Uchaguzi 2020 Askofu Mwingira: Lissu ni mshindi, hajajenga flyover wala reli. Watu wanamfuata

Naona wafia madaraja na maflyover viti vya mbele kwa nabii wamepooza kbs hawamshangilii nabii!
 
Ndege haziongelewi tena wananchi wanadai haki, uhuru na maendeleo.
Wananchi hawahawa wanaosimama barabarani wakimshangilia Jiwe anavyocheza wimbo wa Zuchu wa ccm? Au wale wanaojazana kwenye mikutano ya ccm na huku wakiburudishwa na wasanii?
 
Mwingira Mungu alimuita kuhubiri habari za Yesu sio za Tundu Lisu na risasi zake kapotezea muda waumini walioenda kusikiliza habari za Yesu halafu wakaishia kusikiliza habari za Tundu Lisu

Mwingira 2015 alikuwa UKAWA na mgombea wake CCM tulimshinda ajiandae na huyu wake Lisu tutamshinda
 
Umati anaopata Lissu ni wale wanaomshangaa na sio kumpa kura.
 
Wewe tumekupuuza. Taarifa ya jana imetufumbua macho.

Wewe ni muuaji. Kwa maandishi yako, ndiye uliyeomba upewe kazi ya kumwua Tundu Lisu. Mtu mwenye roho ya shetani kiasi hicho, huna cha maana unachobeba moyoni mwako zaidi ya laana juu yako na kizazi chako.

Mungu wa enzi akutendee kwa kadiri ya ubaya wa moyo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingira kwa wakongwe wa jf wanajua zile threads zilizokua zikianzishwa miaka ya nyuma namna alivyozaa na wanawake za watu kibao ila sababu yupo upande wa pili hayo madhambi yake yote yenye ushahidi yametakaswa na hayaonekani

Ila mtu fudenge yeye anachanganya siasa na dini, nasikia kuna maaskofu walikua wanahutubia majukwaa ya siasa juzi Bukoba, watanzania unafiki utatuua
 
Akaunti zake na za kanisa ziangaliwe yaweza kuwa katakatisha pesa za Lisu toka nje at a fee ndio anapiga hizo kelele za kupamba baada ya mzigo wa pesa kuingia
 
Kura yangu ni kwa Tundu Lisu. Siwezi kuishi maisha ya kumsikiliza mtu mmoja.
Anaye jijali yeye tu. Ashibe yeye tu na anaowachagua.
Hashim Rungwe simpi kura yangu. Bora nimpigie Mrema.
Kwanini usiache kupiga kura kabisa kama mie?sijawahi kujuta.

Maana wewe unaonekana hauendi kupiga kura ili kumpata kiongozi unayeona ndiyo sahihi bali unaenda kupiga kura kutokana na hasira ulizonazo kwa Magufuli.

Ukienda kupiga kura halafu matokeo unaona usiyempenda ndio kashinda hapo lazima stress zizidi.
 
Kwani 2015 matokeo ya kura yalikuwaje? Na huyu sauli alinyenyanganya nafasi ya mwingine umeona ameishia wapi? Acha kushupaza shingo
 
Mi sijamtaja huyo unayemtaja, mi nimewataja watu wawili Tu.
Tafadhari usinizurie kesi.
 
Na Kuna Maaskofu lukuki nao wanaunga mkono juhudi....na ndio hukusanywa kuombea amani na Maendeleo ya Awamu ya Tano....hapa tumeshavurugana na hili donda halitapona....Mimi siwezi fuata Kanisa ambalo lilikaa kimya WAKATI WATAWALA WAKIPIGA MARUFUKU KUMUOMBEA TUNDU LISU AKIWA KITANDA CHA MAUTI...HILO KWANGU NI KANISA LA MASHETANI.....!
 
Maneno yenye ukweli mzito kutoka kwa mtumishi wa Mungu. Tundu Antiphas Lissu ni muujiza kweli unaotembea.

Niliwai sema na nasema tena. Mungu hawezi kukuponya kwenye risasi 16 kirahisi tu bila kuwa na sababu kubwa na wewe!!

Mungu anaenda kuandika historia kuu Tanzania mwaka huu. Tundu Antiphas Lissu anaenda kumuangusha Magufuli vibaya sana na kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020- 2025
 
Mzee anahaki ya kutumia mfano wowote katika kufundisha watu Wake.

Ila Mamlaka iliyopo sasa imekubalika na ilishapata kibali Mbele za Mungu Rais Magufuli anakwenda kushinda term nyingine,

Tunakwenda kuiona Tanzania ikiimarika zaidi ya sasa.
Mkuu na wewe unaishi Tanzania hii hii inayopakana na kenya,uganda,burundi,DRC,zambia,malawi na msumbiji au unaishi Tanzania nyingine?
 
Nimekugongea "like". Yahitaji kujitoa ufahamu ili umsikilize nabii mzinzi
 
Sanduku la kura lina maajabu! watu watakuimbia, kukubeba na watasukuma hadi gari lako ila kura watapiga kwa chama chao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…