ATCL, Reli ya Kati, TAZARA na SGR tuwape wanaoweza kuendesha kwa ufanisi mapema kabla ya kuumizwa

Wewe kwenu wapi?
 
Tumejifunza, tumejisahihisha, tumejirekebisha, tumejipanga, tumejiandaa kwa viwango vya kimataifa, kuiendesha SGR, wenyewe kisasa zaidi, kwa umahiri weledi sana, na matarajio ni kuiendesha kwa faida ambayo haijawahi kutokea humu nchini 🐒

ustahimilivu na Subra ni mambo muhimu sana kuelekea kuanza rasmi operations za SGR🐒
 
Naunga mkono hoja. Pia mashirika yote ya umma yanayojiendesha kwa hasara serikali iingie ubia na wawekezaji binafsi kwajili ya kuyaendesha. Mbona TBL au NMB Bank wanapata faida kila mwaka tunashindwa kuuona huo mfano?
 
Sasa kama tutaruhusu kuongozwa na huyo kichaa atakaekuja nadhani sisi wananchi tutakaomchagua ndio tutakua vichaa zaidi.
 
Nacheka Sana. Tanzania haina watu wenye uwezo kusimamia mashirika ya umma yakaleta faida. Maana yake hata hapa jf hakuna watu wenye uwezo huo. Makampuni ya ujenzi ya china kila siku tunaona kwenye miradi wanawezaje?
 
Kwa hili nakuunga mkono , Watanzania ni wezi tu Bora waendeshe wageni labda Akili zitatukaaa sawa
 
muda si mrefu behewa zitachakaa na service kushindwa kufanyika sababu ya wizi na ufisadi kwenye huo mradi. Mda utaongea tu.
 
Kwa hili nakuunga mkono , Watanzania ni wezi tu Bora waendeshe wageni labda Akili zitatukaaa sawa
Shida ya hao wageni baada ya mwaka tu watakuwa wame adopt tabia za kishenzi. Tunarudi kule kule tu maana viongozi wataanza kuwatishia tishia na kuanza kuomba omba rushwa.

REF: Ujio wa halotel ulivyokuwa na hivi leo hali ikoje.
 
Waambie serikali mashirika yapate watendaji, bodi na menejiment zake kupitia usaili wa wazi, watu waombe hizo kazi na wapimwe kwa vigezo vinavyopimika..hizi sio zama za kuteua mtu kumpa fursa ajikimu! Hicho ulichosema wewe ni limbukeni ndio anafikiri ujinga wa aina hiyo wa kuwapa watu Mali yako wakutengenezee wewe umekunja nne barazani..zama hizo zilishapita kitambo.
 


Basi hata serikali nayo tuwape watu wengine maana nayo pia ipo chini ya Watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…