Aliyekua DC wa Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake leo wamefikishwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya iliyopo Sekei Arusha, ili kujibu tuhuma zinazowakabili, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano.
Itakumbukwa June 04,2021 Sabaya na wenzake walifikishwa Mahakamani hapo ambapo baadaye Tumaini Kweka, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka anayeshughulika na usimamizi wa kesi alisema“uchunguzi katika baadhi ya makosa yanayomkabili Lengai na wenzake umefikia kwenye kiwango ambacho tunasema ni tamati ya kuweza kuwafikisha Mahakamani”.
“Mkurugenzi wa Mashtaka baada ya kujiridhisha kwamba kweli tuhuma zilizokua zinamkabiki Lengai na wenzake kisheria zinatengeneza kosa akaamua leo wafikishwe Mahakamani, kama mlivyoona alikua akituhumiwa kuongoza magenge ya kihalifu, vitendo vya rushwa, kutakatisha fedha haramu ambayo ni matokeo ya vitendo vya rushwa”.
“Vilevile Mkurugenzi alijiridhisha kwamba kuna unyang'anyi wa kutumia silaha, ndio maana amefikishwa Mahakamani leo kwa hayo makosa matano lakini kwa unyang'anyi wa kutumia silaha ni makosa mawili aliyatenda katika wakati mmoja lakini kwa wakati tofautitofauti, na kama tuhuma nyingine zitathibitika basi Mkurugenzi wa Mashtaka ataamua vinginevyo"
My Take: Mahakama na DPP huu ndiyo wa kutuaminisha umahiri wenu. Chapa ilale
======
PICHA: Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake, wakiwasili mahakamani mkoani Arusha kwenye kesi yao, leo Juni 18,2021 Ijumaa
Mbona wanamuwahisha mapema Sana mahakamani kwann asikae kama miaka 6 hivi kama wazee wa escrow au uhamsho kusubiria ushahidi kukamilika ndipo aanze pelekwa mahakamani.Hii sio dabo standard kweli
Kesi inayomkabili Ole Sabaya na walinzi wake imetajwa tena kwenye Mahakama ya Arusha na kuahirishwa hadi July 2 , kwa kile ambacho mwendesha mashitaka amedai upelelezi wake bado haujakamilika .
Sabaya ambaye Suti aliyoivaa leo inaonekana kumpwaya , amerejeshwa rumande ya Kisongo akisubiri kesi itakapotajwa tena .

Hapa ndo kuna swali "Sabaya ambaye Suti aliyoivaa leo inaonekana kumpwaya".Ndugu mleta mada ungesema 'amekonda' na sio "suti Kupwaya". Labda tu walio karibu nae wamshauri hayazoee tu maisha ya Ugali kwa Maharage maana Hakuna namna.
Tunacho taka vyombo vyetu vifanye kazi kwa weledi, kamwe visikubali kuendeshwa ama kusukumwa na maneno ya vijiweni, majungu, fitina na chuki za kisiasa.
Sheria zizingatiwe, tusiongozwe na hisia au dhana.
Kesi inayomkabili Ole Sabaya na walinzi wake imetajwa tena kwenye Mahakama ya Arusha na kuahirishwa hadi July 2 , kwa kile ambacho mwendesha mashitaka amedai upelelezi wake bado haujakamilika .
Sabaya ambaye Suti aliyoivaa leo inaonekana kumpwaya , amerejeshwa rumande ya Kisongo akisubiri kesi itakapotajwa tena .
daa yaani hapo nakuona ulivyokuwa unaandika huku sura yako imechanua tabasamu la nguvu kama vile unaandika habari taaamu ya kufurahisha all in all katesa watu acha ale alichokuwa anakipanda awasaidie maumivu kina mdude nyagali
Mbona wanamuwahisha mapema Sana mahakamani kwann asikae kama miaka 6 hivi kama wazee wa escrow au uhamsho kusubiria ushahidi kukamilika ndipo aanze pelekwa mahakamani.