Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mtakoma mwaka huu. Si zamu yenu imeshaisha mbona mnafata fata watu. Kaeni kwa kutulia.
Kabisa mkuu,

Mataga na sukuma gang wanakoma!
. Pole pole na Bashiru wanakiona cha moto

Mama yuko vizuriiiii... Mi 10 tena kwake!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
. Mh. Rais Samia Suluhu Hassan hafanyi mambo ili kupanda kisiasa.
Umoja wa Kitanzania ulikufa.
Mshikamano wa Kitanzania ulikufa.
Uhuru wa Kitanzania ulikufa.
Furaha ya Kitanzania ilikufa.
Maendeleo kwa Mtanzania yalikufa.
Haki kwa Mtanzania ilipotea.
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kurudisha hayo yote na mengineyo halafu wewe limbukeni moja unaanza kumpiga mkwara,mtashughulikiwa.
Mmezoea siasa za uongo uongo wa kishetani kama shetani alivyo baba wa uongo,leo mnaambiwa ukweli mnaona kuwa ni siasa.
Pendejo!
Na sasa yote hayo yamerudi mama yuko vizuri
 
Watanzania sijui wanataka kuburuzwa mpaka wapi ,mana kwa wanavyoburuzwa na walivyoburuzwa ni wamebaki chakachaka ukiangalia tu mda huu yaani kila kipo juu

Mfumuko wa bei kila kona ...mafuta ya kula juu , tozo za e mone ndio balaa , mbolea juu juu kabisa , petrol juu juu juu zaidi, mahindi juu kodi za kijinga kibao
 
NCHI YA AJABU SANA HII,WANASHABIKIA MAMBO YA KIJINGA HALAFU YA MSINGI WANAYAPUUZA
 
Tofauti yao ni kuwa JPM aliwatetea sana wanyonge na alipigania masilahi ya nchi. Pia JPM alikuwa anasikiliza kero za wananchi na zilizowaumiza alizibadili, mfano mzuri ni suala la kikokotoo.
Na aliua na kutesa sana wanyonge waliotofautiana naye kiitikadi, lilikuwa jitu dhalimu kupata kutokea katika historia ya nchi yetu.
 

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Kwa sasa anabuni tozo na kukopa tu
 
Hizi kodi alizozitunga samia na watu wake sijui amezitoa wapi?

Ni nchi gani duniani inatoza kodi kwenye miamala ya fedha ama manunuzi ya kielekroniki?

Anayetuma fedha anakatwa, anayepokea anakatwa. Muamala mmoja una VAT, TOZO, service charge, sijui EWERU, REA, kodi ya jengo, uliona wapii?

Nchi hii ina kila rasilimali ambazo zinaweza kutulisha hata miaka mia moja bila kuzalisha chochote!

Mmewafungulia mabeberu wanachota madini kama njugu, wanasomba gases, wanapora wanyama na trophies.... ati ndio mnafungulia uchumi!!

Fedha za bandari zinapigwa, miradi inapigwa, ufisadi wizi kila mahali. Hiyo haitoshi, mama huyu kaamua ageukie kuwanyonya masikini!

Hata ukiweka mia kwenye simu wanaifyeka!!

Sio lazima kila mtu awe Rais

Nchi hii ina watanzania zaidi ya milioni hamsini, wasomi, wajuzi, weledi na wenye maarifa. Waachie hao, wewe pumzika.

Kuwa Rais wa nchi kunahitaji mawazo mapana, utulivu wa akili na nafsi. Not everyone can be president!

Tunahitaji Rais anayejitambua na kutambua nini wananchi wanataka na nini nchi inataka!

Lakini kwa mama huyu, HAPANA.
 
Ukiweka salio wanakata
Ukituma ela wanakata
Ukitoa ela wanakata
Ukibonyeza menu ya mobile service ya kibenki wanakata

Sasa ukinunua luku wanakata
Ukipokea salary wanakata
Ukiomba mkopo benki wanakata
Ukinunua bidhaa wanakata VAT
Yaani kila unachofanya serikali inahakikisha unateseka, yaani nikipiga hesabu kodi ninazolipa per day sio mchezo
 
Back
Top Bottom