Mchungaji amesema kuwa hana neno na wazee, ana shida na vijana. Asema vijana wa nchi hii ni foolish, hawawezi hata kusoma katiba na kudai haki zao, vijana wanahongwa elfu 5, tshirt, nyama na wali, baiskeli, eti ndiyo wakapige kura. Vijana hawa ni foolish. Anasema neno la Mungu linasema vijana wamepewa mishale, lakini vijana wa Tanzania ni mishale butu.
Akaongeza kuwa jamii ili iendelee inahitaji vijana, Taifa ili lipate mabadiliko linahitaji vijana.
Akasema ana machozi rohoni baada ya kushuhudia wanafunzi wamejazwa kwenye SGR wanapelekwa kwenye kampeni za CCM. Akauliza, hivi watoto hawa wakipata ajali, wahusika watawaambia nini wazazi wa watoto hawa? Akasema wanaofanya haya ni foolish.
Anasema, huko Arusha alishuhudia mambo ya aibu kabisa, vijana wanahongwa wali na nyama, akauliza, hivi ukishakula huo wali na nyama, mwisho wake ni nini zaidi ya kuchuchumaa chooni? Nadhani anawasema wale vijana waliohongwa mlo na Makonda.
Maneno yake yanafanana na yale ya Mwalimu Nyerere, aliyosema kuwa ili Taifa kuweza kuwa na mabadiliko kuelekea kwenye maendeleo, ni lazima liwe na vijana jeuri, vijana wanaoweza kuhoji, siyo vijana wakiambiwa lolote na mtawala, jibu lao ni 'ndiyo mzee', vijana wasioweza kuhoja chochote.
Kwa sasa tuna vijana wa hovyo kuliko hata hao aliowasema Mwalimu Nyerere, leo tuna vijana wa aina ya akina Mwashambwa, vijana wanafiki, waongo, vijana machawa, wanaomalizwa akili na book 10.
Hakika wakiinuka wachungaji, maaskofu, mapadre, mashekhe na maimamu kama 20 tu wa kiwango hiki, vijana wanaweza kuotambua nafasi waliyo nayo. Maana kwa hakika maovu mengi na masahibu mengi yanayotokea nchi hii, vijana ndiyo waathirika wakubwa. Ni vijana ndiyo hawana ajira, ndiyo wanaotekwa kwa wingi, ndio hawana kipato, ndiyo waliobakiwa na miaka mingi zaidi ya kuishi kwente mateso yanayosababishwa na CCM, lakini wamelala, wakisubiri wakombolewe na wazee!
Sikiliza mwenyewe: