Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Wakristo waache unafiki, msamaha kwani alikosa? Alipewa likizo na kuripoti makato makuu Sasa wapi hapo inaonesha alikosea, kama walikoseana sirini iweje Leo msamaha uwekwe hadharani?
Sasa unafiki wa wakristo wewe unakuumiza nini? Maana kama na wewe ni mkristo basi ni mnafiki mwenzao, lakini kama wewe ni muislamu, acha wanafiki wanafikiane wenyewe..!! Maana hakuna mahala unafiki wa wakristo unawaharibu waislamu kwenye hili..!!
 
Amefanya jambo zuri kuomba msamaha hadharani na kusamehewa,aendelee na kazi ya Mungu sasa popote pale atakapopangiwa.
ANGALIA ELIONA ALIVYO ONGEA KI-MASTA 1. Nashukuru kwa maongezi, maombi na nasaha zako. Tuliongea sana kwenye simu.

2. Nilikuwa nafundisha vijana kuhusu life discipline na personal discipline. Watu wengine huko wakatengeneza clip wakaitafsiri kivingine.

3. Hii likizo kwangu mimi siyo adhabu bali ni wakati mzuri wa kutafakari na kuutafuta uso Mungu.

4. Ahsante kwa kumtuma askofu mstaafu kuja kuongea na mimi.

5. Nakuomba wewe binafsi msamaha!
Yaani Mchungaji Kimaro hajaomba msamaha kwa Mungu kwa sababu anajua hajamkosea Mungu. Kaomba kwa binadamu : Likizo haijaisha so am,esamehewa akiwa likizo, MALASUSA: "umesamehewa, endelea kutafakari" -hiyo kauli tata sana kwa askofu, angata na kupuliza: Lengo ni kuona vyenye upepo unapoelekea:
 
Hilo la kutoomba msamaha kwa Mungu anajua yeye na Mungu wake,lakini pia kumbuka yupo kwenye nyumba ya Malezi ya Kichungaji kwahio suala la Kumuomba Mungu kama ni kulifanya atakuwa amelifanya au analifanya huko maana anasema amefunga na anaendelea na maombi.

Hapa mshindi ni Kristo dhidi ya Roho ya mafarakano,Kama yeye ndio ameomba msamaha kabla ya likizo kwisha na tena hadharani ilikuwa busara pia kusamehewa hadharani maana asingesamehewa hapohapo nayo isingekuwa busara.
 
Mbona Kimaro ndiyo kaomba radhi tena hadharani,japo hajasema alikosa nini.......sasa Malasusa kashindwaje, wakati Kimaro yeye mwenyewe alishika Mic na kuongea?
 
Yaaan wanashindwa kuchanana laivu hapo hio ndo unafiki
 
Mbona Kimaro ndiyo kaomba radhi tena hadharani,japo hajasema alikosa nini.......sasa Malasusa kashindwaje, wakati Kimaro yeye mwenyewe alishika Mic na kuongea?
Chukua maneno yangu, acha zile PR
 
Tatizo la TV za mitandaoni wanapenda clip pale wanapopataka tu.

Ukifatilia video nzima, mchungaji Kimaro kaomba msamaha na kaeleza hadi sababu iliyosababisha awekwe kando.
 
Kuna wakati nasikiliza mahubiri ya Kimaro, hakika anajua kugusa maisha ya watu. Hana unafiki, ni msema kweli.
 

Punguza ushabiki Kwenye mambo usiyoyajua.
 
Hayo ya chumbani baki nayo mwenyewe mkuu,ila mwanaume na ndevu kuomba radhi hadharani siyo udhaifu bali amekubali kuna mambo alikosea
Hiyo ni technical retreat....he just lost a battle, Malasusa should prepare for a full scale war
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…