Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Oneni chizi huyu, unajuwa sheria ya manunuzi?
 

Attachments

  • Screenshot_20230901-104441.jpg
    24.7 KB · Views: 1
Bunge limeshakataa kupokea muswada wa mabadiliko ya sheria ya Maliasili na Ile ya mikataba ya Maliasili, ambayo ililenga kuaccommodate IGA,
 
Baada ya kuacha kupeleka ule mswada bungeni....
 
Bunge limeshakataa kupokea muswada wa mabadiliko ya sheria ya Maliasili na Ile ya mikataba ya Maliasili, ambayo ililenga kuaccommodate IGA,
Tulipofikia ilikuwa ni kutengeneza tatizo ambalo halina sababu. Kwa mara ya kwanza nimeanza kufikiria kutakuwa na mabadiliko ya kweli
 
Tulipofikia ilikuwa ni kutengeneza tatizo ambalo halina sababu. Kwa mara ya kwanza nimeanza kufikiria kutakuwa na mabadiliko ya kweli
Inaweza ikawa dhana tu na isiwe halisi, wanasiasa wakiona mkate ni rahisi kubadilika na hivyo kutoaminika
 
Wewe ndio mjinga kupitiliza msingi wa appendix unatokana na malengo makuu, appendix nisehemu mahususi! Main objective ndio inasubmit bandari zote za bahari, na maziwa! Punguza UJInga na ujuha!
Endelea tu kubwabwaja. Uwekezaji wa DP Lworld kwa mujibu wa Appendix ni sehemu ya Terminal 1.
 
Inaweza ikawa dhana tu na isiwe halisi, wanasiasa wakiona mkate ni rahisi kubadilika na hivyo kutoaminika
Sio sasa hivi. Hata haya mabadiliko yamekuwa ya lazima. Lazima kuweka watu ambao wataweza kusawazisha hizi kelele za miezi kadhaa.
 
Andiko zuri Mkuu, umesahau kuweka namba ya simu hapo mwisho.
 
Sio kila kitu kina ulazima wa kununuliwa kwa sheria ya manunuzi. na hili lilishaelezewa kwa kina na wanasheria wa wizara mbele ya wahariri na mbele ya maaskofu.
Tuambie ni Sheria ipi inayosema sio lazima, na utaje kwamba uwekezaji wa sehemu mahususi kama Bandari au sehemu yoyote kwamba imetajwa humo kufanyika pasina kufuata sheria ya manunuzi!

Lakini ukumbuke kwamba Waziri Mbarawa aliuambia umma kwamba walishandinisha kampuni Saba na DP akaibuka mshindi

PM akauambia umma kwamba waliemda kumtafuta DP wenyewe wakati wa maonesho ya biashara Dubai na wakaona utendaji kazi wake wakamchagua!

Nani mkweli kati ya hao wakati hata mama alidanganywa kwamba DP Wan campaign ya kuchukua bandari ya Mombasa while tunajua 2022 walimkataa,
 
Basi msimamo wa Kanisa ndio msimamo wa Waumini

Kanisa Moja Takatifu la Mitume 😀
Watanzajia siyo wakatoliki, nchi yetu haina dini, huo waraka wao wawaandikie waumini wao waache ulevi, uzinzi na ushirikina. Waachanane na mambo yahusuyo uendeshaji wa nchi, ya kwao yenyewe yamewashinda, hilo ni baraza la kiinjili
 
Ndg yangu hapo kuna wapiga dili na wengine ni manyumbu tu yanafuata yasiyokijua kwasababu ya ujinga wao.
 
Brother hatubwabwaji tunaestablish real facts zilizoko katika maandishi ya IGA.
Sasa kwa mujibu wa Appendix 1 uwekezaji wa DP World ni RoRo Terminal (Berth 0), General Cargo Terminal (Berth 1-4) na Container Terminal ( Berth 5-7)

Ukibisha jambo uwe na data mpuuzi wewe!
 
Watanzajia siyo wakatoliki, nchi yetu haina dini, huo waraka wao wawaandikie waumini wao waache ulevi, uzinzi na ushirikina. Waachanane na mambo yahusuyo uendeshaji wa nchi, ya kwao yenyewe yamewashinda, hilo ni baraza la kiinjili
Swali Rahisi kwako:
Kama umeusoma waraka huo Kuna provision yoyote ambayo imeandikwa Kwa muktadha wa kidini au ukiitaka serikali izingatie matakwa ya kidini au kanisa Katoliki?

Kama hujausoma usicoment utadhihirisha ujinga wako.

Baraza la Maaskofu linaundwa nà Maaskofu ambao ni Watanzania, wanaaongoza waumini wa kanisa Katoliki Tanzania. Hivyo logically Maaskofu wanaongoza sehemu ya watanzania, na sio watanzania wote!
Watanzania ni wananchi wa Tanzania wanaostahili haki za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Maaskofu wametoa waraka kama viongozi wa kanisa Katoliki Tanzania ambapo Kuna watanzania wanaostahili haki za kiuchumi, na katika mkataba wa Bandari Kuna athari za kiuchumi Kwa watanzania bila kujali dini zao au kama hawana dini kabisa!

Kimsingi kisu kimegota mfupani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…