Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Ukishamjua Mbwa wa Jirani si tu ni Mpumbavu bali pia ni Mwendawazimu na hatari kwa Uhai wako kwanini tu usimuepuke kwa ama Kuachana nae au kukaa nae mbali ili asije akakujeruhi vibaya pengine hata ukafikia kupoteza Maisha yako?

Vitu vingine wala havihitaji Akili Kubwa.
Katika historia, Hakuna dikteta aliyefanikiwa kunyamazisha watu wote.
Na kwa viongozi wa dini ndio haiwezekani kabisaaaa.
 
Kumbe huyu aanejiita askofu ni mpinzni wa kisiasa na alikuwa pia mshauri wa Lisu wakati wa kampeni?

Alafu mnalaumu kwanini mmeshindwa uchaguzi?

Imagine Mwamakula ndio mshauri wa mgombea urais katika harakati za kwenda ikulu katika nchi kama tz!

Yani huko chadema hakuna watu wenye akili kabisa?
Ushauri rahisi tu. Tuma e mail kwa support@jamiiforums.com, wape jina lako halisi, waambie litumike kama verified user, utalamba uteuzi fastaa
 
Lisu ni heri angeongea hayo akiwa bongo aone fire⚰️
 
Mkuu Watanzania nawajua, ni waoga kupitiliza. Kile kizazi cha akina Samwel Sitta hakipo, fikiria mtu anahamasisha mgomo hadi kufikia Mwl Nyerere kutoka Ikulu kwenda Chuo Kikuu na Kumchapa viboko.

Hakuna Mtu alijua kuwahamasisha Watanzania kama Tundu Lissu, lakini uliona walivyom disapoint.

Fikiria kuna kundi la vijana zaidi ya laki 5 wame graduate na hawana ajira, lakini hata kusema waandame kuhamasisha utatuzi wa kilio chao.

Imagine watumishi ambao hawajaongezewa mishahara tangu alipowaongezea JK 2014 lakini hakuna anayetoka kulalamika.

Imagine wanufaika wa bodi ya mikopo walioongezewa riba kutoka 8% ya JK hadi 15% za Magufuli na wamekaa kimya

Imagine wakulima wa Korosho kule kusini walipokopwa Korosho zao na Serikali 2018 lakini hakuna aliyethubutu kupanua kinywa chake kulalamika

Fikiria kikokotoo alichosema kitaanza kutumika 2023, kuna aliyesema chochote

Watanzania wangekuwa wadudu tungesema wanadamu ya Kunguni, unamjua kunguni Mkuu 😀😀

Kwahiyo wakati naandika vile, nawajua Watanzania, ndivyo tulivyo.

Imagine bei za vifaa vya Ujenzi ilivyopanda hadi kujenga tumepunguza alafu hakuna anayelalamika, ndiyo kwanza wanasema tumewaachia kujenga Matajiri.

Ingekuwa Nchi nyingine kitendo cha Tundu Lissu kupigwa zile Risasi Serikali yote ingekuwa imeondolewa madarakani lakini wapi bwana, ndiyo kwanza imeanza kampeni ya kuomba aongezewe miaka mingine 10, ujinga tupu
Well said, ngoja shida zitutafune mpaka tupate akili
 
Nacho f

Nachofahamu Askofu Mwamakulah alisoma Azania High school. Na alikuwa mchapuo wa PCM.
Pia alikuwa ni Headboy. Inasemekana alikuwa na uwezo mkubwa darasani. Na alikuwa kiongozi mzuri alie heshimika kwa wanafunzi, walimu na hata Mkuu wa shule alimpenda sana. Wakati huo Mkuu wa shule alikuwa Bwana Kwayu.
Mwamakulah alifaulu vizuri kwa kiwango cha juu katika mtihani wa Taifa kidato cha Sita. Nasikia aliendelea na masomo ya chuo kikuu.
Mambosasa anatafuta kuwa IGP japo ana changamoto ya umri
 
View attachment 1703071


View attachment 1703070



View attachment 1703379


====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.


LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:


Sheria ipi imevunjwa kutoka kipengele kipi cha katiba ewe Mataga elimisha jamii usitutishe!
 
Hivi kudai katiba mpya ni kosa?
Kuidai tunamkosea nani?
Si kwa ajili ya ustawi wa tz yote?
Unajua inatufanya tuamini kuwa wanaotutawala sio binadamu kabisa!
 
Hii move ilikuwa expected. Polisi wetu wapo predictable na Mwamakula nadhani alikuwa akilitegemea hili
 
Well said, ngoja shida zitutafune mpaka tupate akili
Kabisa Mkuu

Binafsi naona kuna kaupendeleo huwa kana fanyika kuhusu maandamano, wakati wa JK watu walikuwa wanaandamana kila uchao.

Utawala huu, naona wamepumzika licha ya kero na malalamiko kuwa mengi.

Ingekuwa enzi za JK kuhusu kufanya kazi mazingira ya hatarishi kwa madaktari wakati huu wa Covid -19 wangeandamana kushinikiza nyongeza ya mshahara, lakini awamu hii hadi On call allowance haipo 😅😅

Kusini watu waliambiwa watapigiwa mashangazi wakaufyata 😀😀😀🙌
 
Kabisa Mkuu

Binafsi naona kuna kaupendeleo huwa kana fanyika kuhusu maandamano, wakati wa JK watu walikuwa wanaandamana kila uchao.

Utawala huu, naona wamepumzika licha ya kero na malalamiko kuwa mengi.

Ingekuwa enzi za JK kuhusu kufanya kazi mazingira ya hatarishi kwa madaktari wakati huu wa Covid -19 wangeandamana kushinikiza nyongeza ya mshahara, lakini awamu hii hadi On call allowance haipo [emoji28][emoji28]

Kusini watu waliambiwa watapigiwa mashangazi wakaufyata [emoji3][emoji3][emoji3][emoji119]
Kila awamu ina kauli mbiu yake

Awamu ya hapa kazi tu kuchanganya na maandamano ni maajabu
 
View attachment 1703425
Askofu Emmaus Mwamakula, mshauri wangu wakati wa Uchaguzi Mkuu 2020, amekamatwa na polisi wa Dar. Askofu alipanga kutembea nchi nzima kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Badala ya kupambana na COVID-19 inayotishia maisha ya wananchi, Dikteta Uchwara anapambana na wapinzani wa kisiasa. https://t.co/yhkHk6ZR3d
Mheshimiwa siasa za hapa Tz zimekushinda, we kula bata huko uliko, acha kudanganya wazalendo, ile biashara ya kutufanya nyumbu tumeishitukia
 
Haka kajamaa bana, kanajaribu kujitutumua ili kaonekane bado kamo wakati kaliufyata kakasepa kwenda kula bata na shoga yake bob huko ubeberuni!
Kasivyo na hekima sasa kamemwanika askofu kuwa ni mpinzani wa kisiasa!
Kiazi kichafu wewe hivyo.
 
Back
Top Bottom