ATM ya kwanza ya maziwa yazinduliwa Moshi Mjini

Ni jambo zuri;
Japo usafi, ulinzi wa mashine hizo na ubora uzingatiwe la sivyo tutapata msiba wa mtaa mzima kama si mkoa wote.
Automatic dispenser ya kimiminika siyo kama ATM ya Pesa a.k.a makaratasi yenye sanamu za viongozi.
 
Wewe ndo hujaendelea. Mambo ya glasi ya maji safi moshi hakuna anaejua shida ya maji maana hata mamlaka ya maji ina uwezo wa zaidi ya 100% kusambaza maji. Maji safi yanapatikana hadi kwenye mabomba ya vyoo vya stand ukiingia na glasi unakunywa.
Let us go to the next level.
 
Usalama na ubora wa maziwa ukoje?
Kama maziwa yamekaa wiki utajuaje
Hata maziwa yakikaa mwaka, umeshaambiwa yamesindikwa (processed) hayaaribiki overnight.
Ni kama unavyonunua tanga fresh dukani inakuwa ina expire date ya miezi kadhaa.
 
Marahaba mkolomije
 
Automatic inajua
Hiyo mashine itawezaje kutofautisha shilingi 50, 100, 200, na 500 za sarafu?
Na je inaweza kutoa chenji kama nimetoa elfu kumi halafu nikanyonya maziwa ya sh 150?
 
Kunywa tu maziwa mkuu yakiharibika yatakuwa yanaingia automatic upande wa mtindi na biashara inaendelea....
 
Yaani mmetupita hata sisi wenye akili nyingi na pesa
Haiwezekani mji wetu wa Bukoba ukose hiiyo kitu muweke moshi
Ngoja sisi tuweke ATM ya samaki na asali
 
Ngoja ianzishwe huko kwenu Dar muiite dispenser. Sisi ndo tushahamua hamuwezi kutupangia kila kitu

Ni maamuzi yako Mkuu, huwezi kuingiliwa. Unaruhusiwa hata kumuita mbwa wenu kuwa ni mbuzi. Ruksa!
 
kwanini yaharibike?
 
Wangetutangazia na bei, ili tupime wenyewe. Tuende atm au tuendelee kupimiana kwa vibobo mtaani kama kawaida
 
Kwanza makosa yanaanzia kwenye neno ATM.
 
Aliyekwambia Moshi wana tatizo la maji safi na salama ni nani??!...maendeleo huwa sio sawa sehemu zote na ndio maana we una simu ya smartphone ila kuna watu wanalala nje. Huwezi sema tusiwe na hiyo smartphone mpaka watu wote wajengewe Nyumba. Kila mtu na kila sehemu ina mahitaji tofauti tofauti
 
Duh kasheshe! Nini mrefu cha ATM? Wenye lugha yao kwenye nchi zao wanaziita vending machines. Kuna za coca, Pepsi na snacks kama chips nyembamba na chocolate.

Utajua mwenyewee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…