katika lolote lile.Imagine yupo busy kuongea na wanawake,kuongea na wazee na teuzi!She is hopeless president.
 
Kwa akili ya kawaida utajengaje ikulu Dodoma Kama siyo ukichaa,au alikuwa anamjengea Ndugai .Wizara zipo Dar ,balozi zote zipo Dar ,uwanja wa ndege kimataifa upo Dar ,Bandari ipo Dar halafu unahamisha Ikulu .Jamaa alikuwa na akili za ajabu
 
Acha majungu fake.Mama kwa muda mfupi ameleta:
1.kuunganishiwa umeme 27,000.
2.Sasa wananchi tuko huru na tunapumua.
3.Bia bei atashuka
4.Boda faini 10,000
5.Amewaondoa viongozi wahahalifu akgna Sabaya,Chalamila.
6.Ameshusha PAYE
7.AMEWARUHUSU WATUMISHIKWENDA NJE YA NCHI.
Hongera sana mama yetu
Mfano mi leo nimetoka Tanesco , niliomba umeme mwaka Jana, nikawa sipo, leo nimeenda baada ya 321000 ,Now Ntalipia 27000/= ,

Hapa nataka kila mpangaji wangu Sasa awe na Luku yake...
Halafu mtu aniambie habari za dikteta mwendazake kuwa alikuwa mzuri, ntamchapa makofi
 
Back
Top Bottom