Baba mkwe Shahidi wa Yehova kakataa mahari ya pesa, anataka apelekewe magovi matano ya watu wazima

Naogopa hata kuunganisha nao ukoo. Yaani yule mzee awe mzazi mwenza wetu???
Inafikirisha sana aisee
 
Hapo tayari wameshatangaza vita. Kijana akutane na binti wapate mtoto maisha yaendelee. Wazee wanakuwa wadwanzi kama nini.
 
Umefanya kosa kubwa sana kuwachafua mashahidi wa Yehova na uchafu/uongo uliouandika hapa kwenye hii forum.

Laiti ungejua ukubwa wa kosa ulilolifanya ungeomba moderators waufute uzi huu. Story yako haina ukweli wowote ule. Hakuna shahidi wa Yehova yeyote ambae anaweza kufanya hicho ulichosema.

Mimi nimesharipoti huu uzi ufutwe kwa sababu umelenga kuwachafua mashahidi wa Yehova, hauna maana yoyote nyingine zaidi ya hiyo.
 
Tukutane tar 18 sep mwaka gani huo? 2020
 
Inawezekana ni kweli na nibwa imani hiyo lkn huo ni msimamo hauusiani na dini. Ila kwa vile dini hyo ni watata... Mshenga akaunganisha matukio
 
Tukutane tar 18 sep mwaka gani huo? 2020
Ukisoma tarehe ya juu, mwanzo wa barua ni mwaka 2022. Huo mwaka wa ndani ya barua nadhani ni makosa tu ya kiuandishi, hasa ukizingatia umri wa mwandishi ni mtu mzima sana.
 
Reactions: Ok9
Kiufupi,
Ni Familia ya kichawi hiyo mkuu,
Ushauri wangu: usioe Hapo,utajuta
Hilo ndio azimio letu. Hata bwana mdogo tume mshauri aachane na huyo binti, kwani hata wakisema wazae bila ndoa, atakuwa anauunganisha ukoo na watu wa ajabu.
 
Kuandika Baba Mkwe Shahidi wa Yehova sio kosa. Wala sijasema Mashahidi wa Yehova hawapokei mahari nyingine isipokuwa magovi.

Nimemuongelea mtu mmoja na mawazo yake.

Sasa kama wewe ni Shahidi wa Yehiva unayehisi umeumizwa hisia zako kwa uzi wangu huu, nenda katangulie mahakamani ili uipate haki yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…