Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Kwanini huyo Askofu asipambane na Covid -19 bali ana hamasisha mikusanyiko kupambana na Katiba??

Lisu hakuliona hilo kwakua mwamba ngoma huvutia kwake!
 
k
View attachment 1703071

View attachment 1703070

View attachment 1703379

====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

kwanza askofu hawajawahi ita watu kufanya maandamano yeye alisema ni matembezi ya hiari kwa lengo la kutoa hamasa.Pia maandamano ambayo hayajafanyika yanakuwaje ni kinyume na sheria wakati hujui kama wangefuata utaratibu au la.=MENS REA without ACTUS LEUS/Attempt no offence committed(Nia tu bila kitendo au jaribio haliwezi kuwa kosa kwa mujibu wa sheria.
 
View attachment 1703425
Askofu Emmaus Mwamakula, mshauri wangu wakati wa Uchaguzi Mkuu 2020, amekamatwa na polisi wa Dar. Askofu alipanga kutembea nchi nzima kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Badala ya kupambana na COVID-19 inayotishia maisha ya wananchi, Dikteta Uchwara anapambana na wapinzani wa kisiasa. https://t.co/yhkHk6ZR3d
Kitendo cha kusema ni mshauri wako anamuweka kuwa watanzania tunajua ameegamia chama fulani siyo Watanzania wote
 
Kwa sheikh watachemka maana yule selo Kwake ni kama nyumbani. Pole baba askofu piga mistari ya ufunuo aote busha yule jamaa wa chato.
huo upako hana.

mshauri akaendelee kupiga siasa na huko sero pia.
 
Kila awamu ina kauli mbiu yake

Awamu ya hapa kazi tu kuchanganya na maandamano ni maajabu
Ina maana kero zimeshughulikiwa na kuisha kwenye jamii??

Au watu wanaogopa kupigiwa mashangazi zao ??😀🙌
 
Askofu fake tu! Ameshindwa kukusanya kondoo wa imani anahangaikia katiba. Injili ameeneza kwa nani? Kama ni njia ya kupata waumini ndo matokeo yake hayo. Sero ya polisi amuulize Gwajima na presha iliyompata.
 
View attachment 1703071

View attachment 1703070

View attachment 1703379

====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

Habari za uhakika ni kuwa Hawa wote wameshapata chanjo, wanatuacha sisi tufe.
 
Nikifikiriacho mimi mambosasa hutumika kuwahonga au kuwafanya mateso makali viongozi wa maandamanokwa lengo la kudhohofisha mpango mzima.

Mbinu hii imeonekana kufanikiwa. Wanaokamatwa wakitoka huwa kimya na kuridhika. Je uhongwa mabunda ya fedha au huhofu mateso?

Maandamano wasiyo na tarehe yatokanayo na tukio la udhalimu lililofanywa na Mtumishi wa serikali likaibua hosia kwa watu ndilo pekee litafanya watu waandamane.

Au viongozi wa maandamano wakatae kukamatwa kabla ya maandamano kwa kujificha au kulindwa na wafuasi wao mpaka siku ya maandamano. Vinginevyo itakuwa kiini macho
 
Ewe Kilaza lini utaacha upumbavu? Uzuri wa sheria ni kuwa kila sheria inafahamika kwa namba yake katika mwaka ilipotungwa. Unazungumzia sheria zipi? Kudai katiba mpya ya watu au kudai tume huru ya uchaguzi ni kutokufuata sheria?...
Naamini huyo kilaza sababu ya ukilaza wake, hatokuelewa katu asilani
 
Atawachungia wapi hao kondoo na kanisa lilimfukuza?
Hana kanisa, kiufupi ni mkorofi kiasili, huwa hawezi kutulia
Hana waumini anazunguka tu na manguo ya kiaskofu aliyojishonea mwenyewe kwa fundi cherehani ndio Maana Mambosasa kasema ANAYEJIITA ASkOFU!!!
 
Huyo siyo askofu wala mchungaji wa kanisa la moravian, huyo ni muhuni tu.

Chanzo gazeti la Habari leo la leo.

Apuuzwe, km anataka siasa aingie tu ktk siasa.
 
Sikujua kama matembezi ya hiari ni kosa la kisheria.Kama ni kosa,chombo gani kinapaswa kusaidia kupatakatiba mpya?
UMemsikiliza vizuri mambosasa? Kaongelea matembezi kwenye barabara za umma na kuleta taaharuki kwa wengine

Ukitaka usiandamane barabara za umma hayo matembezi yako kayafanye porini kusiko na watu na kusiko leta usumbufu kwa wengine wenye shughuli zao

Nendeni mkaendeshe matembezi yenu porini huko
 
Kujiamini, kuwa na watu wasio jiamini, kuwa na watu wasio thamini wananchi kisa kumsaidia mtu awe salama au kufanya kazi kwa mihemko ni mbaya sana.

Kila mtu ana haki yake kutoka kwa Mungu na kutoka kwenye vitabu vya sheria vilivyotungwa na mamlaka zilizowekwa.

Anajitokeza mtu anasema huwa hatufanyii kazi maneno ya kwenye mtandao kisa yeye hana wa kumuwajibisha cha ajabu jana mtu kakamtwa kwa maneno ya kwenye mtandao.

Huyu ana wadhifa aliopewa na Mungu au anajipeleka tu hadi siku yake ya kustaafu ifike ili atulie. Tusijidanganye hata baada ya miaka mtu akishastaafu ataitwa aje ajibu mashtaka yake aliyo yatenda akiwa kazini.

Tufanye kazi ili kumpendeza Mungu na sio kujipendekeza. USHAURI WA BURE.
 
Watakuja kulia na kusaga meno miaka ijayo we waache wadengue tu
Nalog off
 
Hivi kwenye katiba yetu, maandamano ni DHAMBI!? Well, labda nimetumia lugha ya kidini; kwenye sheria zetu Maandamano ni hatia?
 
Back
Top Bottom