Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Maneno mazito sana. Hayana Afya kwa Taifa.

Pole sana Baba Askofu
 
Basi nadhani na Nabii Mwingira ana kitu hatukijui juu yake. Maana hata JK hawakuwa wanaelewana. Alipokuja Dkt Magufuli kipindi cha kampeni alimdhihaki sana hicho kipindi na aliwatabiria waumini wake kusema Dkt Magufuli hatoshinda uchaguzi ila Dkt Magufuli akashinda. Nadhani Nabii atakuwa na kitu na serikali ambacho si chema anakijua ila wananchi hatujui. Pia serikali imuue kwa lipi??? Nadhani Nabii atakuwa na ugomvi wa makanisa yao yaani wao kwa wao ma nabii na maaskofu wanatafutana ili kuzimana kasi ya waumini. Dkt Magufuli hakuwa mtu wa tabia ya kuua watu.
 
Lissu alikoswa! Una jingine?
 
Hao wote waliolalamika awali na hata sasa bado hauwaamini tu?Watunge woootee uongo kuhusu utawala mmoja uliopita kwa faida gani?
Na kama kila anayelalamika ni hasira juu ya jambo fulani, basi utawala ulijaa tabia ya kutengeneza hasira kwa wananchi wake.. Haiwezekani kila anayelalamika aonekane ana hasira ya kitu fulani
 
Utetezi huo ulimtetea haikuwa hoja ya kuwaonea wengine.Kwamba huyu anapigwa bila sababu kwa sababu kuna sehemu watu ni wahalifu?Hakukuwa na haki wala ukweli.
 
Huyo alikuwa na roho mbaya na muuaji mkubwa hakuna mfano wake hapa nchini!
 
Huyo alikuwa na roho mbaya na muuaji mkubwa hakuna mfano wake hapa nchini!
Hapana mkuu acheni hizo mambo. Mwingira alikuwa na chuki binasafi kwa sababu mambo ya uchaga na mke ni mchaga na lowasa.
 
Hasafishiki huyo hata uwe na kichwa cha mwendawazimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…